Tuko tayari kupigana kwa muda wowote vita itakaochukua - Hamas watoa tamko kuadhimisha vita na Israel

Tuko tayari kupigana kwa muda wowote vita itakaochukua - Hamas watoa tamko kuadhimisha vita na Israel

Hili ni tangazo jema sana kwa Israel. Israel inahitaji muda mrefu wa vita Ili kukausha Kila nzi ndani ya Gaza na hatimaye kusimika utawala usio wa kigaidi. Sio kazi ya mda mfupi. Na Adui hajawahi kutamka kuwa ninashindwa.!
Marekani kasema kuanzia mwisho wa mwaka huu atakua hana hela ya kutoa msaada sasa itakuaje?
 
Piganeni fumuaneni ubongo then mshindi ataandika historia upya
 
Sikutegemea jeshi la IDF kwa ubora wao tunaoaminishwa kuchukua miezi zaidi ya miwili kwenye upande wa jimbo moja tuu la Gaza tena kupambana na wanamgambo wasioungwa mkono na wananchi wenzao wa Palestine


Hakika Hamas ni vidume
 
Kiongozi muandamizi wa Hamas, Ismail Haniyeh amesema vikosi vya kivita vya kundi hilo vimejitayarisha vya kutosha kuendeleza vita na Israel kwa muda wowote vita hivyo inakavyochukua.

Katika tamko hilo kiongozi huyo amesifu utayari wa vikosi vya kivita na mikakati mnyumbuliko waliyojitayarisha nayo kabla ya vita hivyo kuanza. Akaongeza kusema ushirikiano na utii wa vikosi hivyo tayari umeleta mafanikio makubwa katika mapambano yao kwani tayari wamefanikiwa wavamizi kutofikia malengo waliyojiwekea kuyatimiza ikiwemo kushindwa kuokoa mateka yeyote na pia kulitia hasara jeshi la IDF katika kupoteza idadi kubwa ya askari na uharibifu mkubwa wa vifaa vyao vya kijeshi.

Ismail Haniyeh akaahidi dunia kwamba itashuhudia Hamas ikiibuka mshindi katika vita hivyo na kulazimisha jeshi la Israel kuiachia Gaza kama walivyolazimika kufanya katika vita baina yao vya mwaka 2005.

Pamoja na ahadi za ushindi, Ismail Haniyeh vile vile alisifu maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao cha dharura cha nchi za kiislamu na jumuiya ya waarabu kilichofanyika Saudi Arabia ambapo alihimiza utekelezwaji wake ili kuharakisha matumaini na kurudisha heshima ya wapalestina.

Hamas says it’s prepared for long war with Israel


View attachment 2836038
Hahaha, anayasema hayo akiwa kwenye uwanja wa vita au akiwa Beirut ! Mjinga sana rudi Gaza ukafe na wenzio, watoto wanakufa wanawake wanakufa , makumi kwa mamia ya wapiganaji wa Hamas wanajisalimisha .
Muoga wewe.
 
Hahaha, anayasema hayo akiwa kwenye uwanja wa vita au akiwa Beirut ! Mjinga sana rudi Gaza ukafe na wenzio, watoto wanakufa wanawake wanakufa , makumi kwa mamia ya wapiganaji wa Hamas wanajisalimisha .
Muoga wewe.
Usiwe na hasira.Hakuna Hamas anayeogopa kufa akaishi kama mnyama.Huyu wenzake wamemridhia abake huko na faida zaidi kuliko kuwepo Gaza.
 
Back
Top Bottom