Tuko tayari kupigana kwa muda wowote vita itakaochukua - Hamas watoa tamko kuadhimisha vita na Israel

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kiongozi muandamizi wa Hamas, Ismail Haniyeh amesema vikosi vya kivita vya kundi hilo vimejitayarisha vya kutosha kuendeleza vita na Israel kwa muda wowote vita hivyo inakavyochukua.

Katika tamko hilo kiongozi huyo amesifu utayari wa vikosi vya kivita na mikakati mnyumbuliko waliyojitayarisha nayo kabla ya vita hivyo kuanza. Akaongeza kusema ushirikiano na utii wa vikosi hivyo tayari umeleta mafanikio makubwa katika mapambano yao kwani tayari wamefanikiwa wavamizi kutofikia malengo waliyojiwekea kuyatimiza ikiwemo kushindwa kuokoa mateka yeyote na pia kulitia hasara jeshi la IDF katika kupoteza idadi kubwa ya askari na uharibifu mkubwa wa vifaa vyao vya kijeshi.

Ismail Haniyeh akaahidi dunia kwamba itashuhudia Hamas ikiibuka mshindi katika vita hivyo na kulazimisha jeshi la Israel kuiachia Gaza kama walivyolazimika kufanya katika vita baina yao vya mwaka 2005.

Pamoja na ahadi za ushindi, Ismail Haniyeh vile vile alisifu maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao cha dharura cha nchi za kiislamu na jumuiya ya waarabu kilichofanyika Saudi Arabia ambapo alihimiza utekelezwaji wake ili kuharakisha matumaini na kurudisha heshima ya wapalestina.

Hamas says it’s prepared for long war with Israel

1701977678942.png
 
Vita imepamba Moto Mkuu.

NATOA RAI, ACHENI KUMWAGA DAMU ZA WASIO NA HATIA.
Ni ahadi ya Mungu wale wote na ndugu zao wakomba dua hujibiwa kwa muda na wakati anaopenda.Muhimu dua zao hazirudi nyuma.
 
Kiongozi muandamizi wa Hamas, Ismail Haniyeh amesema vikosi vya kivita vya kundi hilo vimejitayarisha vya kutosha kuendeleza vita na Israel kwa muda wowote vita hivyo inakavyochukua.

Katika tamko hilo kiongozi huyo amesifu utayari wa vikosi vya kivita na mikakati mnyumbuliko waliyojitayarisha nayo kabla ya vita hivyo kuanza. Akaongeza kusema ushirikiano na utii wa vikosi hivyo tayari umeleta mafanikio makubwa katika mapambano yao kwani tayari wamefanikiwa wavamizi kutofikia malengo waliyojiwekea kuyatimiza ikiwemo kushindwa kuokoa mateka yeyote na pia kulitia hasara jeshi la IDF katika kupoteza idadi kubwa ya askari na uharibifu mkubwa wa vifaa vyao vya kijeshi.

Ismail Haniyeh akaahidi dunia kwamba itashuhudia Hamas ikiibuka mshindi katika vita hivyo na kulazimisha jeshi la Israel kuiachia Gaza kama walivyolazimika kufanya katika vita baina yao vya mwaka 2005.

Pamoja na ahadi za ushindi, Ismail Haniyeh vile vile alisifu maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao cha dharura cha nchi za kiislamu na jumuiya ya waarabu kilichofanyika Saudi Arabia ambapo alihimiza utekelezwaji wake ili kuharakisha matumaini na kurudisha heshima ya wapalestina.

Hamas says it’s prepared for long war with Israel

View attachment 2836038
Hilo tamko wameitolea wapi? alafu alwaz hizi akili ndogo zako acha kutuletea ujinga wenu humu bhana
 
Kama hilo tamko ni kweli basi narudia tena kusema adui wa kwanza wa Palestine ni Hamas. Akili kisoda halafu hayajifunzi kabisa. Wacha wafundishwe adabu
 
Kiongozi muandamizi wa Hamas, Ismail Haniyeh amesema vikosi vya kivita vya kundi hilo vimejitayarisha vya kutosha kuendeleza vita na Israel kwa muda wowote vita hivyo inakavyochukua.

Katika tamko hilo kiongozi huyo amesifu utayari wa vikosi vya kivita na mikakati mnyumbuliko waliyojitayarisha nayo kabla ya vita hivyo kuanza. Akaongeza kusema ushirikiano na utii wa vikosi hivyo tayari umeleta mafanikio makubwa katika mapambano yao kwani tayari wamefanikiwa wavamizi kutofikia malengo waliyojiwekea kuyatimiza ikiwemo kushindwa kuokoa mateka yeyote na pia kulitia hasara jeshi la IDF katika kupoteza idadi kubwa ya askari na uharibifu mkubwa wa vifaa vyao vya kijeshi.

Ismail Haniyeh akaahidi dunia kwamba itashuhudia Hamas ikiibuka mshindi katika vita hivyo na kulazimisha jeshi la Israel kuiachia Gaza kama walivyolazimika kufanya katika vita baina yao vya mwaka 2005.

Pamoja na ahadi za ushindi, Ismail Haniyeh vile vile alisifu maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao cha dharura cha nchi za kiislamu na jumuiya ya waarabu kilichofanyika Saudi Arabia ambapo alihimiza utekelezwaji wake ili kuharakisha matumaini na kurudisha heshima ya wapalestina.

Hamas says it’s prepared for long war with Israel

View attachment 2836038
MashaAllah
 
Hata Netanyahau aliwahi kusema Vita vitakuwa vigumu na vitachukua muda mrefu lakini tutashinda!
Kwa hiyo siyo taarifa ngeni!
 
Sasa mbona una hasira ?😂
Kila jambo linalofanyika linakupa nafasi ya kujifunza. Mtu yupo kibarazani kwako anafanya uharibifu ameshaweka vikwazo vingi, amesababisha umepoteza raia wako kibao na wengine waliobaki wanaishi kwa tabu bado unayo courage ya kusema utapambana naye kisa una mateka umewashikiria. Unamkomoa yeye unawakomoa raia wako wewe?

Sielewi ni wapi pakunifanya nikasirike kwa watu wenye akili kisoda. Acha wanyooshwe
 
Wewe ndio unaakili hiyo ya kuwaza uharibifu , kupoteza raia wengi Sijui vikwazo .wao wanapigania uhuru wao wa ardhi yao na taifa lao kama wanavyopigana IDF kutetea uhuru wao na taifa lao.
Hahaa wananyooshana hiyo ni vita bro.
 
kwa hili tamko Hamas hawajali lolote kuhusu Raia wa palestine kwa kifupi hawajali lolote kuhusu maisha yao pia

imagine mtoa matamko yupo Qatar kwenye five stars hotel akichochea moto uwake Zaid Gaza na wajinga walio Meza tu vifungu tuchache twa dini wanaenda front na kusababisha uhalibifu na mauaji kwa kina mama na watoto wa palestine wasio na hatia
 
Hili ni tangazo jema sana kwa Israel. Israel inahitaji muda mrefu wa vita Ili kukausha Kila nzi ndani ya Gaza na hatimaye kusimika utawala usio wa kigaidi. Sio kazi ya mda mfupi. Na Adui hajawahi kutamka kuwa ninashindwa.!
 
Back
Top Bottom