Tukubali tukatae, mtu kuwa na Tattoo ni kielelezo cha malezi mabovu

Tukubali tukatae, mtu kuwa na Tattoo ni kielelezo cha malezi mabovu

Tukubali tukatae, ukiona mtu ana tattoo yoyote ujue ni matokeo ya malezi mabaya.

Tattoo ni ishara ya mtu kutokujijali, kutojali afya wala thamani ya mwili wake na pia kutokutumia akili sawasawa.

Ndio maana China kwa ajili ya kulinda kizazi cha sasa na kizazi cha baadae imepiga marufuku ukengeufu na kuzuia watu kutokuchora tattoo. Sio China tu, nchi nyingi sasa zimeshaanza kuona kwamba tattoo ni mwenendo mbaya kwa jamii hivyo kuanza kuzipiga marufuku.

Ukiangalia, huwezi kukuta familia zinazojielewa na zenye heshima katika jamii kama wanasiasa, wafanya biashara wakubwa, wanasayansi, wasomi nk watoto wao ama wao wenyewe wamechora tattoo. Na hata kama ikitokea alichora kwa bahati mbaya akiwa mdogo, lazima utakuta anaificha sana isionekane katika jamii. Sababu ya kufanya hivyo ni moja tu kwamba tattoo ni ishara ya malezi mabaya ama tabia mbaya.

Huku Afrika hasa Tanzania ambako usimamizi wa maadili na mwenendo mwema katika jamii imeachwa kwa mtu binafsi, vijana wengi huona kuchora tattoo ni ufahahari kua kama Messi ama 50 Cents.

Tulinde kizazi chetu cha sasa na cha baade kutoka kwenye uharibifu huu wa Tattoo, tueleze vijana tattoo sio jambo jema na sio ufahari, ni ujinga.

Huo ni mtazamo wako tu,huwezi kutuaminisha kwamba kuchora tattoo ni tabia mbaya kuliko kudanga,ulevi,uvivu,wizi,nk.
Miaka ya 90 ilikuwa ni ajabu sana na watu walikushangaa wakiona mwanaume amesuka raster!!(ukiacha wamasai).
Leo hii hata kanisani unaingia tu na raster zako bila shida,kilichoonekana hakifai miaka 30 iliyopita,leo kinakubalika vzr kwenye jamii.
 
Mjomba alichora nanga ya meli mkono wa kulia enzi za ujana wake.Sasa hivi tena kawa mtu mzima ile tattoo anaichukia na anaikava na mashati marefu. Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunakula akaniambia "husithubutu kuchora tattoo mimi sasa hivi inanitesa........".
 
Ila watu wengi waliochora hizo tattoo huwa Wana tabia mbovu sana hata kwa jamii na huharibikiwa akili, na hata wengi huumwa na kushauriwa watoe hizo tattoo maana Zina mapepo mengi
vitu vingine ni upotofu wa imani tuu, mbona wanawake wengi tuu mna mapepo ya kutosha na tattoo hamjachora?. Kila mkutano wa injili wa kuanguka mapepo ni nyie tuu.

Mbona madangaji mengi, malaya, mashoga na wezi hawana tattoo na bado wanatabia mbovu.

usisingizie tattoo, chora tattoo usipo chora, kama una matatizo au tabia chafu ni unazo tuu.
 
Watu wengi? Wangapi?

Watu wengi? Wangapi?

Punguza kuongea kitu usichokijua, unaongea kwa mihemko tu.

Mapepo unayajua? Au sababu umekutana na vichaa wavuta bangi uko mtaani Basi unadhani Kila mchora tattoo yupo hivyo?
futa hiyo tattoo wewe ni wa hovyo
 
Huwezi amini kama uliotoa mada hii kama wewe ni Mkristo basi napaswa kukwambia kuwa, Hatawaliokuletea dini na wanaotoa misaada ya dini ni wenye hizo Tattoo. Kama unabisha tembea kwenye nchi kama USA na Huko bara la Ulaya.

Tataizo linakuja pale unapokutana na mwenye Tattoo kwa mara ya kwanza na akakufanyia uhuni, ndio hapo unapokuja dhana jumuhishi kuwa wenye tattoo ni shida.

Lakini pia unapaswa kujua Tattoo ni kitu gani na wapi kilianzia..?
Binafsi sina hiyo tattoo , lakini naheshimu sana watu wenye uhuru na maisha yao. Wengi hutamani hizo tatto shida ni kwamba wengi wanahofia kukosa kazi na masuala mengine.

Wapo Watu hawana hizo Tattoo lakini wana mambo ya ovyo na wenye kujaa dhambi kuliko hata Lil Wayne mwenye tattoo zake.

Huna tattoo lakini kichwan una mawazo ya kishetani, lakini yupo ,wemye tattoo kama Mess anasaidia watu wengi huko nchini kwako, sasa hapo kipimo cha maadili ni kipi?

Kiasili hatuwezi kuwa sheris moja itakayosimamia dunia nzima, tuache kuhukumu watu, inawezekana ndugu yako hana maadili huko lakini sio watu wote.

Tabia za mtu hazifafanuliwi kwa tattoo, shida tu huku kwetu hatuna uhuru tunaishi ishi tu kwa kuhofia kukosa kazi.

Yangu ni hayo!
 
Mi tattoo niliyochora ni hii hapa sina baya unyama ni mwingi sana blood.
Screenshot_20191026-014551.jpg

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Tukubali tukatae, ukiona mtu ana tattoo yoyote ujue ni matokeo ya malezi mabaya.

Tattoo ni ishara ya mtu kutokujijali, kutojali afya wala thamani ya mwili wake na pia kutokutumia akili sawasawa.

Ndio maana China kwa ajili ya kulinda kizazi cha sasa na kizazi cha baadae imepiga marufuku ukengeufu na kuzuia watu kutokuchora tattoo. Sio China tu, nchi nyingi sasa zimeshaanza kuona kwamba tattoo ni mwenendo mbaya kwa jamii hivyo kuanza kuzipiga marufuku.

Ukiangalia, huwezi kukuta familia zinazojielewa na zenye heshima katika jamii kama wanasiasa, wafanya biashara wakubwa, wanasayansi, wasomi nk watoto wao ama wao wenyewe wamechora tattoo. Na hata kama ikitokea alichora kwa bahati mbaya akiwa mdogo, lazima utakuta anaificha sana isionekane katika jamii. Sababu ya kufanya hivyo ni moja tu kwamba tattoo ni ishara ya malezi mabaya ama tabia mbaya.

Huku Afrika hasa Tanzania ambako usimamizi wa maadili na mwenendo mwema katika jamii imeachwa kwa mtu binafsi, vijana wengi huona kuchora tattoo ni ufahahari kua kama Messi ama 50 Cents.

Tulinde kizazi chetu cha sasa na cha baade kutoka kwenye uharibifu huu wa Tattoo, tueleze vijana tattoo sio jambo jema na sio ufahari, ni ujinga.

Umefanya jumla mno Mkuu, wengine siyo malezi ni watu wazima kabisa wenye maamuzi binafsi. Hivyo kuwasema walezi wake ni kuwaonea.
 
Sasa watu hawajachanja?. 90 ya watanzania wana chale,iwe kwa ajili ya matibabu,kwa asili au vyovyote. Makabila mengine ndio kabisa hakuna anaekosa chale. Kama wamakonde,wabondei,wasukuma. Wengi wasichana pia wametoboa masikio pia.

Biblia ukiingia kiundani sana utachanganyikiwa. Kuna kifungu kitakukubalia jambo fulani,vile kipo kitakachokukataza jambo hilo hilo.

Mwisho ni kwamba sioni tatizo kwa mtu kuchora tatoo kama tu hiyo tatoo ameichora kama urembo. Tatoo isiyo na maagano yoyote mbele za MUNGU ni sawa na mwili uliopambwa tu.

Tusitoe hukumu hapa duniani. MUNGU atamhukumu mtu kuringana na matendo yake. Sioni tatizo kwa wenye tatoo zisizo na maagano.

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom