Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Kuna waliopata wakihudumia wagonjwa na wengine katika ajali pia.
ukweli usemwe (kwa nia ya kujenga) kwa nchi zetu izi ao hawafiki hata 1%, trust me, 99%+ ni ngono zembe.

leo hii sio ajabu kukuta watu wamekutana tu mara ya kwanza wala hawajuani kivile historia zao wanaishia kulana kavukavu na wengine wanenda mbali zaidi kujisifia eti wamekula kimasihara sasa apo kuna kazi tena?.

tukiweza kuchukua hadhari kwa ngono zembe tutakuwa tumeepuka pakubwa sana maambukizi mapya.
 
Kwani ARV haziuzwi?
Makampuni yanatengenezwa hizo dawa hayatafungwa
makampuni kufungwa kunaweza kutokea kama tu hakuna uhitaji au uhitaji ushuke sana kiasi cha makampuni hayo kushindwa gharama za uzalishaji
sasa uhitaji utaendelea kuwepo tu maadam binadam anaendelea kuishi
 
Kama HIV ni mchongo ni sababu ipi iliyofanya watu wakonde sana na kufariki kipindi hicho ugonjwa unaingia mkoani kagera ilihali watu hawaujui ugonjwa wenyewe?
 
Sitosahau huo ugonjwa uliwaua wajomba zangu 5 na wake zao ,ukamuua kaka yangu na mkewe ...wote walikufa ndani ya miaka miwili 1992 na 1993 kutokana na kukosekana kwa elimu binamu yangu akamleta mganga wa kienyeji kwasababu aliwapoteza wazazi wake wote na ndugu yake tena wote mwaka mmoja,,, kwahiyo mganga alipofika alivyopiga Ramli zake ikaonekana ni mama yangu mzazi ndie kawaua kaka zake na wake zao kisa mashamba aisee ni kisa ambacho sitosahau mpaka nafariki kwasababu tulidhalilika mno kijijini
 
ARV muda si mrefu zitakuwa za dili - kufa kufaana huna chochote kitu jiandae ku rest.
 
Hakuna familia kwa miaka hiyo ambayo haikupoteza mpendwa wao kwa Ukimwi.
 
Sehemu kama makete nyumba zilibaki magofu, familia yote ilikwenda na umeme.
 
Huo ulikua ukimwi wa zamani, sasa hivi watu wanaumwa na hawajijui hata wanadunda tu mtaani
 
navoona kama hawa jamaa wataacha kutupatia pesa tutachangia matibabu, sasa apo ndo mtihani sana kwa familia hoehae, kuzingatia dawa kutashuka na maambukizi mapya yatapaa.
Unatakiwa ulipe 76k ndo upewe dawa za mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…