Mleta mada hamjamjua ana nia gani.
Hawezi kutifundisha umahiri wa mbowe, zaidi ya hayo Mbowe ni mwanasiasa mvumilivu na mwenye busara, Mbowe ni zao la kile kilimo kizuri cha CCM asilia ya Hayati Mwalimu Nyerere.
Mleta mada anafikiria kumsifia leo, ataweza kuleta taharuki ndani ya wana CDM, ili mzozo uanze hapa na watu waseme asiachie kamba.
Sisi wana ccm asilia, tunajua fika kuwa Mbowe ni mtanzania kwanza na CDM hufuatiya.
Chadema wafanye yao bila ya kuongiliwa, tumuombe mola awape busara na hekima, wafanye uchaguzi wa maana, kitakacho endeleza chama chao.
Tanzania inahitaji sana chama cha upinzani makini, chenye busara na chupavu.