Tukumbushane maisha ya UDSM enzi hizo, wazee wa Bibo na Main Campus

Kuna mazingira ya kupata honors. Kumantain gpa inahusika zaidi. Au chuo kuwa achievement fulani ktk mwaka miaka uliyokuwa chuoni.
Mimi nina honors ya udsm kwa ninavyoelewa mimi ni gpa kupanda lets say mwaka wa kwanza ulipata 3.0 mwaka wa pili 3.5 mwaka wa tatu 3.8 mwaka wa nne 4
 
Wewe ulikuwa kama mimi tulikuwa wote shadow campus nakumbuka kwenye graduation kuna demu alinishangaa " kumbe na wewe tumesoma wote"
Ilikuwa full kitaa nilikuwa na hiace 3 nazisimamia naendesha toyota hilux 2.4 jumamosi nilikuwa natimba mabibo hostel kuchukua masela kwenda bilcanas.
Kwenye group presentation nilikuwa nachangia kuprint .
Nilisoma kikauzu sana
Nilikuwa ka si mwanafunzi na sikuwahi kusup.
Sikumbuki kama nilishawahi kukaa na wenzangu kufanya sijui group discussion
Sikuwahi kuwa na dem udsm. Nakumbuka watu walikuwa wamegoma chuo kimefungwa (ishu ilikuwa kupinga mswada wakuanzisha bodi ya mikopo) hata sijui naibuka chuo mojakwamoja hadi lecture theater 1 kwenye kipindi nashangaa hamna watu kuuliza watu nje naambiwa wewe vipi jana kulikuwa na bonge la kunji watu tumepigwa mabomu na chuo kimefungwa nikabaki naduwaa nawacheki masela wangu wa mabibo wananiambiwa saa 8 mchana wanatakiwa wasionekane hapo hostel wakaniomba niwahifadhi ikabidi niwafate niwahifadhi kwangu
 
Kwa maisha ya chuo wewe ulikuwa lugumi aka mutu ya pesa
 
Kuna mama mmoja pale Mabibo Hostel aliitwa Mama Mwarabu.Chapati zake zilikuwa kubwa na tamu.Nimekumbuka mbali sana
 
"Tetemeko" kati ya 2013 au 2014 kumbe upepo tu mkali vigorofa vya mkoloni vikayumbaaa....siku hiyo ilikua kama vita na alama kwny kidole mbaka leo ninayo kukimbizana kwny ngazi mle kushuka chini kila mtu anaokoa maisha yake.

Kama ingekua lile jengo kuanguka kweli siku ile ingekua noma snaa mana imagine chumba cha watu wanne mnalala zaidi ya 20 na ni kawaida kubebana na wengine magodoro yanawekwa chini ya uvungu wa kitanda. Usiku yanavutwa sakafuni watu walale.

Kama kulala kwa shifti hivi alooo😁😁na macbook yangu hata sikukumbuka huyo nikasepa ila haikupotea mana lile purukushani halikua la kawaida kila mtu alikua anataka kuokoa roho yake.

Hall II kule juu kabisa gorofani kulikua na kama kastoo hivi, basi wadau wengine walikua wanaishi kama chumba tu. Kushindia mikate na chai semista nzima kawaida tu na mtu anatoka na ufaulu mzuri kabisa wazee wa COET
 
Hall 2 lift ilishaponaga?
 
Haha noma sana mkuu life flani hivi yani
 
kusaja msenge sana
 
Block D 2006 tujuane.

Nilikuwa na kadem ka sociology kalikua kanakaa Block A.

Basi ulikuwa mwendo wa kuchedana tu.

Popote ulipo Rose B, mueleze ukweli mumeo Mimi memento ni nani
Acha hizo.Utavunja ndoa za watu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…