Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Hakuna wimbo wa Vero(nica)? I swear nimewahi kuusikia sehemu
Mariamu nao hakuna?

Veronica sikumbuki ni upi. Ungeliandika maneno mawili zaidi ingelikuwa rahisi.

Mariamu upi? Ule wa Dr. Remmy (Mariam wangu, waja leo waondoka leo, wamtaka leo wampata leo)?

Sahihi ni "obeja kulumba ng'wanone"

Basukuma hawana "mwa" wana "ng'wa"

Kwa mfano Mwanza ni Ng'wanza

Mwana wa fulani ni "ng'wana mbati"

Unanikumbusha mshakaji wangu mmoja tulikuwa naye JKT. Alikuwa akisema MAJI HAYAMOMO. ukimuuliza maanda yake anadai eti kwa sababu kwa Kisukuma tunasema "Minze gatimo-mo". Nafikiri hapa inatekegemeaGA unaongelea Wasukuma wa sehemu ipi.
Kwa mfano wakati Wasukuma wengine wanasema "Ng'wana Lubasha" na jina hilohilo Wasukuma wengine na Wadakama (Wanyamwezi) tunasema "Mwana Lubasha".

Anyway, turudi kwenye nyimbo. (Samahani wengine kwa kuchepuka nje).

Sam Mangwana - 1. Maria Tebola 2. Kabibi
Samba Mapangala - Marina
Tabora Jazz Band - Zabibu, Mariam mpenzi, Asha, Dada Helena, Lemmy, Sophia Mpenzi .....
Vijana Jazz - Chiku, Sifa za Stella......
 
Binti Maringo - Juwata Jazz

TX Moshi alikuwa ni mtunzi mahiri sana jamani,karibu kila nyimbo aliyoitunga ilikuwa ni moto(ili hit hasa)

Binti Maringo

(TX)Penzi langu limekosa umaarufu kwa sababu sina hela ooh Binti Maringo,sifa za uzuri wako zilinifanya niingie kichwa kichwa bila kuuliza,sasa umekuwa dalali unaunadi utu wangu ooh Binti Maringo,sasa umekuwa dalali unaunadi utu wangu ooh Binti Maringo

(Wote)Hapa nilipofika panatosha nisijefuga ugonjwa nikakosa dawa(rudia tena)
najua nina kiu na wewe nitakunywa maji nitulie...Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

(Gurumo)Dada Kawasaki alinikanya hapa mjini nenda polepole,utavamia walanguzi wa mapenzi waikaangae Roho yako inyauke kama mti

(Wote)Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

kuna huu wa TABU sijui ni nani kauimba....ni wewe kipenzi nikupendae, kwa jina unaitwa Tabu, mwenye sura nzuri ya kupendeza, tabia na heshima yako ni ya kuridhisha, japokuwa maana ya jina lako ni matatizo kwangu mimi lina maana ya furaha na faraja,,,,,

Bitchuka na nginde hao...
 
TX Moshi alikuwa ni mtunzi mahiri sana jamani,karibu kila nyimbo aliyoitunga ilikuwa ni moto(ili hit hasa)

Binti Maringo

(TX)Penzi langu limekosa umaarufu kwa sababu sina hela ooh Binti Maringo,sifa za uzuri wako zilinifanya niingie kichwa kichwa bila kuuliza,sasa umekuwa dalali unaunadi utu wangu ooh Binti Maringo,sasa umekuwa dalali unaunadi utu wangu ooh Binti Maringo

(Wote)Hapa nilipofika panatosha nisijefuga ugonjwa nikakosa dawa(rudia tena)
najua nina kiu na wewe nitakunywa maji nitulie...Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

(Gurumo)Dada Kawasaki alinikanya hapa mjini nenda polepole,utavamia walanguzi wa mapenzi waikaangae Roho yako inyauke kama mti

(Wote)Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

(Gurumo)Dada Kawasaki alinikanya hapa mjini nenda polepole,utavamia walanguzi wa mapenzi waikaangae Roho yako inyauke kama mti

(Wote)Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika

Ha ha ha...!

Unanikumbusha mbali,wakati sie wengine wagonjwa wakupenda alafu hatuna bahati ukishaachwa (kupigwa kibuti),unajiliwaza kwa............

"............Dada Kawasaki alinikanya hapa mjini nenda polepole,utavamia walanguzi wa mapenzi waikaangae Roho yako inyauke kama mti..........

.................Maringo Binti Maringo nitakukukmbuka daima,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika,kwenye kitabu cha kumbukumbu mateso yako nitaandika..................."
 
Kalunde - Msondo Ngoma

"Baba alinambia nikaoe nyumbani"
Sasa yamenikuta na huyu dada Kalunde
 
Nimekuwa nikitafuta wimbo zilipendwa unaitwa 'Roza' ama 'Mpenzi Roza' ulioimbwa na Tanga International. Cha ajabu nikiulizia huwa nakuta watu hawaufahamu. Niliwahi tembelea banda la TBC pale Mnazi Mmoja nikaiulizia hawakuufahamu. Wakati nausikiliza nadhani nilikuwa kwenye teens yaani late 70s ama early 80s. Nani anaweza kunisaidia nipate wimbo huu kwani wakati ule unapigwa niliupenda sana?
 
Asante sana balatanda na sikonge pia JF idumu zaidi mambo yenu nayakubali kwa sana
God bless you all
 
Neema mtoto wa songea - Bima Lee
. .. Usiniache peeeke Neema, usifate wayasemayo wafitini ah! wako mbele mbele kuharibu mapenzi yetu mimi na weeee!!

Dada Asha- Tabora Jazz (Shem Kalenga)
 
Salama by Jabali la Muziki

Wapi salama, salama nakuomba
salama nakwita mamaa
umenipa machozi, machozi yasiyokwisha
nifanyeje mwana mamaa

nikilala naota sura yakoo
nikitembea nasikia waniitaa
nageuka sikuoni mwana mamaa
nauliza uko wapi mwana mamaa

Salama! Duh, huyu ndiye wangu....
 
Christina Moshi sikiliza melezo yangu katika wimbo mamaaa,
Naelewa Penzi li bado ni changa, usije tena ukabadilika baadae,
Tulipokubaliana kwa hiari tulikuwa wawili, watatu Mungu wetu *2

........Pendekezo langu kwako kwako uwe kama benki,
........benki mahala pa usalama
........Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe, Moshi ee mamaaaa!
Uwezo sina ningekununulia gari ,bali matatizo madogo hayatonishinda,
Nitajipigapiga ili niyatatue, sababu jungu halikosi ukoko......

Hii nyimbo ilinipagawisha sana wakati wake...

...halafu Skassy kasambula, Muhiddin Gurumo na Bitchuka 'Super Stereo' wanamaliza kwa rapu ya;

'hebu sikia maneno ya kuambiwa na wana ndekule, moshi ee ee ndekule,
hebu sikia maneno ya kuambiwa na wana ndekule, moshi ee ee ndekule.
 
Hii ni ya Wazee: Jabali la Muziki Marijani Rajab. David Musa, Christian Kazinduki na wangine wa Safari Trippers 'Wana Sokomo' na

Mkuki Moyoni:

Mpenzi wangu nakueleza, unavyofanya sasa si vema,
Uaminifu wako umeupoteza, kwa kutotimiza ulivyosema,
Naona kweli kama unacheza, hebu jirekebishe mapema,
Unanitesa Unaniumiza Unanichoma Mkuki moyoni x2

Ukiona ving'aavyo jihadhari, usije jitia katika hatari,
Kwani vyote ving'aavyo si dhahabu, hata almasi hufanana na zabibum
wewe wanifaa wakati wa dhiki, usiponishika sisalimiki,
Moyo waniuma mi nakueleza, unanichoma mkuki moyoni,
uunanitesa unaniumiza unanichoma mkuki moyoni x 2

chorus

Niingekuwa kama sikupendi nisingalisumbuka kwa mapenzi,
Usidhani najipendeleza kwa kuwa nashindwa kukueleza,
mapenzi yaako sitayaweza wapenda pesa zitakupoteza,
badili mwendo huo nakueleza uzidishe uzuri wa tabia x 2
 
Kuna wimbo mmoja nimesahau jina la huyo wanayemwimba lakini upo hivi
'..........uwezo mwingi walionao wazazi wako wengi wao huwa wakiringaaaa......halafu unaishia mwadela!!' naomba mwenye lyrics pleeeeease
 
Hii ni one of the best threads ever!! Asante mwanakijiji kwa kutukumbusha. Muziki ulikuwa zamani ulikuwa na mafunzo na maadili kwa jamii. Once again thank you mwanakijiji
 
Duh.. hadi nimesikia machozi kunilenga. Kwa sababu, hizi nyimbo hazikumbushi burudani tu bali zinakumbusha muda, wakati na mahali. Kuna nyimbo ulikuwa ukizisikia basi uko njiani kwenda home lunch au ndiyo mida ya kutoka kujob. Na zaidi zinakumbusha vile vipindi vya kuomba wimbo ambapo kulikuwa na waombaji wimbo ambao utadhani ulikuwa unawajua..
 
Nimeongeza pale Pamela.. lakini najiuliza hivi ziko "Pamela" mbili au moja?
 
.......Anita Anita wangu yele lelelleel hieeeeeeeeee........
Nasukuma sukuma ili siku ziende urudi nyumbani tuishi pamoja.....
 
Back
Top Bottom