Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tuseme labda ni kweli alipata ajali kwenye fiesta, hata angepata ajali akiwa jukwaani anaperform kama hiyo ajali haikusababishwa na uandaaji mbovu wa tamasha au uzembe kwenye kuandaa jukwaa bado tusingeliwalaumu clouds.
Mtoa mada umeunganisha vitu vingi sana kisheria ambavyo ni tofauti. Mtoa mada unaunganisha insurance na social security kwenye kapu moja wakati hivi ni vitu tofauti.
Umeongelea bima (insurance), hii mtu binafsi anajikatia bima kwamba akipata risk fulani kampuni ya bima (insurer) wamlipe na huwa inalipiwa premium kila baada ya muda Fulani, sijui ulitaka huyo msanii akate bima kwa janga gani ulemavu au ajali? Je alikuwa na bima? Je ni kazi ya clouds kuwakatia bima wasanii?
Unazungumzungumzia NSSF hiyo tayari ni social security, mwajiriwa anakatwa pesa zake kila mwezi ili akistaafu apate mafao yake, na akipata ulemavu anapewa fao la ulemavu. Pia siku hizi social security laws zipo wazi mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii hata kama haujaajiriwa umejiajiri kwenye kilimo au muziki unarihusiwa kujiunga ambapo unakokotolewa kiwango kutokana na kipato chako unakuwa unacontribute kila mwezi.
Tukirudi kwenye hoja je ulitaka huyo msanii alipwe na nssf? Je alikuwa memba? Je ni kazi ya clouds kumuunganisha kwenye mfuko?
Swala lingine lililokuchanganya ni aina ya mikataba ya wasanii kuperform, unatakiwa ujue kuwa kuna contract of service na contract of employment sheria za wafanyakazi zinawalinda watu walio kwenye contract of employment kama labda mchomvu au Dozen angepata hiyo ajali akiwa kazini angelipwa na mwajiri halafu siku hizi kuna mfuko unaitwa OSHA ambao ndiyo kazi yake, waajiri wote wanacontribute kwenye huo mfuko.
Msanii anapoitwa kwenye show hapewi contract of employment anapewa contract of service, analipwa kwa kazi yake akishaperform akalipwa mkataba kwisha, kiufupi wanaitwa independent contractors.
Sioni popote ambapo waandaaji wa fiesta walikuwa na wajibu kwa huyo msanii wako na hata wangemsaidia ingekuwa hisani sawa na kumchangia ombaomba barabarani.