"Tetemeko" kati ya 2013 au 2014 kumbe upepo tu mkali vigorofa vya mkoloni vikayumbaaa....siku hiyo ilikua kama vita na alama kwny kidole mbaka leo ninayo kukimbizana kwny ngazi mle kushuka chini kila mtu anaokoa maisha yake.
Kama ingekua lile jengo kuanguka kweli siku ile ingekua noma snaa mana imagine chumba cha watu wanne mnalala zaidi ya 20 na ni kawaida kubebana na wengine magodoro yanawekwa chini ya uvungu wa kitanda. Usiku yanavutwa sakafuni watu walale.
Kama kulala kwa shifti hivi alooo😁😁na macbook yangu hata sikukumbuka huyo nikasepa ila haikupotea mana lile purukushani halikua la kawaida kila mtu alikua anataka kuokoa roho yake.
Hall II kule juu kabisa gorofani kulikua na kama kastoo hivi, basi wadau wengine walikua wanaishi kama chumba tu. Kushindia mikate na chai semista nzima kawaida tu na mtu anatoka na ufaulu mzuri kabisa wazee wa COET