Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Bk. huko watu walikufa Kijiji kizima. Yaani Kila siku wanazikwa watu watatu, wanne kwenye Kijiji kimoja kama vile kuku na kideri.
upo sahihi kabisa. zile filamu zilizorekodiwa huko bukoba kwakweli zilikuwa za kutamausha sana km ulivosema apo. walisema kuna kijiji kinakaribiana na uganda huko ndo hali ilikuwa mbaya zaidi unakuta nyumba kabaki mbibi tu amezika wanawe wote. nyumba zingine hakuna aliyebaki ni magofu tu. nyumba zingine unakuta wazazi wote wameshafariki wameacha watoto wanajilea wenyewe.
 
ni kweli kabisa wakati huo elimu ililenga zaidi kuwaogopesha watu kuepuka kupata maambukizi. saivi mambo yamebadilika sana.
Sasa hivi wanaimiza kutumia mipira,,kuwa na mpenzi mmoja,sio kuacha zinaa!!!!,,washauri nasahaa na watu wengine wa ajabu kweli kweli,, mhimu kuacha zinaa baasi,ndo ushauri bora sana.
 
Ilikua stigma ya hali ya juu sana.
Mwathirika huwezi ku-share nae vyombo huku ukiogopa atakuambukiza.
 
Sasa hivi wanaimiza kutumia mipira,,kuwa na mpenzi mmoja,sio kuacha zinaa!!!!,,washauri nasahaa na watu wengine wa ajabu kweli kweli,, mhimu kuacha zinaa baasi,ndo ushauri bora sana.
wanasema wanatumia ABC model
A - Abstain (acha ngono)
B - Be faithful (uaminifu)
C - use a Condom( tumia kondom)
 
Kulikuwa na documentary ya huko Makete aiseee; mitaa mitupu kabisa watu wamekufa ,mayatima ni wengi sana ...Ilipekelea umaskini mkubwa sana miaka hiyo.
ni kweli mkuu makete ilikuwa balaa jingine kuliliza watu sana adi media za kimataifa zilihamia uko. hali ilikuwa tete sana.
 
Kuna mtaalam anaitwa TC msingwa wa ifakara anasema anaweza kusupress viral load za HIV to non detectable
 
pia ifahamike hali hii ya maambukizi na vifo haikuwa tu kwa bongo tu. nchi zote hizi hasa za chini ya sahara kama Kenya Uganda Zambia malawi sauzi mwendo ulikuwa uouo ni mwendo wa kuzikana mfululizo KILA SIKU! na hapo unakuta kuna mamia kwa maelfu wengine wako uko mahospitalini au majumbani mwao wanaugua.
 
Pumzika kwa amani dada yangu ulifariki ukiwa mdogo sana 2003 hiyo nakumbuka ulivyoteseka nilikuwa mdogo ila sijasahau. Dada angu ulienda ukiwa na miaka 24 tu.
rip
huyo alipishana kidogo sana na utoaji wa dawa maana zilianza kugawiwa miaka iyoiyo. nina jamaa zangu nao walikata kipindi ichoicho.
 
Kulikuwa na documentary ya huko Makete aiseee; mitaa mitupu kabisa watu wamekufa ,mayatima ni wengi sana ...Ilipekelea umaskini mkubwa sana miaka hiyo.
Lamomy anasemea hii hii makete yetu ya mapembelo vavene!?,njoo ushuhudie hapa
 
Lamomy anasemea hii hii makete yetu ya mapembelo vavene!?,njoo ushuhudie hapa
Tafuta ile documentary , nyumbani tulikuwa na mkanda wake wa VHS....Kuna nyimbo pia iliimbwa kipind kile ....Walikuwa na imani kila anayekufa amerogwa .

Kionjo '' mama alikufa eeh , wakasema amerogwa ''

Kiitikio ''njooni mtufungulieni , tunahitaji upendo kwa pamoja ''
 
Duuuh basi wazee wa zamani mpo humu,, wengine wakati huo tuna 3 yrs tu hatuelewi kitu,,kushukuru tulizaliwa wazima.
 
Kuna mtu miaka ya nyuma alikuwa anajiita deception humu, natamani sana atokee nyakati hizi ambapo hofu imetanda kuhusu kukosekana kwa ARVs
Haahaa mkuu Deception na theory zake. kitambo sana hajaonekana humu.
 
Mashujaa kama Philly Lutaya wa Uganda wangejua kama zama hizi Kuna kizazi kingekuja kusema kuwa UKIMWI ni jambo feki, wangefanya zaidi kuliko walivyofanya
uyu philly bongole lutaya (rip) alikuwa star mkubwa wa muziki uko uganda. yani ni kama ivi alivyo diamond platinumz leo hii kwa apa bongo. sasa ilitokea nayey alijikuta kapata maambukizi ilikuwa simanzi kuu. akapiga moyo konde na kujiweka wazi hali yake ya maambukizi. akawa anaelimisha jamii kwa nyimbo zake kuhusu hiv. akapiga muziki adi afya ilipozorota akaaga dunia.
 
Hizi sentensi ndio huwa zinafanya watanzania tuonekane kama specie tofauti kabisa na watu wengine na kama nyani vile ambao wanaendelea kudevelop kuelekea kuwa binadamu kamili!
 
Hao wagonjwa walikondeshwa na kifua kikuu, typhoid, na wakikufa Kwa nimonia,shida ya Figo,vidonda vya tumbo kiufupi walinyanyapaliwa badala ya kutibiwa ,Kwa sasa ni ngumu kumkuta mtu kakonda hivyo Kwa sababu matibabu anapata
 
Pumzika kwa amani dada yangu ulifariki ukiwa mdogo sana 2003 hiyo nakumbuka ulivyoteseka nilikuwa mdogo ila sijasahau. Dada angu ulienda ukiwa na miaka 24 tu.
Pole sana aseh!!,lkn hali hiyo imewatokea wengi,kufiwa wapendwa wao,just imagine katika familia mko kumi,nane wanakufa mnabaki wawili tu,ilikuwa hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…