Tukumbushane maisha ya UDSM enzi hizo, wazee wa Bibo na Main Campus

Enzi hizo Makamu Mkuu wa Chuo ni Mathew Luhanga! Taaluma yuko Prof. Mayunga Nkunya, Fedha Prof. Yunus Mgaya!!

Hakika Udsm ilikua ni 🔥🔥🔥! Dk mbili tu, KUNJI!!! 😁😁😁 Revolution Square!!!
Hivi kweli Luhanga alikuwa mjivuni sana??
 
Maisha yalikuwa na stress Sana pale kitivoni( sheria) wahuni tulikuwa tuna jibalance kwa kununua kuponi za RB 600, nimekaa mabibo hostel miaka minne , bila kunji ninge disco, nawakumbuka Prof majamba alikuwa anatupeleka mno, videmu vya education tumepiga Sana uwanjani mabibo, corner bar,Riverside nk kuangalia epl hapo kighorofani, club le mambo sijui Bado ipo, unaenda club unarudi unakula tikiti nk kifupi udsm Ni sehemu nzuri
 
Hiki ndicho kipindi ambacho na mimi nilipita udsm! Boom 2500! Rais wa Daruso akiwa ni Mwita Mwikabwe (Mwita Waitara MB)!!

Kwa mara ya kwanza niliishi kwenye nyumba ya ghorofa na yenye madirisha ya aluminium pale Mabibo Hostel!!
Kuna mwita mwingine alikuwa na upara hivi alikuwa engineering kule alikuwa president wa Daruso achana na huyu mbunge jina limenitoka. Janki flani mtaratiibu.
 

Alikuwa anajua kiswahili ?
 
Duuuh, ilikuwa nona sana!!
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa pili kulikuwa na mgomo tulipigwa mabomo siji sahau nilijikuta nipo kwenye mtalu wa maji taka Ila Kuna miamba sokwe mtu na alishababu aka mabilika sijui wako wapi Hawa miamba na kadada flani ka Arusha jina nimekasahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…