Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


Mkuu, heshima yako. naomba nichomeke tu hapa kuwa Binaisa ni jina moja na sio majina mawili kama unavyoonyesha. Alikuwa ni Godfrey Binaisa, kama sikosei. Asante.
 
Mwenzenu hii picha inanivutia mpaka wa leo.


Sisi tunataka kuwasha mwenge,
tunataka kuwashaa mwengee x2

Na kuuweka juu ya mlima,
mlimaa Kilimanjarao x 2

kuwasha mwengee, kuwasha mwengee,
na kuweeka Kilimanjaro x 2

Umulike hata nje ya mipaka yetu,
Uletee tumaini x 2

Pale ambapo hakuna matumaini,
upendo mahali ambapo pana chuki,
na heshima ambapo pamejaa dharauu x 2





Definitely, Those were the days.....!!!
 
Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.

Mwiba,hio signature yako really sums it all up soo nicely......



... Or WRITE. Zanaki!! Take FIVE, mkuu....! teh teh. Nimecheka. You'v really made my Day! thanx.
 


Compa! Hujatulia, mkuu! Thanx. teh teh teh!
 
Mwenyezi Mungu azidi kuziweka roho ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere & Moringe Sokoine Mahali pema peponi. Amina.....

Asanteni mliotuwekea picha hizi kutuliwaza, i feel like crying!

Hivi kuna ukweli gani kwamba watu WASAFI, MAKINI, WEMA,.... hawana maisha marefu hapa DUNIANI? Au ni kwa sababu ya UCHACHE wao na hivyo MAADUI wao wanapata urahisi kuwamaliza?
 
Kamanda Mkuu FMES, kauzalendo kako kananifurahisha sana. Dont give up!
 
Mkuu Kichuguu,

Heshima mbele sana mkuu, hapo ni Mwanamuziki Mbaraka Mwinshehe "Baba Zole Zole", au kwa jina maarufu "Soloist Natiionally", kama sikosei akiwa safarini Songea na bendi yake mpya ya Super Volcano, baada tu ya kutoka katika bendi yake ya zamani maarufu sana ya Morogoro Jazz, yaani Wana-Sululu Saka Saka na Likembe Mahoka,

Baada ya hiyo ziara ya Songea, alirudi mjini Dar ambako nilimuona akishiriki katika mashindano ya Muziki ya kutafuta nafasi ya kuliwakilisha taifa letu katika Maonyesho Ya Mtu Mweusi, yaliyofanyika Mjini Lagos in the 70s, nakumbuka ingawa nilikuwa mdogo lakini nilihudhuria sana mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika katika Uwanja Wa Mnazi Mmoja, saaa za jioni baada ya kutoka Shuleni. Bendi ya Afro 70 na Patric Balisidya, ndiyo iliyoshinda na kupewa nafasi hiyo ya kwenda Lagos, ambayo ndio hasa iliyokuwa safari yao ya mwisho katika ulimwengu wa muziki.

Marehemu Mbaraka Mwinshehe, na Mpiga Ngoma RIP Morris Nyunyusa, hawa walikuwa ndio wawakilishi wakubwa wa taifa letu, kwenye maonyesho mbali mbali ya sanaa ya kimataifa na walilitangaza sana jina la taifa letu huko, hasa mwaka 1970 walipokwenda kutuwakilisha kwenye maonyesho ya Expo Japan, Mungu awaweke mahali pema huko mbele ya haki,

mara ya mwisho nilimuona Marehemu Mbaraka Mwinshehe, akipiga muziki wa dansi katika ukumbi wa muziki wa Planters, kwenye kona ya njia panda ya Uwanja wa Ndege wananchi wengi tulimiminika kumuona huyu shujaa, lakini alipiga nyimbo tatu tu na umeme ukazimika, ikawa ndio basi tumeliwa kiingilio mwezi uliofuatia Mbaraka alisafiri kwenda nchini Kenya, kurekodi santuri mpya na kutafuta vyombo vipya vya bendi yake, akiwa nchini Kenya alianzia Nairobi, baadaye akiwa safarini kwenda kupiga muziki mjini Mombasa, ndio mauti yakamkuta katika ajali mbaya sana ya gari, ambapo alipoteza damu nyingi sana, kuna uvumi ambao ulienea baadaye kuwa kukosekana kwake kuwa na hela za kutosha ndiko kulikosababisha kushindwa kutibiwa katika Hospitali kubwa ya Private kule Nchini Kenya, ambako inadaiwa angeweza kuponyeshwa iwapo angepewa msaada haraka kama angekuwa na hela zinazotakiwa, lakini siuamini sana huu uvumi,

Lakini anyway, huyu alikuwa mmoja wa mashujaa wetu, ambaye aliweza kulitumia gitaa lake kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia, bada ya kufariki kwake mdogo wake Ibrahim Mwinshehe na mpiga rythm wake, Charles Kasembe, walijaribu kuendeleza libeneke, lakini hawakufika mbali ilikuwa ni vigumu kuvaa viatu vya marehemu ambaye pekee tu ndiye aliyekuwa nyota wa ile bendi,

Mpigaji wake mwingine kwa jina la Lazaro Bonzo, yeye alihamia Nairobi na kuunda bendi ya Orch. Lombe Lombe, lakini nayo pia haikudumu sana, Moro Jazz nao pia hawakufika mbali, na to this day Morogoro hakuna tena bendi ya kutisha kama enzi hizo, ule wimbo wa Mbaraka wa kuisifia timu yetu ya taifa ya mpira wa miguu, mpaka leo unapigwa sana kwenye radio Germany, akiwasifia kina Elias Michael, Mweri, Mohamed Chuma, Zimbwe, Chitete, Shiwa, Maulidi "Mexico" Dilunga, Kitwana Manara, Adama Sabu, Gibbons Sembuli, Abdulrahamani Juma, Mohamed Salim, Omar Mahadhi, Zakaria Kinanda, Mohamed Ngulungu na kocha wao alikuwa akiitwa Paul West Gwivaha, damn! hizo zilikuwa ni enzi ndugu zangu yaani za Gossage Cup.

Ahsante Mkuu Kichuguu, kwa hizo picha za huyu shujaaa, Mungu amuweke mahali pema.
 

Pole Mkuu, naiombea hiyo computer yako ipone haraka kwa sababu wengine tunafuatilia kimyakimya haya mambo makubwa yanayofanyika kwenye thread hii
 
Compa! Hujatulia, mkuu! Thanx. teh teh teh!

Mkuu sitanii mkuu. Tuache kasumba. Historia ya sayansi wa Mtanzania/Mwafrika haijaandikwa ipasavyo. Tulikuwa na mainjinia wa maji waliokuwa wanaweza kuleta mvua kama ile aliyotaka kutuleta Lohasa kutoka Uthai. Huyu Injinia Kinjeketile japo sina picha yake alikuwa na mtambo kabisa na aliufanyia majaribio ndio maana walishinda awamu ya kwanza ya vita vile vya Maji Maji. Inabidi tukautafiti utaalamu huu badala ya kunga'nga'nia walichotuambia wanahistoria wa Kikoloni pale waliposema kuwa hatujawahi kuwa na uwezo wa kuvumbua kitu chochote cha kiteknolojia.

Pia kulikuwa mainjinia wa kuchunguza silaha za maangamizi. Inasemekana mmojawapo alikufa kwa ajali kazini pale alipolipukiwa na kipande cha risasi/baruti huko Katika Ngome ya Mtwa Mkwawa pale Kalenga. Injinia huyo wa Nuklia alikuwa anatengenesha vitu vilivyo ndani ya risasi walizozikamata baada ya kulishinda jeshi la Mjerumani Zelewiski pale Lugalo. Yote hii ilikuwa katika kutafuta kanuni ya kutengeneza silaha. Angalau wao walikuwa wanathubutu. Heri yao waliokuwa wanajitengenezea vitu vyao wenyewe.
 

mkuu umenikumbusha mbali sana bwana maana dingi na maza wamezipamba hizi picha pale sebuleni na kamwe hawataki zitolewe kwi kwi kwi kwi kwi............
 
hizi nazo ni sehemu ya historia yetu
 

Attachments

  • african leaders.jpg
    38.2 KB · Views: 842
  • forest-whitaker.jpg
    25.4 KB · Views: 829
  • jk1.jpg
    6.1 KB · Views: 1,149
  • jk2.jpg
    5.7 KB · Views: 1,070
  • jk3.jpg
    6.1 KB · Views: 1,080
sikuwa najua kuwa nyerere na yeye alikuwa anavaa pete zaidi ya ile ya ndoa! kumbe nae alikuwa 'tozi' enzi zake
 

Rev.Kishoka,

..bado sijaweza kufahamu mahusiano ya Karume na hawa 14 boyz kabla ya Mapinduzi.

..nadhani Karume alipewa uraisi kutokana na heshima yake kama kiongozi wa ASP, chama ambacho kilikuwa kikipata kura nyingi ktk chaguzi kama 3 zilizofanyika Zanzibar.

..ukiondoa Okello aliyetimuliwa, nadhani 14 boyz wengine waliendelea kuwa ktk circles of power kwa muda mrefu tu. siyo lazima wawepo ktk baraza la mawaziri.

..dhana kwamba 14 boyz walidhulumiwa jasho lao haina msingi sana. jaribu kulinganisha na waasisi wa Tanu walivyokuwa treated baada ya Uhuru.

..zaidi ya Okello aliyetimuliwa, je kuna member yeyote wa 14 boys aliyeswekwa kizuizini, au kuuwawa na utawala wa Karume?

NB:

..halafu Abdulrahman Babu tunayejaribu kumkweza naye si alikuwa DSM siku ya Mapinduzi?

..Babu na kundi lake walikuwa wasomi-wasomi sioni wakilandana hata kidogo na hawa 14 boys.

..14 boyz wanalandana zaidi na wafuasi wa ASP wa wakati huo, yaani makabwela.
 
picha ya mwisho...you mean kabla ya mwalimu kukutana na mauti? hiyo ilipigwa akiwa hospitalini london!

picha ya mwhisho akiwa tanzania? hiyo ilipigwa akiwa aiport dar es salaam akiagana na ndugu pamoja na viongozi just before boarding the plane to UK.
 
Kishoka,
Baada ya mapinduzi ya Zanzibar na mwungano wa 1964 Abdulrahman Babu alihamia Dar-es-Salaam full time. Kulikuwepo rumours wakati huo kuwa aliogopa kurudi Z'bar kwa sababu alidhania Karume angemkolimba. Hata Salim Ahmed Salim alikuwa hatubutu kuweka mguu wake Zanzibar mpaka mwaka 1975. There's more about Zanzibar and Karume that we simply do not know.
 
Mkuu Invisible na Mods,

Tafadhali naomba mzifungue hizi picha hapo kwa Mkuu Ochu, maana kuna picha muhimu na safi sana,

Mkuu Ochu,

Kofia chini na heshima mbele kwa uzalendo wako, ubarikiwe tu! Ndio maana ninaiheshimu sana JF mawe mazito hutokea kila kona, tena bila habari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…