tujadiliane sio conclusive statement, Well kwangu navyoona and i am open to be criticised / kuelimishwa ni kwamba :
Huwa nashangaa sana nikiona baadhi (sio wote) waliofunga ramadan wakilalamika swaumu imetaiti (njaa), nina uhakika hawa wanaolalamika (baadhi) hawawezi kutoboa mfungo wa kikristo.
Funga ya mkristo akila saa moja jioni ni mpaka kesho tena saa moja jioni hakuna kunywa maji wala kula, na hata mle hadharani wala hapagawi au kulalamika mnamuingiza tamaa.
Upande wa pili ukila saa moja jioni unaweza kutupia tena mida ya saa nne flani hivi kabla hujalala, hapo bado tena kuna daku la saa kumi alfajiri, ni kama vile ratiba ya lunch inahamia alfajiri na ratiba ya chai kabla ya kulala, cha kushangaza baadhi yao hata wakipiga daku lakini bado wakiona mtu anakula hadharani tayari kuna roho ya kutamani inaingia utasikia wakilalamika "huoni aibu kula hadharani", Zanzibar wameenda mbali zaidi ukikutwa unashushiwa kipigo.