Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Sijui kama za wanamuziki wa nje ya nchi yetu zinajadiliwa ktk mada hii...
Nimeikumbuka 'Hidaya' yake Pepe Kale(RIP)....nimepoteza kipenzi changu nchini Tz,nimepoteza mkanda wa kiuno...kama kule Arushaa sijui...kama kule Morogoroo sijui....kama kule Mwanzaa Chavila nitafutiee eeh!
 
.......Huu umeimbwa na Matonya.

asante sana mammy maana naona thread ilikuwa ime-base kwenye za zamani zaidi japo sio lengo lake, kwa maana hiyo kuna Nzela (banana band)
 
Nyingine ya Wazee: marehemu Patrick Balisidya, Monte Makangila, Shabby Mbotoni, Paul Mndasha na wengineo wa Afro 70 Band 'Wana Afrosa':

Dada Lidya:

Dada Lidya ee tulipendana sana aa x 2
Imenibidi nikueleze wazi ingawaje nakukatisha tamaa x 2
uamuzi uliofanya kwa hakika umepotoka dada x2
kwa baba yako ulishasema kuwa mimi nitakuoa x 2
naona haya kukueleza kuwa mimi nimeshaoa x 2

chorus:

Mpenzi lidya ee lidya ee,
umeishachelewa lidya ee
nafasi si yako lidya ee,
jaribu mwingine utafanikiwa x 2
eee wakati unao, ee wakati unao x 2
 
...Wimbo mwingine wadau ni "Hiba" ulioimbwa na Hassan Rehani Bitchuka.
..Kibwagizo chake:.....Hiba oh Hiba oh Hiba Oh! Imekuwaje Hiba..nieleze leo....Badiliko la pendo linatia wasiwasi......lipi lililokuhudhi Hiba..."
Hakika Bitchuka ni mwimbaji mahiri...Sijui wakati huo alikuwa na bendi gani....
 
Rehema... sijui umeimbwa na nani ila una maneno haya... Rehema mama wee nakupenda sana wee kuachana nawe sitaweza unielewe mpenzi eeh, ingawa hujaamini mama aaa nakupenda rey wangu eee...


Annina
 
Nyingine ya Wazee: Wilson Peter Kinyonga na nduguye George Peter kinyonga, Lwiza, John Ngereza, Proffeor Omar, Tom Malanga na wengineo wa Simba wa Nyika:

Halima

Naimba ya yulee mamaa,
naimba ya yule ee nyonda wangu,
Sioni sioni ii mama aa x 2 oo ni wewe halima,

Natoka mbali kijana kukufuata,
Ili mama mapatano miie na wewe,
Nia yangu waijua aa,
mama tufunge ndoa aa x 2

Nanii kijana kavunja moyo,
Ilii mimi na wewe tukosane,
naona kijana wanuna,
Fitina aa mama ni mbaya x2

Nia yangu kubwa kijana aa,
Mimi na wewe tufunge ndoa aa,
Mengi tumekwisha kubaliana aa,
mbona mama wabadilika aa, mbona mama wakasirika aa,

Halima nakuomba tafadhali ee e,
tafadhali shika ninalosema aa,
Achana na fitina wabaya, fitina wabaya x 2

Jilazimishe japo siku moja x 2
Mwenzio mimi ninakonda,
Penzi lako mama motomoto,
jilazimishe kijana siku moja x 2

Hawa wanamuziki wa zamani walikuwa wanajua kupanga maneno ya kubembeleza mwanamke, sio mchezo!
 
Dalili zote zinaonesha kuwa wanamuziki wetu walikuwa na matatizo sana katika mapenzi!!! gademu!!
 
Clara ya marquees:

Clara ooh mamaa sikujua kama utanikataa eeeh, clara ooh mamaaaa...

Wazuri ni wengi nimekuchagua wewee
Miaka mingi tumeishi mimi na wee...
Nimevumilia yote ooh mamaa...
Clara eeeh nimekukosea nini maama

Clara ooh mamaa sikujua kama uanikataa eeeh
Clara ooh mamaaaaa
 
Conjesta la Nginde...

Na sasaaa lako penzi limefikia ukingoonii eeh...
Sitegemei kupenda mwingine tena, zaidi yako eeh Conjesta...

Mtoto mwenye imaani, conjesta,
Nimeamua kukupenda we pekee duniani...
 
Salaam bikira maria kutoka kwa mt cecilia mwenge...

Sisi wana wa dunia
Tukumbukee maneno
Aliyosema bikira mariaaa

Alisema tusalii
Tusali rozaali
Tupate aamaniii...

Na wasiomwamini Yesu mwokozi
Wamuamini ili waokokee
 
Judy ya Njata...

Juudy eeeh eeh
Nikupe nini uridhike
Judy eeh cha kukupa siina
Judy eeh...
Unihurumiiee maamaaaaaaa

Ufukara nilionao mamamaaaa
Ufukara umekuwa kashfa eeeh
Ya mapenzi yaangu eeh kwaako kwako eeh...
Pole mama eeh mamaa eeh
 
Sasa ndugu zanguni ngoja niende Bar nikapate za kulalia then nikija tutaendelea na Helena ya Dar International
Kwa ufupi tu inaimba...

Umasikini japo hupita kwa wanadamu
Lakini hakuna anaeupenda,
Ila ni basi mtu ufanyeje
Huna la kufanya aah maauwaa
Oooh masikini mieee

Hukufanya uwe mnyonge siku hadi siku...........................halafu ukichanga Marijani anakuja kuimba...

Kila penye uzia ooh
Basi penyeza rupiiaaaa.....
 
Oooh sory.
Kabla sijaenda Bar ngoja niwaache na nyimbo toka kwa Maquees songi linaitwa Mama maria...

Maria nyerere mama mpendwa kwaheri mama aaaaah aaaaaaaah
Pokea shukrani zetu za dhati maria Nyerere maamaaaa

Kwaaheriiiii iii maria Nyeereree mamaaaaa
Twakutakieni mapumziko mazuri pmj na maisha, marefu sana...
 
Judy ya Njata...

Juudy eeeh eeh
Nikupe nini uridhike
Judy eeh cha kukupa siina
Judy eeh...
Unihurumiiee maamaaaaaaa

Ufukara nilionao mamamaaaa
Ufukara umekuwa kashfa eeeh
Ya mapenzi yaangu eeh kwaako kwako eeh...
Pole mama eeh mamaa eeh

Mkulu,
Heshima Mbele!

Umenikumbusha 92' Hotel na akina Eddy Sheggy RIP.
Watu njat njata (Ushirika Tanzania Stars)
Mwanangu wewe mkali pia

Nakumbuka sigara zangu za mwanzo mwanzo!

Ha ha ha ha .......!!!!
 
Mwanakijiji naomba offpoint kiduchu balatanda na babadesi Sikonge naombe mistari song moja .nilikumbwa na mikasa nikawa napenda kuliimba ila sijui heading wala mtunzi

"nimekusamehe lakini sitokusau visa ulivyonitendea mama ee eeh ulinikana wakati nilpokuwa na shida ukasahau yote nilokutenda wakati unaelewa hakuna komandoo wa shida "
 
Jamani kuna wimbo nimelala naukumbuka nikasema leo nijiniwaulize kama kuna mtu anao maneno yake yote hapa aweke
Ni wa bendi ya RAINBAW kama sikosei Marehemu Eddy sheggy aliimba pia baadhi ya maneno yake...........

...........Umekua kama Helkopta...ndege isiyochagua mahari pa kutua eee...........!!!!

sasa i cant connect the following words tafadhali wakulu puliziiiiiiiiiiiiiiiii..................
 
Mwanakijiji naomba offpoint kiduchu balatanda na babadesi Sikonge naombe mistari song moja .nilikumbwa na mikasa nikawa napenda kuliimba ila sijui heading wala mtunzi

"nimekusamehe lakini sitokusau visa ulivyonitendea mama ee eeh ulinikana wakati nilpokuwa na shida ukasahau yote nilokutenda wakati unaelewa hakuna komandoo wa shida "

Mwimbaji alikuwa Komandoo Hamza Kalala. Sina uhakika na bendi aliyokuwa wakati anaimba wimbo huu. Itakuwa kati ya Uda Jazz Band au kikundi chake cha Bantu Group.
Nakumbuka hiki kibwagizo, natumai wadau wengine watakuja na mashairi ya wimbo huu.
 
Back
Top Bottom