Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Naona tunarudi huko tena.Ukimwi hutakuwa tena ugonjwa wa kutaja taja
 
Naomba unijuze kwa maswali haya,1.je virusi vinavyopelekea ukimwi vipo au havipo?,2.kama ukimwi haupo kwanini wale wanaopimwa nakubainika kuwa wana ukimwi,ubainika kwao pia kifua kikuuu,kuharisha mara kwa mara, kikohozi kisichokoma,kukonda sana,mafua makali???, kwanini ni wao tu?,.
 
Naona tunarudi huko tena.Ukimwi hutakuwa tena ugonjwa wa kutaja taja
navoona kama hawa jamaa wataacha kutupatia pesa tutachangia matibabu, sasa apo ndo mtihani sana kwa familia hoehae, kuzingatia dawa kutashuka na maambukizi mapya yatapaa.
 
haya mambo ni ya kitalaam sisi wengine sio watalam tunaelezea yale yaliyotukia na tukayashuhudia wenyewe kwa macho ya uso wa nyama. nina hakika kuna watalam humu wataona hoja zako na kukujibu .

pia unaweza kupitia mijadala kama hiyo ilifanyuka humu miaka ya nyuma iliongelea sana ayo mambo uliyosema. kuna memba amezungumziwa humu akiitwa Deception alikuwa na maono kama yako.
 
Kuna mtaalam anaitwa TC msingwa wa ifakara anasema anaweza kusupress viral load za HIV to non detectable
haya mambo ya imani ni magumu kama jina lenyewe ''imani" lilivyo. kuna mwaka nazani 2009 alitokea tabibu uko loliondo kule umasaini akiitwa babu wa loliondo. uyu alidai kuwa na dawa inayotibu magonjwa 5 ikiwemo hiv.

akapata wateja wengi sana hata viongozi wengi wa serikali na wazungu walienda uko. watu wengine wengi kutoka nchi zingine wakaenda uko.

wale waliokuwa na wagonjwa kwenye haya mahospitali wakawatoa wagonjwa wao mahospitalini wakaenda nao uko. tena wagonjwa wengine wakisafiri wametundikwa drip zao za hospitali. lakini ndoivo tena bdae ikaonekana ile dawa haikuwa kitu na wale walioacha kabisa dawa walizopewa mahospitalini wengi walipotea.
 
Hao wagonjwa walikondeshwa na kifua kikuu, typhoid, na wakikufa Kwa nimonia,shida ya Figo,vidonda vya tumbo kiufupi walinyanyapaliwa badala ya kutibiwa ,Kwa sasa ni ngumu kumkuta mtu kakonda hivyo Kwa sababu matibabu anapata
siwezi kukubishia mtazamo wako kiongozi mimi sio tabibu, naeleza tu yaliyotukia wakati uo.
 
Kwanini mnabase kwenye ngono tu, Chukueni tahadhari ya kuwalinda watoto pia wasichangie vitu vyenye ncha Kali e.g wembe, sindano etc.

Na sio kila mwenye HIV/AIDS alifanya ngono.
Kuna waliopata wakihudumia wagonjwa na wengine katika ajali pia.

Mwisho aliyeleta HIV/AIDS alaaniwe.
Watu wasiokuwa na hatia wamefariki kwa uchungu.
 
Tukiacha zinaa tutaliepuka hili janga hakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…