Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Jumamosi itv walikuwa na hekaya za journey to the west a.k.a brother monkey sun wukong, zhu bajie nguruwe na master shifo hsuan tsan. Pia katuni za kina john quest, silver hawks na popeye the dreamer.

Nakumbuka pia tangazo la michael power na katili hekta dekta kama movie flani hivi ya kuitangaza bia ya guiness

Kule ctn na ndugu yake cen katuni network kila saa kumi jioni. Tangazo la tritel watu wamebeba bonge la simu.

Dtv tulikuwa tunaona ligi ya uingereza kila wiki mchambuzi dakta leakey stori nyingi. Pia kulikuwa na vitimbi vya mzee majuto, mwanachia, mangushi na gladys zipompapompa
Unakumbukumbu sn mkuu
 
Hii CTN tunaijua sisi wa Dar 2,mikoani utamu huu hawakupata ladha kitambo kabla ya clouds,azam TV wala star TV.
Kweli historia ikipita haijirudii kama ilivyokuwa awali kiuhalisia.
 
Tamthilia zilioneshwa nyingi pamoja na the bold and the beatfull, nilikuwa napenda ctn wikiend action movies, ila kuna siku sitoisahau tulikaa familia na majirani tukiangalia picha ya Van Damme, ghafla wakaanza kugegedana da niliona noma. Watangazi walivuma ni wengi Akina Rukia Mtingwa, Vick Msina, John Ngayoma alikuwa anachapia sana akisoma habari, tamasha la michezo, habari na matukio aisee its a long time
Kama movie gani mkuu
 
ITV DAIMA kulikua na tamthilia kama THE BEASTS...ROBOCOP.... THE BOLD AND THE BEAUTIFUL...PASSION....TAUSI (Sugu,baraza.,mzee kasri....siti binti kasri... Nk. ) Vitimbwi vya kina Mzee Ojwang na Mama Kayayiiii.... Watoto wetu ya Eddy Sultan..... Tangazo la Revola aliloigiza Miriam Odemba.... Tangazo la Guiness Michael Power ...... African Soccer Show ijumaa usiku..... Katuni SAA kumi jioni ( Popeye and Son, wale mapacha against the shadow, nk. )
I wish warudie nyakati hizoooo daaaah
 
Umenikumbusha enzi hizo CNN wanatuletea live ya World War I kutoka katika viwanja tofauti tofauti accros Europe. Kuna mtangazaji momoja nimemsahau, mwaweza kunikumbusha.

Mniombee.
CTN au CNN mkuu?
 
Neighbor, everybody need good neighbor........ Halafu kulikuwa na mziki wa kibongo unasumbua enzi hizo sijui nani kapiga. Kukurukakala zako wewe zitakuponza acha we acha we, kukurukakala zako wewe zitakuponza brother sister.
Hii neighbor huna kakionjo kake?
 
ITV nakumbuka vipi vya MUZIKI kama vile, music kasi kasi, Rappem, Jam adelic, Rhymix, muziki muziki etc... Watangazaji Sunday Shomari, Monica Mfumia etc...
 
jumong...naikumbuka xna hii tamthilia ikikuwa inarushwa ITV nilikuwa silali kabixa mpka nione nadhani walikuwa wanaonesha j4/j5 na alhmas..ta eso ..maro .jumong mwenyewe na ssuhinho daaaah dada alikuwa mzuri aiseee...nilimpendagaa
 
CTN kulikuwa na kipindi cha hip hop kikiongozwa na Rahma Aziz ilikuwa balaa. Hiyo tisa kumi WcW Monday Nitro! Aisee NWO walikuwa wanaiumiza sana roho yangu ila kiboko yao alikuwa sting!! DTV wakati ule yaani EPL live ilikuwa kitu cha kawaida tuu mpaka walipokuja wezi DSTV. ITV tamasha LA michezo, mambo hayo ya sumbi na bocha ilibamba sana. DTV tangazo LA world link, Mussa Telecommunications. Mzee King Majuto na marehemu Mwanachia na kistuli na hotel yao ya aljawaz kariakoo
 
Kasongo hour pale DTV.vilevile walikuwa wanaonyesha ligi ya uingereza bureee
 
Back
Top Bottom