Nyingine ya Wazee: Wilson Peter Kinyonga na nduguye George Peter kinyonga, Lwiza, John Ngereza, Proffeor Omar, Tom Malanga na wengineo wa Simba wa Nyika:
Halima
Naimba ya yulee mamaa,
naimba ya yule ee nyonda wangu,
Sioni sioni ii mama aa x 2 oo ni wewe halima,
Natoka mbali kijana kukufuata,
Ili mama mapatano miie na wewe,
Nia yangu waijua aa,
mama tufunge ndoa aa x 2
Nanii kijana kavunja moyo,
Ilii mimi na wewe tukosane,
naona kijana wanuna,
Fitina aa mama ni mbaya x2
Nia yangu kubwa kijana aa,
Mimi na wewe tufunge ndoa aa,
Mengi tumekwisha kubaliana aa,
mbona mama wabadilika aa, mbona mama wakasirika aa,
Halima nakuomba tafadhali ee e,
tafadhali shika ninalosema aa,
Achana na fitina wabaya, fitina wabaya x 2
Jilazimishe japo siku moja x 2
Mwenzio mimi ninakonda,
Penzi lako mama motomoto,
jilazimishe kijana siku moja x 2
Hawa wanamuziki wa zamani walikuwa wanajua kupanga maneno ya kubembeleza mwanamke, sio mchezo!