Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Ukoo wangu Walifariki 21...1986_1997 Nakuacha Familia yatima...namimi mwenyewe yatima...NDO CHANZO CHA MIMI KUSOMA UDAKTARI.
pole sana mkuu na hongera kwa maamuzi mazuri ya kuokoa jamii yako.
 
Nakumbuka kijijini kwetu mgonjwa wa kwanza alikuwa mwanajeshi
wahanga wengi wa mwanzo walikuwa ni watu kama hao wenye vipato na wanaosafirisafiri nje ya maeneo yao kwenda kwenye hii miji mikubwa iliyochangamka wanachukua ngoma kwa warembo wa uko wanarudisha ugonjwa nyumbani hlf ukizingatia wenyewe hawajijui. marehemu kepteni komba aliimba wimbo 'mgeni' kwaajili hii. kipindi icho watu wa kawaida walikuwa salama sana.
 
ARV zimefanya baadhi ya watu waone ukimwi ni kama mafua, zikianza kuwa adimu hakika watu wataumia
- Hizi ARV zimeanza kutolewa kwenye mwaka 2003 au 2004 hapa wenye kumbukumbu sahihi mtanirekebisha. kabla ya hapo hapakuwa na dawa za kufubaza.

- Ugonjwa huu uliogopesha sana kiasi ambacho jamii haikuwa tayari kuuzungumzia. kimya kikuu kilitanda bila shaka kila mmoja akiomba kwa mola wake amuepushe na kikombe.

- Elimu kwa jamii zilitolewa zikichagizwa na picha za kilichokuwa kinaendelea mkoa wa kagera. kwa mujibu wa taswira zìle huko kagera ugonjwa ulimaliza watu wengi na wengine hata nyumba zilifungwa hakuna aliyebaki. nyumba zingine nyingi zilibaki zikiendeshwa na watoto mayatima baada ya wazazi wote kufariki.

- Kimya kingi kilitanda huku ugonjwa ukiendelea kutafuna watu kimyakimya.

- Kwenye hatua za mwanzoni wagonjwa wengi walikuwa wakionekana kupata mkanda wa jeshi yani miaka hiyo kama wewe una mkanda wa jeshi tu basi ilikuwa ni uthibitisho tosha tayari una tatizo hilo.

- Ukiona jirani yako flani haonekani hapo mtaani hiyo ilikuwa ni ishara tosha kuwa kama jirani uyo hajasafiri basi tayari uenda mambo yameshaharibika.

- Ugonjwa ulikuwa haufichiki. Ukiwa nao utajulikana tu apo kitaani kwenu. maana mwanzoni utajifungia ndani kwako lakini bdae lazma utoe ukahemee au kupata matibabu nk. ukitoka tu habari zako zinaanza kusambaa kama moto wa nyika.

- Ili kuepuka macho na vidole vya walimwengu familia nyingi ziliwapeleka mahospitali wapendwa wao mapema alfajiri sana au hata usiku.

- Familia nyingi zilikuwa zinaepuka kuwapima wagonjwa wao maana unampimaje mtu wakati unajua ugonjwa wenyewe hauna dawa. hivyo basi familia nyingi ziliishia kuuguza tu wagonjwa wao kimyakimya hadi wagonjwa anapokutana na mwisho wake.

- Wagonjwa wengi waliisha sana miili yao. hata kama ulikuwa kibonge kama pipa mwili wote utaisha kabisa unabaki kichwa ngozi na mifupa mitupu tu. ilikuwa sio ajabu kukuta mtu mwenye mwili mkubwa kama wale mabaunsa kaisha mwili wote kiasi hata usiweze kumtambua.

- Ilikuwa kawaida tu mtu mzima kabisa mwenye mwili uliojengeka vema akamalizwa na kubaki makongoro tu kiasi ambacho akilala kitandani hlf wewe ukapita apo usimuone au kujua kama pale kitandani kuna mtu amelala. najua kuna wanaozani natania lakini iyo ndio hali ilivyokuwa wakati huo.

- Watoto wengi waliozaliwa na maambukizi hawakuweza kuishi wengi walifariki baada ya muda mfupi na wachache kwa kudra za mwenyezi waliweza kuishi na wengine wako hai hata leo hii.

Hapa tunakumbushana tu hatutishani ukimwi upo tujilinde.

***Tafadhali msiuunge uzi huu tuna vijana damu changa wengi humu wanapaswa kupata ufahamu wa kule tulikotoka.
 
Bk. huko watu walikufa Kijiji kizima. Yaani Kila siku wanazikwa watu watatu, wanne kwenye Kijiji kimoja kama vile kuku na kideri.
Yeah, nadhani Kijiji kimoja kiko mpakani na Uganda,kulikuwa na mavazi fulani maarufu yakiuzwa toka uko kuingia tz,watu walihisi ndani yake kulikuwa na ugonjwa huo, maana hawakujua unapatikanaje,,baadae sana ndo ikajulikana !!!,too late watu washapukutika balaa,ilikuwa hatari!!.
 
Msisahau na nyimbo special kwa ajili ya ngwengwe za kipnd hiko…
nyimbo nyingi sana ziliimbwa kwa ajili ya ugonjwa huu. marehemu kepteni komba aliimba wimbo uliitwa 'mgeni' akifananisha hiv na mgeni aliyetembelea nyumba flani na kujikaribisha mwenyewe adi chumbani kwa baba na mama, prof jize na dad nundaz ya feruz bdae nao waliimbata sana
 
Nikiwa shule salamu ilikuwa "UKIMWI UNAUA TUJIHADHARI TUSIPATWE NA UKIMWI, SHIKAMOO MWALIMU"
ni kweli kabisa wakati huo elimu ililenga zaidi kuwaogopesha watu kuepuka kupata maambukizi. saivi mambo yamebadilika sana.
 
Back
Top Bottom