Tukumbuke kisa hiki cha msanii Noorah na Fiesta

Tukumbuke kisa hiki cha msanii Noorah na Fiesta

NOORAH Kitandani…..FIESTA Uwanjani!!

Japo muda kidogo umepita tangu utokee huu mkasa lakini sio mbaya tukikumbushana hii kitu. Jinale halisi ni Haji Nurah Ngarama almaarufu kama ‘Noorah’ au Baba Stylz.

Mwaka 2005 Noorah mwanachemba Squad alipata bahati ya kushiriki kwenye tamasha la Fiesta. Sasa akiwa katika hiyo Tour ya Fiesta alipata ajali mbaya sana,angalau kwa kipindi hicho ajali haikutangazwa sana kama kulivyotangazwa kufana kwa show hizo.

Noorah alipata ajali akiwa kazini. Baada ya kwenda hospital daktari akasema hatakiwi tena sio tu kufanya show bali hata kufanya kazi yoyote ngumu. Hapo ndipo mtihani kwa MwanaChemba huyu ulipoanzia.

Noorah akaona hapana, sasa ntaishije aisee? Akaamua kujivuta hadi muhimbili kwa uchunguzi zaidi ndipo ndipo ilipogundulika kuwa ajali ile imesababisha sehemu ya fuvu la kichwa chake kupata ufa.

Daktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili akashauri kwamba sio tu kutofanya kazi ngumu bali mgonjwa huyo anatakiwa apumzike kabisa. Hakuwa na namna Noorah akapumzika na kuwa baba wa nyumbani.

Noorah akapumzika lakini show za Fiesta ziliendelea na zingalipo zinaendelea mpaka leo, kwao yaliyotokea kwa Noorah ni kama ajali kazini tu. Hapo kwenye ajali kazini ndipo hasa kwenye mzizi wa matatizo. Kwanini ajali kazini kwa wasanii hazina bima? Mikataba karibia yote ya wasanii haizungumzii wasanii watafidiwaje wakipata ajali ya kupelekea ulemavu/ugonjwa/kufariki wakiwa kazini. Mikataba mingi haitambui show kama nazo ni kazi iwe ya muda mfupi au mrefu. Kuburudisha kunachukuliwa juu juu tu.

Katika wimbo NSSF Mbeleni wimbo unaopatikana katika mixtape za Anti Virus, Mapacha walizungumzia hii kitu. Nini mustakabali wa msanii katika maisha yake ya baadae? Hii sio kwa Noorah tu bali wengi wanakutana na changamoto kama hizi wakiwa kwenye mikataba ya kazi.

Noorah alikaa nyumbani mpaka alipoona sasa inatosha,akaamka na kwenda shule pale IFM na baadae akarejea tena kwenye muziki ingawaje haikuwa kama zile zama akiwa katika ubora wake.
Na Iddy Mwanaharam
habari toka kwenye kipande kidogo sana na chakavu cha gazeti la UWAZI
 
ugali? ugali upi? kuja hapa na kukuzodoa ulivyotaka kuwapotosha watu ndio unasema natetea ugali

ndio huwa kimbilio la akili ndogo mnaposhindwa kwa hoja..

leo imeshindikana kupotosha uma... umeleta kitu ambacho kipo well known alafu wewe unataka kupindisha ukweli
MBONA Husemi Noorah Alipata ajali wapi ili h ukweli wenu uwe na ushahidi?
ILA Endelea kuwa Wakala wa Shetani,
SIKU ya Hukum yaja
 
Noorah hakupata ajali kazini mzee au labda kama alikuja kupata ajali nyingine baadae...ninayoikumbuka alikuwa anatoka zake batani na mashorty...tena shorty moja alifariki
mashorty ndo manani ayo?
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tuseme labda ni kweli alipata ajali kwenye fiesta, hata angepata ajali akiwa jukwaani anaperform kama hiyo ajali haikusababishwa na uandaaji mbovu wa tamasha au uzembe kwenye kuandaa jukwaa bado tusingeliwalaumu clouds.

Mtoa mada umeunganisha vitu vingi sana kisheria ambavyo ni tofauti. Mtoa mada unaunganisha insurance na social security kwenye kapu moja wakati hivi ni vitu tofauti.

Umeongelea bima (insurance), hii mtu binafsi anajikatia bima kwamba akipata risk fulani kampuni ya bima (insurer) wamlipe na huwa inalipiwa premium kila baada ya muda Fulani, sijui ulitaka huyo msanii akate bima kwa janga gani ulemavu au ajali? Je alikuwa na bima? Je ni kazi ya clouds kuwakatia bima wasanii?

Unazungumzungumzia NSSF hiyo tayari ni social security, mwajiriwa anakatwa pesa zake kila mwezi ili akistaafu apate mafao yake, na akipata ulemavu anapewa fao la ulemavu. Pia siku hizi social security laws zipo wazi mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii hata kama haujaajiriwa umejiajiri kwenye kilimo au muziki unarihusiwa kujiunga ambapo unakokotolewa kiwango kutokana na kipato chako unakuwa unacontribute kila mwezi.

Tukirudi kwenye hoja je ulitaka huyo msanii alipwe na nssf? Je alikuwa memba? Je ni kazi ya clouds kumuunganisha kwenye mfuko?

Swala lingine lililokuchanganya ni aina ya mikataba ya wasanii kuperform, unatakiwa ujue kuwa kuna contract of service na contract of employment sheria za wafanyakazi zinawalinda watu walio kwenye contract of employment kama labda mchomvu au Dozen angepata hiyo ajali akiwa kazini angelipwa na mwajiri halafu siku hizi kuna mfuko unaitwa OSHA ambao ndiyo kazi yake, waajiri wote wanacontribute kwenye huo mfuko.
Msanii anapoitwa kwenye show hapewi contract of employment anapewa contract of service, analipwa kwa kazi yake akishaperform akalipwa mkataba kwisha, kiufupi wanaitwa independent contractors.

Sioni popote ambapo waandaaji wa fiesta walikuwa na wajibu kwa huyo msanii wako na hata wangemsaidia ingekuwa hisani sawa na kumchangia ombaomba barabarani.
Mkuu siyo OSHA ni WCF
 
SIKUMBUKI KAMA AJALI YA NOORAH ILIKUWA NA UHUSIANO NA FIESTA

NOORAH hakupata ajali akiwa kazini alipata ajali akiwa na demu wake (sandra)

nakumbuka gari ilikuwa rav 4 huyo demu wa noorah alikuwa anasoma Kenya na alikuja tanzania bila kwao kujua

lengo lilikuwa kumuona bwana ake akiperfom sasa baada ya noorah kumaliza show yake wakawa wanarudi wote wamelewa na wako speed ulitokea ubishani

maana noorah alikuwa anataka kumrudisha yule demu kwao(oysterbay) na yule demu hataki kurudi kwao maana nyumban kwao walikuwa wanajua yupo shule Kenya

katika mabishano huku gari ikiwa speed yule demu aliisukuma gear kwenye parking

kana ujuavyo gari za zaman hazikuwa na sensor za kutema gear ya packin gari inapokuwa speed kali basi ilifanya tairi zote nne kufunga ghafla na gari ilibingirita mara nane

noorah hakufunga mkanda alitupwa nje ya gari na akapata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu alikuwa anamkumbuka huyo demu tu...

na siyo kwamba alijipeleka hospital noorah alitoka eneo la ajali akiwa hajitambui kabisa alikuja kupata fahama akiwa hospital

alikaa sana muhimbili hadi alipokuja kupona na kuendelea na mziki pamoja na masomo (IFM)

hawa jamaa fiesta wana mapungufu yao ila sometimes mnazidisha kuwaonea
Sandra Ringo namkumbuka huyo binti, waliishi pia mjini mtaa wa Nkurumaah kabla hawajahamia mbezi.
 
Najua nachosema kinaukweli toka kwa muhusika....hawa wanaficha ukweli labda wanamaslahi na ukweli huu.
 
Oya babu tale acha kelele basi ushaonekana boya..sasa ulitaka clouds wafanye nn wamlipie hospital kwani huyu mtu mzi a alivyosign mkataba hakuona hayo
Hahah
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tuseme labda ni kweli alipata ajali kwenye fiesta, hata angepata ajali akiwa jukwaani anaperform kama hiyo ajali haikusababishwa na uandaaji mbovu wa tamasha au uzembe kwenye kuandaa jukwaa bado tusingeliwalaumu clouds.

Mtoa mada umeunganisha vitu vingi sana kisheria ambavyo ni tofauti. Mtoa mada unaunganisha insurance na social security kwenye kapu moja wakati hivi ni vitu tofauti.

Umeongelea bima (insurance), hii mtu binafsi anajikatia bima kwamba akipata risk fulani kampuni ya bima (insurer) wamlipe na huwa inalipiwa premium kila baada ya muda Fulani, sijui ulitaka huyo msanii akate bima kwa janga gani ulemavu au ajali? Je alikuwa na bima? Je ni kazi ya clouds kuwakatia bima wasanii?

Unazungumzungumzia NSSF hiyo tayari ni social security, mwajiriwa anakatwa pesa zake kila mwezi ili akistaafu apate mafao yake, na akipata ulemavu anapewa fao la ulemavu. Pia siku hizi social security laws zipo wazi mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii hata kama haujaajiriwa umejiajiri kwenye kilimo au muziki unarihusiwa kujiunga ambapo unakokotolewa kiwango kutokana na kipato chako unakuwa unacontribute kila mwezi.

Tukirudi kwenye hoja je ulitaka huyo msanii alipwe na nssf? Je alikuwa memba? Je ni kazi ya clouds kumuunganisha kwenye mfuko?

Swala lingine lililokuchanganya ni aina ya mikataba ya wasanii kuperform, unatakiwa ujue kuwa kuna contract of service na contract for service sheria za wafanyakazi zinawalinda watu walio kwenye contract of service kama labda mchomvu au Dozen angepata hiyo ajali akiwa kazini angelipwa na mwajiri halafu siku hizi kuna mfuko unaitwa Workers Compensation Fund (WCF) ulioanzishwa chini ya OSHA ambao ndiyo kazi yake, waajiri wote wanacontribute kwenye huo mfuko.
Msanii anapoitwa kwenye show hapewi contract of service anapewa contract for service, analipwa kwa kazi yake akishaperform akalipwa mkataba kwisha, kiufupi wanaitwa independent contractors.

Sioni popote ambapo waandaaji wa fiesta walikuwa na wajibu kwa huyo msanii wako na hata wangemsaidia ingekuwa hisani sawa na kumchangia ombaomba barabarani.
umegundua makosa mangapi katika haya maandiko uliyoandika kwenye Uzi huu?
 
Naona watu wanalazimisha uongo kuwa ukweli ili kutimiza ule msemo wa “ukitaka kumwua mbwa mbatize kwanza jina baya”
 
Back
Top Bottom