Kuna wimbo wa Sikinde ambao mwanzo anaimba Chidumule, huu wimbo kuna mtu anao?
Je kuna mtu anafahamu JINA la wimbo huu anirushie?
Penzi ni kati yake mke mume, Na hustawi kwenye Mahaba aa
Penzi ni kileo cha fikara, Wala usione ajabu nikipeeenda
Uliponikubalia tuwe mke na mume
Nilitamani Dunia isimame hata kwa sekunde moja
Ili niione nuru ya mapenzi yako
Na roho yangu iwe radhi kuwa huru
Chorus)
Penzi letu liwe moja, Lenye dhiki na faraja
Tukiishi vizuri ni Taji kwa wapendanao
Iliyobaki tusaidiane tulindiane heshima
Tuipende familia, Ndio kustawisha pendo
Beats zake zinafanana sana mwanzo na wimbo wa Koffi Olomide.

Hiyo sauti unayoisikia hapo si ya Chidumule ni ya Maxmillian Bushoke.....una kingine?
Sawa Mkuu. Ni kweli kabisa ni Bushoke na nafikiri kwa sababu siku hizi nimekuwa mpenzi zaidi wa nyimbo za Chidumule. Miaka hiyo nilikuwa namzimia sana huyu jamaa. Ni moja ya Wanamuziki wachache niliowahi kuwaona LIVE wa Kitanzania. Nakumbuka enzi hizo akiwa na BIMA aliimba ule wimbo wa Kisa Cha Messenger na ilikuwa furaha kumuona akiimba pale Amana Ilala.
Sasa waweza kunipatia TITTLE ya huo wimbo au wimbo wenyewe?
Kuna wimbo mmoja naona wote tumeushahu nadhani ulipigwa na OSS- Ndekule; uliitwa Aminani Mandari yaani utadhani ni kisa cha kweli jinsi MAx Bushoke alivyokuwa analalamika... "anakumbukwa na ndugu na jirani zakee eeenhe then Mola mlaze pema peponi roho yake, Aminani Mandari mpenzi sitamsahahu...
1.Rudi Mpenzi Zarina~NUTA JAZZ BAND
2.Lella~VIJANA JAZZ
3.Zinduna~KUMULIMULI JAZZ
4.Asmaa
5.Magreti~MARIJANI RAJABU
6.Faulata~JUWATA JAZZ
7.Magdalena Ananipa Tabu~VIJANA JAZZ
8.Paulina~URAFIKI JAZZ
9.Salza~MAQUIS
10.Anifa~MZEE MAKASSY & ORCHESTRA MAKASSY
Jamani hii thread nzuri..nitaikalia kitako niisome vizuri maana nilianza na flashback style..
Mie naufahamu wimbo wa Georgina umeniachia masikitiko, Georgina Georgina ooh!!
Belinda unagida mbwali?
Manake wanywaji woote huo ndio wimbo wao kipenzi
Binti Maringo - Juwata Jazz