Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Ukoo wangu Walifariki 21...1986_1997 Nakuacha Familia yatima...namimi mwenyewe yatima...NDO CHANZO CHA MIMI KUSOMA UDAKTARI.
pole sana mkuu na hongera kwa maamuzi mazuri ya kuokoa jamii yako.
 
Nakumbuka kijijini kwetu mgonjwa wa kwanza alikuwa mwanajeshi
wahanga wengi wa mwanzo walikuwa ni watu kama hao wenye vipato na wanaosafirisafiri nje ya maeneo yao kwenda kwenye hii miji mikubwa iliyochangamka wanachukua ngoma kwa warembo wa uko wanarudisha ugonjwa nyumbani hlf ukizingatia wenyewe hawajijui. marehemu kepteni komba aliimba wimbo 'mgeni' kwaajili hii. kipindi icho watu wa kawaida walikuwa salama sana.
 
ARV zimefanya baadhi ya watu waone ukimwi ni kama mafua, zikianza kuwa adimu hakika watu wataumia
 
Bk. huko watu walikufa Kijiji kizima. Yaani Kila siku wanazikwa watu watatu, wanne kwenye Kijiji kimoja kama vile kuku na kideri.
Yeah, nadhani Kijiji kimoja kiko mpakani na Uganda,kulikuwa na mavazi fulani maarufu yakiuzwa toka uko kuingia tz,watu walihisi ndani yake kulikuwa na ugonjwa huo, maana hawakujua unapatikanaje,,baadae sana ndo ikajulikana !!!,too late watu washapukutika balaa,ilikuwa hatari!!.
 
Msisahau na nyimbo special kwa ajili ya ngwengwe za kipnd hiko…
nyimbo nyingi sana ziliimbwa kwa ajili ya ugonjwa huu. marehemu kepteni komba aliimba wimbo uliitwa 'mgeni' akifananisha hiv na mgeni aliyetembelea nyumba flani na kujikaribisha mwenyewe adi chumbani kwa baba na mama, prof jize na dad nundaz ya feruz bdae nao waliimbata sana
 
Nikiwa shule salamu ilikuwa "UKIMWI UNAUA TUJIHADHARI TUSIPATWE NA UKIMWI, SHIKAMOO MWALIMU"
ni kweli kabisa wakati huo elimu ililenga zaidi kuwaogopesha watu kuepuka kupata maambukizi. saivi mambo yamebadilika sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…