Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded."
Julius K. Nyerere

"Freedom to many means immediate betterment, as if by magic. Unless I can meet at least some of these aspirations, my support will wane and my head will roll just as surely as the tickbird follows the rhino."
Julius K. Nyerere

"African nationalism is meaningless, dangerous, anachronistic, if it is not, at the same time, pan-Africanism"
Julius K. Nyerere

"Violence is unnecessary and costly. Peace is the only way."
Julius K. Nyerere

Source: http://thinkexist.com/quotes/julius_k._nyerere/

RIP Nyerere

Love from my heart

Kalenge
 
FMES,
Kenyatta hakuwa na fimbo peke yake. Alikuwa pia na ule mkia wa ng'ombe uliosukwa kwenye fimbo. Wenyewe wanaita whisk. Ningekuwa na hiyo picha nigeiweka hapa.


Hapa Mzee Kenyatta ameshika fimbo pamoja na whisk
Hii ilikuwa 30th March 1965, Akimpa degree ya heshima ya udaktari wa falsafa


 
nimependa sana hii thread kwa kweli inatupa changamoto

Asante kwa picha nzuri.
Je hapa ni wapi? Je ni Ikulu? kusema kweli Mwalimu alikuwa hana makuu, hapa yuko more than relaxed na wananchi wake. Yes, policy zake hazikufanikiwa, lakini kwa mtazamo wangu kama mtu wa watu alijitahidi.
 
Mzeeba,

..nadhani hapo alipokaa Mwalimu ni nje Karimjee Hall.
 

Hii picha imenipa huzuni sana...hayo maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa na nguvu sana.

YAP! Nakubalina na wewe, pia sikuwahi kujua kama maneno haya Mwalimu aliyasema wakati akitoa hotuba ya kwanza siku ya uhuru. Ama kweli Mwalimu alinuia kuwafikisha Watanzania kwenye nchi ya ahadi.
 

Nimejaribu kuangalia tovuti ya TRC nikijua walau ntapata historia kidogo, wapi!!! wao mbali kabisa... ni kuanzishwa TRC 1977. Tutangojea kuandikiwa historia yetu mpaka lini? Tatizo kubwa nadhani (sio kwa serikali tu, hata watu binafsi) hatuna tabia ya kujiwekea kumbukumbu kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Au kwa vile tumezoea kupeana historia zetu kwa hadithi za kusimuliana? Vyovyote vile, tuna takiwa kuandika historia zetu na za taifa letu
 
Vile vile kumbukeni cabinets za kwanza. Hii hapa ni cabineti baada ya uhuru:


Na hii hapa ni cabinet mara baada ya Muungano

Hii ni miaka 40 baadae


Na hii 2008


Je Historia katika huu mtiririko inakuonyesha nini?

Mwenye baraza la wakati wa Raisi Mwinyi na Raisi Mkapa aweke hapa nadhani nachoongelea tutakiona vizuri
 
FMES,

Heshima yako Mkuu.

Kuhusu Nkurumah kuhusika na kuua EAA, ninadhani huenda siyo sahihi kwa sababu jamaa huyu alipinduliwa kutoka madarakani na General Joseph Ankrah mwezi February mwaka 1966, ikiwa ni miaka miwili tangu tuwe na muungano wa Tanzania. East african Community ilizaliwa 1967 wakati Nkurumah hayupo madarakani kabisa. Ingawa EAAC ilikuwapo tangu mwaka 1948 ikiwa inaendeshwa kama branch ya BOAC (British Overseas Airways Corporation), haikuwa mali ya serikali za afrika ya mashariki wakati huo hadi baada kuanzishwa kwa EAC mwaka 1967, ambapo Nkurumah alishaishia kusikojulikana. Kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1972, EAA ilikuwa inaendeshwa vizuri sana wala hakukuwa na matatizo yoyote. Ni katika kipindi hicho walipoweza kununua ndege za jet kama vile Comet na VC10






Matatizo yalianza mwaka 1974 baada ya Amini kuwa madarakani huko Uganda, na vile vile uchumi wa Tanzania kuanza kuyumba pole pole baada ya zoezi la kuhamisha watu kwa nguvu kwenda kwenye vijiji vya ujamaa na hivyo kupunguka kwa uzalishaji wa chakula, jambo lililosababisha kuyumba sana kwa uchumi kufuatia njaa ya mwaka 1974, ndipo Kenya walipodai wawe na sauti kubwa kwenye jumuia ile kwa vile uchumi wao ulikuwa imara. Sasa kuwepo kwa madai haya ya Kenya huku Nyerere na Amini hawakai meza moja ndiko kulikuyumbisha sana jumuia hadi ikafa.


Sote tunaelekea kumoja. Huko nyuma niliwaambia nilikuwa fundi wa kutengeneza magari ya mabua. Je unadhani naweza kufanya kazi hiyo tena kwa leo?
 
FMES,

..Kenya walibakiwa na mali nyingi zipi hizo?

..Makao Makuu ya EAC yalikuwa Arusha.

..pia kulikuwa na msuluhishi wa mgawanyo wa mali za EAC, akiitwa Dr.Victor Umbrich.

..kuna uwezekano Kenya walionekana na ahueni kwasababu uchumi wao ulikuwa imara from the beggining kwasababu za KIHISTORIA.

Kichuguu,

..kwa mtizamo wangu EAC was bound to collapse.

..Tanzania ilikuwa ikinung'unika kutokana na disparity ya maendeleo ya kiuchumi kati yake na wenzake. nitajaribu kukuletea chanzo cha habari hiyo.

..vilevile nadhani Wakenya walikuwa wanataka kuendeleza ile status quo ya kiuchumi iliyoachwa na mkoloni EAC.

..nina wasiwasi kwamba Muungano mpya tunaojaribu sasa hivi utakuwa na matatizo yaleyale ya kama ule uliovunjika.

NB:

..Nyerere pia alikuwa amezidi kumchokonoa Iddi Amini.

..baada ya Obote kupinduliwa akiwa ng'ambo, alikuja na kukaa ikulu ya Tanzania. Nyerere aliendelea kupeperusha bendera ya Raisi wa Uganda kwa kipindi chote Obote alichokaa ikulu ya dsm.

..pia Nyerere ali-host wakimbizi wengi tu waliokuwa wakimpinga Amini na kuwapa mafunzo na misaada ya kijeshi.
 


All this goes back to Cecil Rhodes aliyeakuwa mwanzilishi wa Rhodesia an kuleta ile ambition project the Cairo to Cape Town, exploring and exploiting Africa from one point north the the south point, Cape Town!

Sasa LonRho wao wakaja na Tiny Rowland ambaye kama kumbukumbu zangu ni nzuri, waliwahi kufukuzwa na Mwalimu ingawa walirudi baadaye na wame-invest kwenye mashamba ya Chai!
 
kazi nzuri wakuu......Mimi naomba kama anaweza kujua majina ya hawa vijana walioshika hilo bakuli ambalo mwalimu anachanganya mchanga huo na bado wako hai?mbona sijawahi kusikia wakikumbukwa.......pia hao akina mama kushoto ni akina nani na huyo mzee kushoto anaepiga makofi......
 
Hao walioshika mabakuli ya udongo na hao akina mama inasemekana wako hai. Kama sikosei last week walitwa bungeni wakati mjadara wa muungano unazungumziwa na majina yao yalitoka kwenye one of the papers, nafikiri nipashe. Jaribu kucheck kwenye mtandao wa nipashe for the past week unaweza ukawaona.
 

FMES,
Ni kweli Nkrumah hakutaka EA Federation ifanikiwe kwa sababu hii ingeua
hoja yake ya instant African federation. Hata katika kikao cha OAU 1963 walibishana sana na Mwalimu lakini at the end of the day Nkrumah akaishia kumpigia Mwalimu makofi kwa sababu ya nguvu za hoja zake kuhusu mwungano wa hatua kwa hatua. Lakini khasa khasa aliyeua mipango ya EA Federation alikuwa ni Mwingereza. Mwalimu alikuwa tayari kumpisha Kenyatta awe rais wa kwanza wa Federation. Obote naye alikuwa amekwishakubali. Lakini kwa sababu ya age Waingereza wakatambua kuwa eventually Mwalimu angekuwa kiongozi na hawakumwamini kwa sababu hawakuweza kumtumia kama walivyokuwa wanamtumia Kenyatta. Basi wakamshawishi Kenyatta kuwa asikubali, and that was the end of it.
 


Ni kweli, bado wapo hai.

 

jokaKuu,
Ukweli ni kwamba Tanzania ndiyo ilikuwa common market kwa bidhaa zote zilizotengenezwa Kenya. Na sisi ndio tuliowafungulia mlango wa kuingia katika soko la Zambia na Malawi. Kulikuwa na maelewano kwamba kuweko aina fulani ya parity kati ya hizi nchi tatu, ndio maana mamlaka ya bandari yalihamishiwa Dar na shule ya kuendesha ndege ikahamishiwa Uganda. Lakini uchoyo wa Waingereza kwa kutumia watu kama vile Njonjo, zaidi ya tofauti baina ya Nyerere na Idi Amin, ulichangia zaidi kuivunja EAC. Unakumbuka wakati Nyerere alipofunga mpaka na Kenya nani alikuja kulalamika Tz? Alikuwa ni Mwingereza kwa sababu ya biashara zake za utalii.
 
Ni kweli, bado wapo hai.
Mkuu hapo sijui ni macho yangu hao walioshika vikapu ni wavulana......na hao akina mama wawili wa upande wa kushoto....naona wametajwa watatu tu......
 
Mkuu hapo sijui ni macho yangu hao walioshika vikapu ni wavulana......na hao akina mama wawili wa upande wa kushoto....naona wametajwa watatu tu......

Hapana, walioshika kikapu kile kuna mvulana mmoja na msichana mmoja: msichana yupo upande wa kulia wa Nyerere, wakati mvulana yupo upande wa kushoto wa Nyerere. Nadhani hawa ndio waliokuwa na miaka 16 wakati huo, halafu yule anayeonekana kama mama ambaye yuko mbele kabisa ya picha akiwa amevaa khanga yenye mapambo ya vibuyu ndiye yule mwanamke ambaye alikuwa na miaka 30 wakati huo.
 

Mkuu Jasusi,

Heshima mbele sana, nimewahi kuongea na mkulu mmoja aliyehudhuruia hicho kikako OAU, kule Adis ambako Nkurumah alikuwa amepania sana kuanzisha huo muungano wa Afrika na jinsi alivyokuwa akumuona Mwalimu kama ni tatizo katika hiyo ndoto yake ya kuwa rais wa kwanza wa huo muungano,

Nkurumah alifanya mambo mengi ya aibu sana kwenye hicho kikao, akijaribu kummshusha hadi Mwalimu, lakini Mwalimu hakuonyesha kuwa na wasi wasi naye wala kugombea hiyo power kama Nkurumah alivyofikiri, mkulu aliniambia kuwa katika hiyo kiu ya power Nkurumah alisafiri sana kuonana na Wareno, watawala wa Then Mozambique, katika kutafuta njia za kuiua EAA,

Anyways, ninakushukuru sana mkuu kwa kuweka habari hii sawa, kwa kweli tunakula elimu nzito sana hapa.
 
..Kenya walibakiwa na mali nyingi zipi hizo?

Ninaamini sana kuwa katika kuvunjika kwa EAA, Kenya walituzidi ujanja kwa sababu wao walishapanaga kuiua Jumuiya kabla hata sisi hatujajua nia yao, waliilimbikiza madeni kwa EAA, kwa makusudi ambayo baadaye yalihesabiwa kuwa ni madeni ya Jumuiya, Siku EAA inakufa ndege karibu zote zilikuwa nchini kwao, na hata Treni pia,

Ndio maana hata SADC ilipoanzishwa Tanzania ilituchukua muda sana kujiunga, kwa sababu ambazo tulizisema wazi kuwa baada ya kuumizwa kwenye EAA, hatuwezi kurukia rukia tena miungano au jumuiya, bila ya kuwa na uhakika na tunachofanya,

Tanzania tulikuja kushituka mwishoni sana kuwa tumeibiw ana wa-Kenya, ndio Rais Mwinyi, akamtuma Malecela ambaye alikuwa amewahi kuifanyia kazi sana EAA, kwenda kusimamia mgawanyo wa mali zake na madeni yake, lakini ilikuwa too late, wa-Kenya walikuwa wameshatuzidi akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…