Kiongozi muandamizi wa Hamas, Ismail Haniyeh amesema vikosi vya kivita vya kundi hilo vimejitayarisha vya kutosha kuendeleza vita na Israel kwa muda wowote vita hivyo inakavyochukua.
Katika tamko hilo kiongozi huyo amesifu utayari wa vikosi vya kivita na mikakati mnyumbuliko waliyojitayarisha nayo kabla ya vita hivyo kuanza. Akaongeza kusema ushirikiano na utii wa vikosi hivyo tayari umeleta mafanikio makubwa katika mapambano yao kwani tayari wamefanikiwa wavamizi kutofikia malengo waliyojiwekea kuyatimiza ikiwemo kushindwa kuokoa mateka yeyote na pia kulitia hasara jeshi la IDF katika kupoteza idadi kubwa ya askari na uharibifu mkubwa wa vifaa vyao vya kijeshi.
Ismail Haniyeh akaahidi dunia kwamba itashuhudia Hamas ikiibuka mshindi katika vita hivyo na kulazimisha jeshi la Israel kuiachia Gaza kama walivyolazimika kufanya katika vita baina yao vya mwaka 2005.
Pamoja na ahadi za ushindi, Ismail Haniyeh vile vile alisifu maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao cha dharura cha nchi za kiislamu na jumuiya ya waarabu kilichofanyika Saudi Arabia ambapo alihimiza utekelezwaji wake ili kuharakisha matumaini na kurudisha heshima ya wapalestina.
View attachment 2836038