Mkuu Kibunango,
1. Heshima mbele bro, naona hapo mstari wa mbele kuna marais wa zamani kuanzia kushoto ni Ngwabi wa Congo Brazaville, Bokassa wa Central Afrika, Haile Selassie Wa Ethiopia, Kenyatta wa Kenya, Siaka Stevens wa Siera Leone, na Mobuttu wa Zaire,
2. Mstari wa Nyuma ni Kayibanda wa Rwanda, Obotte wa Uganda, Mwalimu Baba Wa Taifa letu Tanzania, Kaunda wa Zambia, hao wengine wawili siwakumbuki kabisaa, ninaomba msaada na ninaweza kuwa nimewakosea wengine pia!
3. Huko chini ni rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete, ahsante kwa kuziweka kwa chini ya wazee wa kazi.
Mkuu Kibunango, ahsante sana kwa ufundi na maarifa yako mazito sana, na Mkulu Ochu, ubarikiwe.