Tukishinda tutamshukuru Mwenyezi Mungu, ila 98% ni Sare ya aina yoyote au tunafungwa Kuanzia Goli 2

Tukishinda tutamshukuru Mwenyezi Mungu, ila 98% ni Sare ya aina yoyote au tunafungwa Kuanzia Goli 2

Ni Mpumbavu Mkomavu tu pekee ndiyo atajiaminisha na Kujidanganya huku akijipa Matumaini mbele ya Klabu Kubwa, Bingwa na Bora Afrika Al Ahly ambayo Thamani tu ya Wachezaji wake Wanne ni Thamani ya Klabu nzima ya Simba SC ambayo hadi leo hii Mohammed Dewji ' Mo ' hajaiweka katika Mfumo wa Uwekezaji kama alivyotakiwa katika Mchakato mzima.
Tuwe na hakiba ya maneno Leo haibu yako tehteheteheeee
 
Sijakulazimisha na Sikulazimishi ukubaliane na nilichokiandika hapa ila sijawahi kuja na Utabiri wangu na usiwe sahihi kama nilivyousema.

Tukishinda hata Mimi nitafurahi mno na Kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ila tusidanganyane Al Ahly ni zaidi ya Simba SC ndani na nje ya Uwanja huku zaidi ikiwa ni katika Ufundi.

Nina uhakika wa Matokeo ya Suluhu (Sare bila ya Magoli) au Sare Pacha (ya Magoli) au Simba SC Kufungwa na Al Ahly goli Kuanzia 2 (Mbili)

Wale mtakaochukia na huu Uzi mnisamehe, tuvumiliane na muupokee tu kwani ndiyo Utabiri wangu kama ambavyo nimekuwa nikiutoa kwa Matokeo mengine mbalimbali yaihusuyo Simba SC yangu (yetu)

Kumfunga Al Ahly Kesho Kiutamaduni (Kiuchawi) Simba SC inatakiwa ifanye Kafara kubwa la Kiongozi wake Mmoja wa Juu Afe ghafla (tena kwa Ajali) na Damu yake itumike. Pia Kucheza huo Mchezo Saa 10 Jioni tumekosea mno kwani Jini la Ushindi la Simba SC huwa linaanza Kufanya Kazi kuanzia Saa 1 Usiku hadi Saa 6 Usiku tu.

Na Safari hii Al Ahly nao wamejidhatiti sana Kindumba (Kiuchawi) japo Wao wanatumia zaidi Kitabu na kuna Jambo wamelifanya Leo na Kesho Saa 5 Asubuhi watalifanya tena. Wamejiandaa mno kwa Fitna za nje ya Uwanja.
Khaaaaaah..... sijui ulikua unawaza nn.... sasa ndo mjue kwa level ya simba sasa... hakuna kudoubt timu yoyoyte na ije 80% matokeo ni mazur
 
Back
Top Bottom