Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

1474164846680.png
 
Mwenye msaada wa kuzipata series za The Passion kina timmy,miguel, tabitha anisaidie
 
La mujer de mivida.na pia kulikua na kitu cha chuck noris walker Texas ranger kila ijumaa si mchezo ,mieleka ya akina nick freno,mysterious,chriss benat na chriss Jericho bila kumsahau sting aliekua anataka unga usoni kila jumapili ilikua nzuri sana
Wakina WCW na NWO.
Wakina Scott Hall, Machomeni, Kevin Nash, Hulk Hogan,
Mieleka ya CTN baadae ITV wakaanza kuonyesha mieleka pia
 
Katika matangazo nilokuwa nayapenda moja wapo la revola.
'Tueleze siri ya mafanikio,
Sio siri, ni revola,
Revola pekeyake?
Ndio, kwani marashi yake ni tulivu na huniweka fresh mchana kutwaa.
Yalikuwa kama matatu tofauti, ila me nilikuwa nalipenda la yule mdada alokuwa anafanya mazoezi, ile lafudhi yake ilikuwa tamu na mbwembww zake.
Jengine la maji ya kilimanjaro.
'Maji safi kilimanjaroooo'
Tangazo la colgate la watoto, na tangazo la fanta la watoto pia.
Tamthilia nilokuwa naipenda ni Acapulco bay.
Dahhhhh umenikumbusha mbali mno
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.

Dtv nimekumbuka movie ya MAGAYVER, jamaa alikuwa mwanasayansi balaaa, alafu kupigana ye hajui! Ni mapicha Picha tu!
 
Tamthilia zilioneshwa nyingi pamoja na the bold and the beatfull, nilikuwa napenda ctn wikiend action movies, ila kuna siku sitoisahau tulikaa familia na majirani tukiangalia picha ya Van Damme, ghafla wakaanza kugegedana da niliona noma. Watangazi walivuma ni wengi Akina Rukia Mtingwa, Vick Msina, John Ngayoma alikuwa anachapia sana akisoma habari, tamasha la michezo, habari na matukio aisee its a long time
 
ITV DAIMA kulikua na tamthilia kama THE BEASTS...ROBOCOP.... THE BOLD AND THE BEAUTIFUL...PASSION....TAUSI (Sugu,baraza.,mzee kasri....siti binti kasri... Nk. ) Vitimbwi vya kina Mzee Ojwang na Mama Kayayiiii.... Watoto wetu ya Eddy Sultan..... Tangazo la Revola aliloigiza Miriam Odemba.... Tangazo la Guiness Michael Power ...... African Soccer Show ijumaa usiku..... Katuni SAA kumi jioni ( Popeye and Son, wale mapacha against the shadow, nk. )
 
Back
Top Bottom