Tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano

I beg to differ !
 
Upuuzi mtupu uliouandika jambo tunalolipata ni Ile asilimia 4 yetu ambayo mlitunyonya miakaa yote hiyo sitini ya muungano ambayo ilikuwamo katika makubaliano yetu ya muungano.
 
Best option ni kuvunja muungano,huu ndo muungano wa hovyo duniani
 
Upuuzi mtupu uliouandika jambo tunalolipata ni Ile asilimia 4 yetu ambayo mlitunyonya miakaa yote hiyo sitini ya muungano ambayo ilikuwamo katika makubaliano yetu ya muungano.
Kuwa na dhana kwamba Tanzania bara inainyonya Tanzania visiwani ni sawa na kusema ndama ananyonyesha mama yake. Haiwezekani hata ungejaribu vipi.
 
Inshort tanganyika tume pigwa..na ni makosa Rais wa Tanzania awe kutoka Zanzibar ni uwendawazimu
 
Inajua ndo itakuwa mwisho wa muungano,maana wananchi wengi kwa pande mbili za muungano hawautaki huu muungano wa kulazimishana unaolindwa na dola kwa amri ya viongoz wachache,but l have a dream kwamba sku moja tusioijua muungano huu utakufa naTanganyika itaibuka tena,kila jambo lina mwisho
 
Sio kweli ht kdg,kama walikuwa na lengo hilo kwann hawakuichukua comoro ambayo ni kisiwa kipo krb na Tz?
 
Hamna mtu mwenye akili anataka huu muungano kwa sababu una masumbufu mengi mno na chokochoko za watu wasiostaarabika. Kuna wengine hatuzitaki kabisa. Wakae na utumbatu yao. Tuseme ukweli, mtu kama mimi, common man on the street huku bara, muungano unanisaidia nini? Mtu yeyote wa bara, muungano unamsaidia nini? Halafu kila siku wale wanaonufaika zaidi na muungano ndio walalamishi wakubwa. Nyerere aliwaambia mnakuwa kama mtoto mchanga, mnajinyea, halafu tukitaka kuwatawaza msinuke nyie ndio mnalia, bado hawakuelewa.
 
Malalamiko ya muungano yapo toka G55, lakini walioshikilia nchi hawataki mabadiliko yoyote, Wana nguvu na watu wa kutetea muungano vyovyote ulivyo, matumaini ni kidogo, labda Mungu mwenyezi aingilie Kati, bila shaka mama anajua hizi fursa huwa hazijirudii, hawezi fanya makosa, ni zamu yao zenji, na ni zamu yao kwelikweli
 
Sio kweli ht kdg,kama walikuwa na lengo hilo kwann hawakuichukua comoro ambayo ni kisiwa kipo krb na Tz?
Comoro hatukuungana nayo lakini ilikuwa chini ya control ya Tanzania. Kuna wakati hata jeshi letu lilikuwa pale na kata kuna mapinduzi ya kijeshi yalizimwa na Tanzania. Hivyo tulikuwa na makubaliano ambayo yalifafanya tuwe salama. Nyerere hakuwa mtu mdogo bwana, alikuwa ligi kubwa yule sio mtu wa kusimamia mambo ya vijiweni kama raisi

Hata hapa juzi tu tulienda huko. Wanaongea kiswahili pia na vitu vyao vingi vinatoka Tanzania

On March 25, 2008, military forces of the Union of the Comoros, supported by African Union (AU) troops from Tanzania, Sudan and Senegal, landed on the Comorian island of Anjouan. They met little resistance and took control of the island quickly in order to topple the regime of renegade Anjouan strongman Mohammed Bacar. He had ruled Anjouan legally and illegally, initially coming to power in an island coup in 2001, then being elected Anjouan’s president in 2002, and since 2007 refusing to step down with the expiration of his five-year mandate.
 
Wa kulaumiwa ni jiwe. Jiwe ndiye muasisi wa upuuzi huu wa kuipendelea kwao na wa kwao..

Mama Samia anafuata nyayo ,za dikteta.
 
Comoro hatukuungana nayo lakini ilikuwa chini ya control ya Tanzania. Kuna wakati hata jeshi letu lilikuwa pale na kata kuna mapinduzi ya kijeshi yalizimwa na Tanzania.
Acha uwongo. Comoro haijawahi kuwa chini ya control ya Tanzania. Jaribio la Mapinduzi ya kijeshi nchini humo kuzimwa na JWTZ ilikuwa ni maombi maalumu kama ilivyokuwa kwa Uganda chini ya Obote
 
Wa kulaumiwa ni jiwe. Jiwe ndiye muasisi wa upuuzi huu wa kuipendelea kwao na wa kwao..

Mama Samia anafuata nyayo ,za dikteta.
Unajua uko very right. Lakini kama raisi Samia anapendelea Zanzibar, anapaswa kuwa na busara ya kuelewa kwamba mazingira ya Magufuli kupendelea Chato ni tofauti sana na mazingira ya Samia kama raisi kupendelea Zanzibar. Asipoelewa hilo basi tuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhani.
 
Acha uwongo. Comoro haijawahi kuwa chini ya control ya Tanzania. Jaribio la Mapinduzi ya kijeshi nchini humo kuzimwa na JWTZ ilikuwa ni maombi maalumu kama ilivyokuwa kwa Uganda chini ya Obote
Sawa, Comorro haijawahi kuwa chini ya control ya Tanzania. Officially. Wewe ulitaka tuitangazie dunia, jamani eeh, Comoro iko chini ya control yetu.

Unapopinduliwa, na kurudishwa madarakani na raisi wa nchi nyingine, unafikiri hutakuwa chini ya control yake?

Au Uganda ya Lule, Binaisa, haikuwa chini ya control ya Tanzania? Ongeza elimu uelewe siasa zinavyoenda
 
Tuna muungano wa kinyonyaji na usio na usawa. Katika hili waasisi walitukosea sana. Ni wakati muafaka wa kuupitia upya muundo wa muungano na ikiwezekana kuuvunja kabisa. Tanganyika inahitaji mtetezi.
 
Na hapo ndipo raisi Samia anatakiwa kuwa mwangalifu sana. Hii kufanya mambo kwa kuifanya Zanzibar iwe zamu yao kwelikweli ndio kutaharibu mambo vibaya sana, labda kama mission yake ndio hiyo, huwezi kujua. Kuna watu wanamwangalia tu, hawasemi kitu ila wanaona, na wana uwezo wa kufanya kitu.
 
Kwanza hawezi maana Urais ni taasisi

Pili Tanzania Bara Tanganyika wanachukua pesa ya Zanzibar zaidi ya bil.400 Kila mwaka.
Eti Urais ni taasisi! Kichekesho hiki. Maana katiba inampa Rais umungu mtu, hapo taasisi inakuja vipi!?
 
Eti Urais ni taasisi! Kichekesho hiki. Maana katiba inampa Rais umungu mtu, hapo taasisi inakuja vipi!?
U Mungu mtu wa kufanyaje? Tuna Rais wa kutoa Zanzibar miaka 3 Sasa,huo u Mungu mtu wa kupendelea kwao uko wapi? Thibitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…