Tukumbushane kazi alizofanikisha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Tukumbushane kazi alizofanikisha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Mengi sana yanasemwa kuhusu mafanikio ya Mwendazake kama vile watangulizi wake hawakufanya lolote. Kimsingi JK amefanya kazi kubwa sana. Kimsingi amefanya hata kazi za awali kwa yale aliyoyakamilisha Mwendazake kama uwanja wa Terminal III, Daraja la Mfugale, Daraja la Kijazi, SGR na barabara za Dar es Salam Metropolitan Project.

Mambo "kiduchu" aliyofanya Jakaya;

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29. Ajira kila mwaka
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka
34. Aliwagomea CCM na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.

Hayo ni machache ya Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa hakufanya chochote zaidi ya wizi na ufisadi walikuwa wanaishi nchi gani?

Hivi huyo wanaemtukuza amefanya jambo gani kubwa linalofikia hata robo ya mkubwa aliyoyafanya Kikwete?

Kwakuhitimisha Kikwete alifanya makubwa na Mikopo aliyokopa kila mmoja ananufaika nayo na vitu vinaonekana.

👉Kubwa zaidi lingine aliwaunganisha watz kwa pamoja bila kujali vyama vyao tofautu na sasa ambapo mpinzan anaonekana kama adui.
Mimi nashauri ungeanza hivi halafu vingine ndiyo vikafuata baada ya hapo:
1. UDOM
2. Shule za Sekondari za Kata

Yaani JK katika mambo haya mawili, aliugusa kwa kiwango cha juu mno moyo wangu. Na hata kwa mengine pia, ila kwangu mimi haya ndiyo yaliyoongoza
 
Kuna vitu umeviandika lakini haviko katika context

1. Mkapa alipeleka maelfu ya wanafunzi China, Ukraine, Urusi etc Lakini siyo bure, Waliondoka kwa makubaliano ya Mkopo, na hilo kundi lililokwenda huko sasa hivi linalia, Ni kundi linaloongoza kwa kudawaiwa Mamilioni mengi na bodi ya Mikopo. Kuna watu walionufaika na hizo scholarship Wanadaiwa hadi milioni 80. Government works on papers na inatunza kumbukumbu kwelikweli!. Wanajuta wale vijana leo!

2. Kikwete hakuwa na haja tena ya kuendeleza mpango wa kupeleka maelfu ya Wanafunzi China kwa sababu alifanikisha uwepo wa vyuo vikuu vingine nchini kama vile UDOM na Nelson Mandela, Na pia kuongezeka kwa vyuo binafsi nchini kama vile vya Kanisa, na pia baada ya JK kubadili vyuo vya advanced dipoma na kuvifanya viwe vyuo vikuu, Hapo unahitaji kupekeka vijana maelfu kwa kwa maelfu nje kwa udhamini wa serikali ili iweje? —Hata hivyo scholarship za kawaida kutoka kwa nchi rafiki ziliendelea kama kawaida.

3. Unazungumzia kipindi cha Mkapa wanafunzi kupata mkopo 100%, Labda nikukumbushe tu wakati Mkapa anaondoka madarakani kulikuwa na vyuo vikuu nchini vya kutoa degree havifiki 10, na vyuo vikuu vya serikali vilikuwa viwili, Yaani UDSM na SUA, Muhimbili nadhani kilikuwa bado chuo chini ya UDSM. Sasa Mkapa angeshindwaje kutoa mkopo wa 100% kwa idadi ndogo ya wanachuo waliodahiliwa katika vyuo hivyo, Ukizingatia kuwa miaka michache nyuma wakati wa Mwinyi hao wanafunzi walikuwa wakisoma Bure!

3. Kuhusu deni la Taifa, Mkapa alisamehewa deni, kwa hiyo reasonably wakati anaondoka deni lilikuwa dogo around Trillion 10 (Dola bilion 9.3) kwa exchange rate ya mwaka 2005 ambayo ilikuwa ni around sh 1169+ kwa USD), Sasa hadi mwezi July mwaka 2015 deni la Taifa lilikuwa around Dola bilion 17. 6.(exchange rate ilikuwa around 1600+ mwezi huo, kabla ya sh kuserereka kwa kasi kushuka na kwenda hadi 2000+ per dollar wakati wa uchaguzi mkuu) kwa hiyo JK ndani ya Miaka 10 aliongeza deni la Taifa kwa Takriban dola Bilion 8.3 (Natumia Dola ambayo ni stable currency kulinganisha na Shilingi)

Magufuli kakuta deni ni around Dola bilion 17.6, kaondoka likiwa around dola bilion 26 takriban dola Trilion 61 (mwezi march), Sasa ndani ya miaka mitano Magufuli kaongeza deni kwa Takriban dola Bilion (26-17.6 =8.4), Yaani kaongeza deni kwa kiwango cha pesa kinacholingana na alichoongeza Jakaya kwa miaka 10!, Je Magufuli naye angetawala kwa miaka 10 ingekuwaje?

Halafu wewe hauko honest, Upande mmoja unasema JK kaongeza Trillion 26 TSH lakini kwa Magu hutamki MaTSH unataka tutumie dola, Ila nakubaliana na wewe kuwa hayo maTSH hayatatupa picha halisi ya deni kwa sababu yako subjected to Depreciation ya hela n. k, Yaani sh 1 ya mwaka 2005 haina thamani sawa na sh 1 ya mwaka 2015, kwa hiyo ukisema JK kaongeza Trillion 26, Upo sahihi kwa mahesabu yetu ya pesa za madafu lakini Internafionally kule tunapolipa kwa dola reality ni tofauti. Ila nadhani umeona tukirudi kwenye dola, Msgufuli kakopa sana kwente miaka yake mitano madarakani!

4. Kuhusu miundo mbinu, Uongo mbaya JK alipiga kazi kubwa sana, Na ni miundo mbinu hiyo iliyompa Ujiko hata waziri wake wa ujenzi Magufuli mpaka akakubalika sana kwa watu, nakumbuka kauli za Magufuli akiwa waziri wa ujenzi kuwa "Nchi nzima inatifuka vumbi", na nyingine in context "Sasa hivi nchi inatandikwa mkeka", Ukiangalia vivuko, madaraja makubwa na madogo, Mwendokasi Dar, Barabara za kuunganisha mikoa, na hata zile alizoacha upembuzi yakinifu ukiwa umeshaisha na akiwa ameshazitafutia hela za ujenzi, barabara ambazo zilikuja kukamilishwa katika utawala wa Magufuli, Utaona kazi kubwa ambayo Jakaya aliifanya.
Ni kweli naweza kua out context bt kwa muktadha upi?nway ngoja nikujibu point zako km ifuatavyo.
1.1 Ni kweli Mkapa alipeleka Maelfu ya wanafunzi nje na hii ni kutokana na ukweli kua inchi iendelee lazima kuwe exposure na transfer of technology kutoka mataifa yaliyoendelea, na hapa ndipo China,Japan, korea kusini zilipotoboa kwa kupeleka vijana wao wengi USA na Ulaya huko waka aquire na kuiba technologies zilizowapaisha kiuchumi...huu mpango haukupaswa kufutwa ulipaswa uendelezwe kwa supawapatia subsidized rate hawa wanafunzi, bt akaifuta then full scholarship wakawa wanawapa watoto wao.
1.2 Issue ya kudaiwa ni kweli wanadaiwa ila unategemea nn umesomeshwa kwa gharama then unatafta ajira serikalini?mi nna wana wa3 walisoma russia & China, mmoja yupo USA, mwingine Geita na mwingine Songas and they are doing great ht hio mikopo hawaiskiii km inawaumiza maana package zao zimenona..

2. Point ya kuifuta hii program kwa kigezo cha Udom na Nelson Mandela nayo sio sahihi. Program ilifutwa 2006 while intake ya kwanza ya udom ikiwa Late ni 2007 na Nelson Mandela ikiwa 2011(5yrs later) na hapa ukumbuke Nelson Mandela ina chukua postgraduate tu sio undergraduate waliokua walengwa wa program ya mkapa. So hii point sio ya kimantiki.

3. Ktk hili ni kweli JPM amekopa zaidi in a short period bt angalia magnitude ya miradi yake compre na hio list iliyowekwa hapo juu inayo include kiwanda cha dangote km mradi uliojengwa wa JK.

4. Umaarufu kwa JPM haukuanza enzi za JK ulianza enzi za Mkapa hadi wenzake kutaka kumrestisha, Mkapa akaamua kumpa ulinzi maalumu. JK alivyoingia akamtoa Miundo Mbinu akampeleka ardhi akijua huko hatang'aa. MiundoMbinu akamuweka Chenge Mzee wa vijisenti akavurunda, then akampa Ndugu yake Shukuru Kawambwa akavurunda sana ikiwemo gharama za ujenzi kwa kilomita kupanda mpaka 1.3B na usimamizi Mbaya rejea ubora wa Kawawa(Mivinjeni to Mbagala) road akaona isiwe tabu ngoja tumrudishie mwenye wizara yake...kifupi JPM ndie alieing'arisha hio wizara sio mzee wa msoga aliekua anashinda hewani hajui nn kina endelea on the ground..Raisi anashindana millage na marubani..Raisi alietawala miaka 10 bt 2 yrs out of those akiwa safarini inchi za Ng'ambo.
 
Hapo kwenye kuunganisha unachemka enzi za unanijua mie ni Nani jamani kweli.
Mtu ukiwa na hela unavamia eneo la mtu inachukua kimabavu.
Kuna eneo moja kigamboni liliporwa kimabavu jamani yaani wewe nakuambia acha. Nilitamani kuhama nchi.
Unakumbuka Brazil walikuja kucheza na Taifa stars kwa gharama yetu ya 3 billions na huku Kuna shule watt wanakalia tofali za tope,madarasa ya udongo muda wowote yaweza kuwangukia na kuua watt wetu jamani.
Hospital ndo usiseme mama zetu na dada zetu wanakufa kwa kukosa huduma Mana hospital ama dispensary ziko mbali Sana.
Nafuu enzi za "we unanijuwa mimi ni nani?" KULIKO enzi za Rais wa awamu ya 5 kumiliki kikundi cha "WASIOJULIKANA" ambacho kilikuwa kina KIDNAP na ku- MURDER watu wanaokosoa tu uendeshaji wa nchi
 
Hio sio legassy
Hili jukwaa ndugu yangu MURUSI siyo size yako. Wewe soma upite tu kwa wanaojua Mambo wakujuze.

Hakuna neno legassy kwa Kiswahili wala English. Kwenye English kuna legacy
 
Nafuu enzi za "we inanijuwa mimi ni nani?" KULIKO enzi za Rais wa awamu ya 5 kumiliki kikundi cha "WASIOJULIKANA" ambacho kilikuwa kina KIDNAP na ku- MURDER watu wanaokosoa tu uendeshaji wa nchi
Kukosoa hao walitakiwa waaachwe Ila wale majambazi sio kabisa. Pia na kuchukua hela za wafanyabiashara Napo sio kabisa
 
Mengi sana yanasemwa kuhusu mafanikio ya Mwendazake kama vile watangulizi wake hawakufanya lolote. Kimsingi JK amefanya kazi kubwa sana. Kimsingi amefanya hata kazi za awali kwa yale aliyoyakamilisha Mwendazake kama uwanja wa Terminal III, Daraja la Mfugale, Daraja la Kijazi, SGR na barabara za Dar es Salam Metropolitan Project.

Mambo "kiduchu" aliyofanya Jakaya;

1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. JNIA terminal III
8. DART(Mwendo kasi)
9. Sekondari za Kata nchi nzima kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha
17. Dangote industry
18. Bomba la gesi Mtwara Dar
19. Kinyerezi I&II
20. Hospitali ya Moyo
21. MOI
22. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami(zaidi km 14000 zilijengwa nchi nzima)
23. Umeme kwa makao makuu ya wilaya
25. Ujenzi wa Mkongo wa taifa wa mawasiliano(leo tunajimwambafai na internet matunda ya JK)
26. JNICC Conference center(Ukumbi wa kisasa)
27. Hata CCM wenyewe aliwajengea ukumbi wa kisasa Dodoma.
28. Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi julai
29. Ajira kila mwaka
30. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
32. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu katika ukanda wa maziwa makuu.
33. Demokrasia iliyopevuka
34. Aliwagomea CCM na kuwaambia hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, sio kwa kipigo cha polisi.

Hayo ni machache ya Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete lakini hakujimwambafai.

Hawa wanaomtukana na kusema kuwa hakufanya chochote zaidi ya wizi na ufisadi walikuwa wanaishi nchi gani?

Hivi huyo wanaemtukuza amefanya jambo gani kubwa linalofikia hata robo ya mkubwa aliyoyafanya Kikwete?

Kwakuhitimisha Kikwete alifanya makubwa na Mikopo aliyokopa kila mmoja ananufaika nayo na vitu vinaonekana.

[emoji117]Kubwa zaidi lingine aliwaunganisha watz kwa pamoja bila kujali vyama vyao tofautu na sasa ambapo mpinzan anaonekana kama adui.
Kunakitu mnakitafta nyie hiyo yote nikutaka kufta legacy ya mwenda zake ukwel ni kwamba haitoftika milele maana hayo mnayoonesha ni ya miaka 10 pamoja na hivo mengine ni yauongo;
 
Kwa mtaji huu legacy ya mwendazake zinabakia huku:

1. Chatto International Airport
2. Burigi National park
3. Daraja la Busisi
4. Upanuzi wa barabara kijitonyama
5. Upanuzi wa barabara njia nane Dar - Kibaha
6. Kudorora kwa mahusiano ya kimataifa
7. Kukosekana kwa ajira mpya
8. Kutokupandishwa mishahara kwa wafanyakazi.
9. Ikulu kuwapo Chatto
10. Mdororo wa demokrasia nchini
11. Kushamiri kwa wasiojulikana
12. Kushamiri kwa kesi bambikizi
13. Na mengine ya namna ya #10 - #12

Kwa kweli nchi hii ilikuwa imechezewa sana!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
1. Unesema mradi ulisitishwa mwaka 2006 na UDOM ikaanza 2007, kwa hiyo ni gepu ya mwaka mmoja tu, Hii ni reasonable kabisa kwa sababu ni dhahiri serikali ilishaamua kuwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha ujayo yaani 2007 vijana wale waanze kusomea humuhumu nchini, kwa hiyo ni sahihi kusitisha mwaka mmoja kabla—Nadhani unaelewa bajeti huanza kuandaliwa mwaka mmoja kabla

2. Ingekuwa ni ajabu uendelee kutumia gharama za kumsomesha mwanafunzi mmoja nje wakati sasa vyuo vya kumsomeshea ndani kwa gharama nafuu sasa vipo, Kumbuka vyuo binafsi viliendelea kuongezeka kuanzia 2005

3. Ishu ya Exposure ni nzuri ndiyo maana scholarship hazikuzuiwa, Wizara ya elimu iliendelea kupokea scholarships kwa nchi rafiki ikiwemo china, urusi, Misri, Uturuki, India etc LAKINI serikali yenyewe ichukue maelfu ya wanafunzi ikawalipie gharama mara hadi mara 10 ya gharama za mwanafunzi anayesomea hapahapa nchini hiyo siyo sustainable, busara ilikuwa ni kuboresha capacity humuhumu nchini na ndicho kilichofanyika. Hata kama Kikwete angeendelea na project hiyo kwa miaka kadhaa, ingefikia myda ingekoma tu, maana serikali hatimaye ingejenfa vyuo vyake

3. Hoja kuwa Kikwete alimtoa Magufuli wizara ya Ujenzi ili asing'ae hiyo ni hoja muflisi, maana Hakuna waziri mwenye hati miliki na wizara fulani, Na wizara zote ni muhimu, haijalishi ni ya mifugo au uvuvi vyote hivyo ni muhimu kwa nchi. Kama Kikwete angeamua kumpiga chini Magufuli angeweza bila kujali ana umarufu kiasi gani kwa raia, Sema tu Kikwete alikuwa anathamini uwezo wa wengine ndiyo maana akaona JPM atamsaidia kwenye serikali yake, Lakini usijidanganye eti JPM nje ya serikali basi watu wangempindua Kikwete au wangeandamana amrudishe!, Hilo sahau, Hakuna mtu nchi hii anaweza kumletea rais Jeuri halafu rais huyo akakunjua makucha kisha huyo mtu eti akasababisha chochote!

5. Kuhusu ishu ya deni ya waliopelekwa nje na Mkapa kusoma, This thing is really, Wewe unayetoa statistic za watu 3 kuwa wako njema, unasahau maelfu ya wengine waliorudi nchini na kazi zao ni hizihizi waliosoma vyuo vya kawaida wanazofanya. Kwa hiyo the burden is real, na wanahenyeka!. Si kila mtu aliyesoma huko China na Ukraine na Urusi basi amepata chance ya kwenda Marekani au ufanya kazi kwenye makampuni makubwa au kujiajiri, Wengine ni malecturer humuhumu nchini na Deni linawakwangua kichizi
 
Stand kubwa na za kisasa karibu nchi zima masoko makubwa nayakisasa maeneo mengi ya nchi kukamirisha mwendo kasi Barabara nyingi za rami umeme vijijini kwavitendo Kuondoa biashara haramu za madawa yakulevya na viungo vya binadamu albino Kufufua shirika la ndenge atcl madaraja Kama ifakara busisi ambayo haijaisha n.k uadilifu na uwajibikaji makazini elimu bila Ada shule ya msingi na sekondari mikopo na pesa za matumizi chuoni bila blabla na porojo kuhamisha makao makuu dar to dodoma bwawa la nyerere kutokomeza ujangiri wa wanyamapori tembo vifaru kuongezeka kupunguza matumizi mabaya ya fedha(safar za nje n.k) na mengine mengi in 5years
 
CDM kwenye ubora wao.....madawa yakulevya, migomo ya Mara kwa Mara ya madactari na wanafunzi wa vyuo,kutekwa kiongozi wa madactari na waandishi wa habari (kibonde kubenea mwangoswi tegambwage.…), mapadri kuuawa kwa risasi na kumwagiwa tindikali, mahusiano mabaya na nchi jirani(Rwanda, Kenya malawi) makundi ndani ya chama chake, ufisadi na kashfa kibao, ajari za mabasi Kila Mara za kizembe zilizochukua uhai wa watanzani kutokana na viongozi kutokuwajibika....watu kusingiziwa uongo( Mara rowassa mwizi mara sio mwizi) kutokana na kushamiri media kanjanja.......nk
 
Yaani madereva wasababishe ajali lawama ziende kwa rais?

Migomo ya madaktari na wanafunzi hiyo ni sababu ya demokrasia kubwa, ungegoma kipindi cha magufuli unafukuzwa kazi au chuo

Mahusiano mabaya ya Rwanda na Malawi siyo kosa la Kikwete ni kosa la viongozi wao na tuliwanyoosha, Rwanda walikasitrika sisi kuwazuia wizi wao na uonevu wao Kongo, Malawi walileta chokichoko kuhusu Ziwa tukawapiga biti, Kenya uhusiano wetu overall ulikuwa mzuri, zile tit for tat zilikuwa ni tactical kwa ajili ya kulinda maslahi yetu

Mapadri kuuawa kwa risasi ni matendo ya kihalifu, vyombo vya dola havikuhusuka, na uchunguzi ulifanywa kutoka nje.

Habari za kashfa za kifisadi kutoka ndo uburu wa habari wenyewe, angetaka angefungia vyombo vyote vyenye kuripoti ufisadi usingezisikia

Haya uliyoripoti ni minor issues sana kulinganisha na Uharamia alioufanya Magufuli nchini
 
CDM kwenye ubora wao.....madawa yakulevya, migomo ya Mara kwa Mara ya madactari na wanafunzi wa vyuo,kutekwa kiongozi wa madactari na waandishi wa habari (kibonde kubenea mwangoswi tegambwage.…), mapadri kuuawa kwa risasi na kumwagiwa tindikali, mahusiano mabaya na nchi jirani(Rwanda, Kenya malawi) makundi ndani ya chama chake, ufisadi na kashfa kibao, ajari za mabasi Kila Mara za kizembe zilizochukua uhai wa watanzani kutokana na viongozi kutokuwajibika....watu kusingiziwa uongo( Mara rowassa mwizi mara sio mwizi) kutokana na kushamiri media kanjanja.......nk
Hizi kasoro ulizo mbebesha JK ni peanut sana. Mengi ni maisha ya kawaida ya Watanzania wala siyo udhaifu wa JK. Migomo ni njia ya kidemokrasia ya kudai haki kutoka kwenye mfumo au Utawala.

Mwendazake alitishia kupeleka Polisi wenye mabomu dhidi ya waandamanaji wa vyama vya upinzani.

ALL in all Watanzania tulikuwa na furaha
 
Stand kubwa na za kisasa karibu nchi zima masoko makubwa nayakisasa maeneo mengi ya nchi kukamirisha mwendo kasi Barabara nyingi za rami umeme vijijini kwavitendo Kuondoa biashara haramu za madawa yakulevya na viungo vya binadamu albino Kufufua shirika la ndenge atcl madaraja Kama ifakara busisi ambayo haijaisha n.k uadilifu na uwajibikaji makazini elimu bila Ada shule ya msingi na sekondari mikopo na pesa za matumizi chuoni bila blabla na porojo kuhamisha makao makuu dar to dodoma bwawa la nyerere kutokomeza ujangiri wa wanyamapori tembo vifaru kuongezeka kupunguza matumizi mabaya ya fedha(safar za nje n.k) na mengine mengi in 5years
Yaani tuko very low kwenye reasoning. Kweli tunajuvunia Stendi za mabasi Kama maendeleo?

Unapata nini kwenye standi ya mabasi? Hata usingekuwa na standi bado mabasi yangekuja na kubeba abiria tu.

Mwendokasi ilibuniwa na kukamilika kipindi cha JK.

ADA ya shule ni propaganda tu. Ni JK Nyerere na kidogo Mwinyi ndiyo walikuwa wanasomesha bila ada kwa kuwa kulikuwa wanafunzi wachache. Tusidanganyane kabisa hapa bado wazazi wanagharamia nauli, uniforms, kalamu na madaftari.

Hiyo Tsh 20,000 ni mchango ndiyo umeondolewa ambao siamini kama kuna mzazi amewahi kushindwa kumpeleka mwanae shule kwa kukosa Tsh 20,000.
 
Ujuaji mwingii waTz..yeye kajb ww unamcriticize!!ASSS HOLE WW
 
Ujuaji mwingii waTz..yeye kajb ww unamcriticize!!ASSS HOLE WW
Hakuna tusi jipya duniani ni marudio tu. Halafu unapomtukana mtu mwenye parody ID ni sawa na kujitukana mwenyewe.
Mimi nimekuja na hoja kuonyesha kuwa uwekezaji wa standi za mabasi ni vitu vidogo sana. Ulipaswa uni criticise kwa kuonyesha kuwa ni vitu vya maana kwa hoja.
 
kwa hyo waziri alikuwa anamlazimisha mh. rais..!😟🥺
Magu alikuwa aki'force' mambo mengi, hata JK mwenyewe alisema mawaziri wake wote hawakthubutu kumtania au kum'force' isipokuwa ngosha pekee! Hakuangalia sura, mziki wake JPM akiwa waziri chini ya JK mkwele anautambua muulizeni Liz1 atawaeleza!
 
Back
Top Bottom