Tukumbushane kazi alizofanikisha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Mimi nashauri ungeanza hivi halafu vingine ndiyo vikafuata baada ya hapo:
1. UDOM
2. Shule za Sekondari za Kata

Yaani JK katika mambo haya mawili, aliugusa kwa kiwango cha juu mno moyo wangu. Na hata kwa mengine pia, ila kwangu mimi haya ndiyo yaliyoongoza
 
Ni kweli naweza kua out context bt kwa muktadha upi?nway ngoja nikujibu point zako km ifuatavyo.
1.1 Ni kweli Mkapa alipeleka Maelfu ya wanafunzi nje na hii ni kutokana na ukweli kua inchi iendelee lazima kuwe exposure na transfer of technology kutoka mataifa yaliyoendelea, na hapa ndipo China,Japan, korea kusini zilipotoboa kwa kupeleka vijana wao wengi USA na Ulaya huko waka aquire na kuiba technologies zilizowapaisha kiuchumi...huu mpango haukupaswa kufutwa ulipaswa uendelezwe kwa supawapatia subsidized rate hawa wanafunzi, bt akaifuta then full scholarship wakawa wanawapa watoto wao.
1.2 Issue ya kudaiwa ni kweli wanadaiwa ila unategemea nn umesomeshwa kwa gharama then unatafta ajira serikalini?mi nna wana wa3 walisoma russia & China, mmoja yupo USA, mwingine Geita na mwingine Songas and they are doing great ht hio mikopo hawaiskiii km inawaumiza maana package zao zimenona..

2. Point ya kuifuta hii program kwa kigezo cha Udom na Nelson Mandela nayo sio sahihi. Program ilifutwa 2006 while intake ya kwanza ya udom ikiwa Late ni 2007 na Nelson Mandela ikiwa 2011(5yrs later) na hapa ukumbuke Nelson Mandela ina chukua postgraduate tu sio undergraduate waliokua walengwa wa program ya mkapa. So hii point sio ya kimantiki.

3. Ktk hili ni kweli JPM amekopa zaidi in a short period bt angalia magnitude ya miradi yake compre na hio list iliyowekwa hapo juu inayo include kiwanda cha dangote km mradi uliojengwa wa JK.

4. Umaarufu kwa JPM haukuanza enzi za JK ulianza enzi za Mkapa hadi wenzake kutaka kumrestisha, Mkapa akaamua kumpa ulinzi maalumu. JK alivyoingia akamtoa Miundo Mbinu akampeleka ardhi akijua huko hatang'aa. MiundoMbinu akamuweka Chenge Mzee wa vijisenti akavurunda, then akampa Ndugu yake Shukuru Kawambwa akavurunda sana ikiwemo gharama za ujenzi kwa kilomita kupanda mpaka 1.3B na usimamizi Mbaya rejea ubora wa Kawawa(Mivinjeni to Mbagala) road akaona isiwe tabu ngoja tumrudishie mwenye wizara yake...kifupi JPM ndie alieing'arisha hio wizara sio mzee wa msoga aliekua anashinda hewani hajui nn kina endelea on the ground..Raisi anashindana millage na marubani..Raisi alietawala miaka 10 bt 2 yrs out of those akiwa safarini inchi za Ng'ambo.
 
Nafuu enzi za "we unanijuwa mimi ni nani?" KULIKO enzi za Rais wa awamu ya 5 kumiliki kikundi cha "WASIOJULIKANA" ambacho kilikuwa kina KIDNAP na ku- MURDER watu wanaokosoa tu uendeshaji wa nchi
 
Hio sio legassy
Hili jukwaa ndugu yangu MURUSI siyo size yako. Wewe soma upite tu kwa wanaojua Mambo wakujuze.

Hakuna neno legassy kwa Kiswahili wala English. Kwenye English kuna legacy
 
Nafuu enzi za "we inanijuwa mimi ni nani?" KULIKO enzi za Rais wa awamu ya 5 kumiliki kikundi cha "WASIOJULIKANA" ambacho kilikuwa kina KIDNAP na ku- MURDER watu wanaokosoa tu uendeshaji wa nchi
Kukosoa hao walitakiwa waaachwe Ila wale majambazi sio kabisa. Pia na kuchukua hela za wafanyabiashara Napo sio kabisa
 
Kunakitu mnakitafta nyie hiyo yote nikutaka kufta legacy ya mwenda zake ukwel ni kwamba haitoftika milele maana hayo mnayoonesha ni ya miaka 10 pamoja na hivo mengine ni yauongo;
 
Kwa mtaji huu legacy ya mwendazake zinabakia huku:

1. Chatto International Airport
2. Burigi National park
3. Daraja la Busisi
4. Upanuzi wa barabara kijitonyama
5. Upanuzi wa barabara njia nane Dar - Kibaha
6. Kudorora kwa mahusiano ya kimataifa
7. Kukosekana kwa ajira mpya
8. Kutokupandishwa mishahara kwa wafanyakazi.
9. Ikulu kuwapo Chatto
10. Mdororo wa demokrasia nchini
11. Kushamiri kwa wasiojulikana
12. Kushamiri kwa kesi bambikizi
13. Na mengine ya namna ya #10 - #12

Kwa kweli nchi hii ilikuwa imechezewa sana!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
1. Unesema mradi ulisitishwa mwaka 2006 na UDOM ikaanza 2007, kwa hiyo ni gepu ya mwaka mmoja tu, Hii ni reasonable kabisa kwa sababu ni dhahiri serikali ilishaamua kuwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha ujayo yaani 2007 vijana wale waanze kusomea humuhumu nchini, kwa hiyo ni sahihi kusitisha mwaka mmoja kabla—Nadhani unaelewa bajeti huanza kuandaliwa mwaka mmoja kabla

2. Ingekuwa ni ajabu uendelee kutumia gharama za kumsomesha mwanafunzi mmoja nje wakati sasa vyuo vya kumsomeshea ndani kwa gharama nafuu sasa vipo, Kumbuka vyuo binafsi viliendelea kuongezeka kuanzia 2005

3. Ishu ya Exposure ni nzuri ndiyo maana scholarship hazikuzuiwa, Wizara ya elimu iliendelea kupokea scholarships kwa nchi rafiki ikiwemo china, urusi, Misri, Uturuki, India etc LAKINI serikali yenyewe ichukue maelfu ya wanafunzi ikawalipie gharama mara hadi mara 10 ya gharama za mwanafunzi anayesomea hapahapa nchini hiyo siyo sustainable, busara ilikuwa ni kuboresha capacity humuhumu nchini na ndicho kilichofanyika. Hata kama Kikwete angeendelea na project hiyo kwa miaka kadhaa, ingefikia myda ingekoma tu, maana serikali hatimaye ingejenfa vyuo vyake

3. Hoja kuwa Kikwete alimtoa Magufuli wizara ya Ujenzi ili asing'ae hiyo ni hoja muflisi, maana Hakuna waziri mwenye hati miliki na wizara fulani, Na wizara zote ni muhimu, haijalishi ni ya mifugo au uvuvi vyote hivyo ni muhimu kwa nchi. Kama Kikwete angeamua kumpiga chini Magufuli angeweza bila kujali ana umarufu kiasi gani kwa raia, Sema tu Kikwete alikuwa anathamini uwezo wa wengine ndiyo maana akaona JPM atamsaidia kwenye serikali yake, Lakini usijidanganye eti JPM nje ya serikali basi watu wangempindua Kikwete au wangeandamana amrudishe!, Hilo sahau, Hakuna mtu nchi hii anaweza kumletea rais Jeuri halafu rais huyo akakunjua makucha kisha huyo mtu eti akasababisha chochote!

5. Kuhusu ishu ya deni ya waliopelekwa nje na Mkapa kusoma, This thing is really, Wewe unayetoa statistic za watu 3 kuwa wako njema, unasahau maelfu ya wengine waliorudi nchini na kazi zao ni hizihizi waliosoma vyuo vya kawaida wanazofanya. Kwa hiyo the burden is real, na wanahenyeka!. Si kila mtu aliyesoma huko China na Ukraine na Urusi basi amepata chance ya kwenda Marekani au ufanya kazi kwenye makampuni makubwa au kujiajiri, Wengine ni malecturer humuhumu nchini na Deni linawakwangua kichizi
 
Stand kubwa na za kisasa karibu nchi zima masoko makubwa nayakisasa maeneo mengi ya nchi kukamirisha mwendo kasi Barabara nyingi za rami umeme vijijini kwavitendo Kuondoa biashara haramu za madawa yakulevya na viungo vya binadamu albino Kufufua shirika la ndenge atcl madaraja Kama ifakara busisi ambayo haijaisha n.k uadilifu na uwajibikaji makazini elimu bila Ada shule ya msingi na sekondari mikopo na pesa za matumizi chuoni bila blabla na porojo kuhamisha makao makuu dar to dodoma bwawa la nyerere kutokomeza ujangiri wa wanyamapori tembo vifaru kuongezeka kupunguza matumizi mabaya ya fedha(safar za nje n.k) na mengine mengi in 5years
 
CDM kwenye ubora wao.....madawa yakulevya, migomo ya Mara kwa Mara ya madactari na wanafunzi wa vyuo,kutekwa kiongozi wa madactari na waandishi wa habari (kibonde kubenea mwangoswi tegambwage.…), mapadri kuuawa kwa risasi na kumwagiwa tindikali, mahusiano mabaya na nchi jirani(Rwanda, Kenya malawi) makundi ndani ya chama chake, ufisadi na kashfa kibao, ajari za mabasi Kila Mara za kizembe zilizochukua uhai wa watanzani kutokana na viongozi kutokuwajibika....watu kusingiziwa uongo( Mara rowassa mwizi mara sio mwizi) kutokana na kushamiri media kanjanja.......nk
 
Yaani madereva wasababishe ajali lawama ziende kwa rais?

Migomo ya madaktari na wanafunzi hiyo ni sababu ya demokrasia kubwa, ungegoma kipindi cha magufuli unafukuzwa kazi au chuo

Mahusiano mabaya ya Rwanda na Malawi siyo kosa la Kikwete ni kosa la viongozi wao na tuliwanyoosha, Rwanda walikasitrika sisi kuwazuia wizi wao na uonevu wao Kongo, Malawi walileta chokichoko kuhusu Ziwa tukawapiga biti, Kenya uhusiano wetu overall ulikuwa mzuri, zile tit for tat zilikuwa ni tactical kwa ajili ya kulinda maslahi yetu

Mapadri kuuawa kwa risasi ni matendo ya kihalifu, vyombo vya dola havikuhusuka, na uchunguzi ulifanywa kutoka nje.

Habari za kashfa za kifisadi kutoka ndo uburu wa habari wenyewe, angetaka angefungia vyombo vyote vyenye kuripoti ufisadi usingezisikia

Haya uliyoripoti ni minor issues sana kulinganisha na Uharamia alioufanya Magufuli nchini
 
Hizi kasoro ulizo mbebesha JK ni peanut sana. Mengi ni maisha ya kawaida ya Watanzania wala siyo udhaifu wa JK. Migomo ni njia ya kidemokrasia ya kudai haki kutoka kwenye mfumo au Utawala.

Mwendazake alitishia kupeleka Polisi wenye mabomu dhidi ya waandamanaji wa vyama vya upinzani.

ALL in all Watanzania tulikuwa na furaha
 
Yaani tuko very low kwenye reasoning. Kweli tunajuvunia Stendi za mabasi Kama maendeleo?

Unapata nini kwenye standi ya mabasi? Hata usingekuwa na standi bado mabasi yangekuja na kubeba abiria tu.

Mwendokasi ilibuniwa na kukamilika kipindi cha JK.

ADA ya shule ni propaganda tu. Ni JK Nyerere na kidogo Mwinyi ndiyo walikuwa wanasomesha bila ada kwa kuwa kulikuwa wanafunzi wachache. Tusidanganyane kabisa hapa bado wazazi wanagharamia nauli, uniforms, kalamu na madaftari.

Hiyo Tsh 20,000 ni mchango ndiyo umeondolewa ambao siamini kama kuna mzazi amewahi kushindwa kumpeleka mwanae shule kwa kukosa Tsh 20,000.
 
Ujuaji mwingii waTz..yeye kajb ww unamcriticize!!ASSS HOLE WW
 
Ujuaji mwingii waTz..yeye kajb ww unamcriticize!!ASSS HOLE WW
Hakuna tusi jipya duniani ni marudio tu. Halafu unapomtukana mtu mwenye parody ID ni sawa na kujitukana mwenyewe.
Mimi nimekuja na hoja kuonyesha kuwa uwekezaji wa standi za mabasi ni vitu vidogo sana. Ulipaswa uni criticise kwa kuonyesha kuwa ni vitu vya maana kwa hoja.
 
kwa hyo waziri alikuwa anamlazimisha mh. rais..!😟🥺
Magu alikuwa aki'force' mambo mengi, hata JK mwenyewe alisema mawaziri wake wote hawakthubutu kumtania au kum'force' isipokuwa ngosha pekee! Hakuangalia sura, mziki wake JPM akiwa waziri chini ya JK mkwele anautambua muulizeni Liz1 atawaeleza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…