Tukumbushane tulikotoka

Tukumbushane tulikotoka

Sijui na watoto wa miaka hii watakuaga wanakumbushia nini sasa miaka kadhaa ijayo,,,,hasa kwenye mavazi...Sijui watakuaga wanakumbuka modo,skin tyt,bikini,boxers/pents zao izi za kisasa..!!

Sijui pia nao watakuaga WAHENGA hapo baadae afu na watoto wao wawe wanasema "Wahenga walisema"....!!!

Najaribu tu kujiulza haya maswali na kuimagine lakini sipati majibu na picha nzima itakavokuaga miaka iyo ijayo.....
 
Mwaka 1985 wakati wa transition of power kutoka kwa Rais Nyerere kwenda kwa Rais Mwinyi, wengi hasa wazee wakiwaza Tanzania bila Nyerere inawezekana?

Tulianza kuona plastic shoes madukani, enzi zile ziliitwa Yondo Sister, saa za battery ziliingia, khanga za Mombasa zikauzwa madukani si tena kwa mchoro mchoro.

Ninakumbuka yellow fashion, ualikwe kwenye party umepiga yellow shoes kichwani una yellow hair band kama Madonna kila mvulana anataka kucheza na wewe.

Unakumbuka nini?
Dah...
Mwinyi + Mkapa + Kikwete + 0.25JPM ... si mchezo 😀😀😀
 
Daaah Yaani hapa mm ndio kijana mdogo kabisa Jf nzima ninayetumia huu mtandao..
Yaan kumbukumbu zangu zinaanza 2012 kurudi nyuma ndio naona zamaniii..
Nakumbuka hv tu
Chupi za Tmk
Mashati ya Nelly,Eminen,50Cent.
Mabege na viatu vya Spiderman.
Suruali za kacha,koba, kadeti.
Mifuko ya Sports na pundamilia kubeba daftari..

-Mond-
 
Mwaka 1985 wakati wa transition of power kutoka kwa Rais Nyerere kwenda kwa Rais Mwinyi, wengi hasa wazee wakiwaza Tanzania bila Nyerere inawezekana?

Tulianza kuona plastic shoes madukani, enzi zile ziliitwa Yondo Sister, saa za battery ziliingia, khanga za Mombasa zikauzwa madukani si tena kwa mchoro mchoro.

Ninakumbuka yellow fashion, ualikwe kwenye party umepiga yellow shoes kichwani una yellow hair band kama Madonna kila mvulana anataka kucheza na wewe.

Unakumbuka nini?
Mkuu heshima yako. Nami nakumbuka baada ya viatu vya Bora, tuliletewa viatu vya Bruce Lee na soncha (utanikoma saa sita) vyote vikiitwa ahsante Salim. Baadae zikaingia raba DH(dada hakija) na nyota. Kwa machekibobu kulikuwa na kiatu cha plastic (Joseph) kikiwa na mfumo wa moka. Tulitumia mafuta ya shanti ambayo ukipakaa kichwani nywele zina badilika rangi na unakuwa rafiki mkubwa wa nzi. Baadae ndio ujio wa suruali za Micheal Jackson, Zico, raba mtoni, mashati ya Juliana, n.k.
 
Hongera zenu wahenga wa miaka hiyo...nawaona AGE GO wengi hapa hahaha
 
Mmh huu uzi haunifai maana sina cha kuhadithia maana enzi zangu ni kuanzia miaka ya 2000 kuja juu
 
Dah Mbowe hotels hivi jamaa amegoma kufufua Bills sehemu nyingine ? Nshafanya maasi kule kwenye masofa Mungu anisamehe tu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaa hadi kwenye sofa za disco?
 
Back
Top Bottom