Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Mkuu mimi nime move on japo sijutiii kuwa nae, aliniacha bada ya yy kupangiwa kazi serikalini Mwanza wakat mm npo Dar, so nikamkosa hivyo
Yani hivyo tu ndio upewe talaka?
Ebu kuwa mkweli hukuwahi kuchepuka mkuu?
Na sasa hivi jimbo liko wazi au lilishapata muwakilishi?
 
Upo sahihi, mwishowe watoto wanakuwa wahanga kwa mambo yasiyowahusu.

Hata kama ni lazima mtengane suala la watoto namna watakavyopata mahitaji yao lijadiliwe na lipatiwe ufumbuzi.
Wengine hata hawajali kuhusu watoto. Kabla hata talaka wameshaanza mahusiano mengine. Bora muache watoto wakue kwanza ndio muwe na mahusiano ya wazi.
 
😂😂
Utakuwa poti bila shaka..
Maana kwa lugha ile hata msamiati wa neno 'talaka' hakuna!
 

Copy that
 
😅😅😅 Naona umetuchamba mno si viboro dinda
 
Maisha kabla ya ndoa ni mazuri sana kwa sbb ya uwepo wa nidhamu ya hali ya juu na maigizo ya kutosha.
Maisha baada ya ndoa kiburi, dharau, jeuri vinastawi na kuwa mahali pake, na kufuta uwepo au umuhimu wa ndoa.

Ukweli ni kwamba talaka, zina faida zake hasa nyakati zetu hizi. Badala ya kuishi kwenye mazingira hatalishi kwa afya ya akili, mwili na roho ni bora kila mmoja akatafuta njia yake.
TALAKA NI BORA KULIKO WATOTO WASIKIE BABAYAKO ALIUA MAMA YAKO!
 
Wengine hata hawajali kuhusu watoto. Kabla hata talaka wameshaanza mahusiano mengine. Bora muache watoto wakue kwanza ndio muwe na mahusiano ya wazi.
Yaani nikose kufurahisha nafsi yangu kisa watoto. Kwani maisha ni watoto tuu?
 
Huwezi endelea kukumbatia kifo eti kwa ajili ya mustahbali wa watoto.
Niliandika Ili watu wajue kuwa kutokuelewana ndani ya nyumba matokeo yatakuwa mabaya zaidi kwa watoto wao enfapo watafikia hatua ya kuachana, kama ni ndoa iliyoshindikana baaasi sijahimiza watu waendelee kuwa pamoja
 
Mkioana nyota zenu zinafanana ni ngumu talaka mtazisikia kwa wengine.Mtaishi zaidi ya ndugu plus kufanana sura.
Mkuu ni kweli kabisa nasaidiki, lakini nadharia hii hukutana na kizingiti cha muda na mazingira yenu, kadri muda unavyoenda ndipo picha halisi kati yenu huonekana. Pia mazingira mnayoishi, wanandoa mnapoelewana huwaga kuna hasadi, fitna na husda sana toka kwa watu wanaowazunguka kwa maana ya majirani, marafiki na ndugu bila hata ya kujua zimetokea vipi.

Mtajikuta siku mnaingia mtego kirahisi sana na kisha mkaachana, huwezi amini anaewaachanisha anaweza kuwa hata mama au baba yenu mzazi, eti kwasababu ya mambo ya kijinga. Katika maisha yenu ya ndoa omba sana muishi katika misingi ya dini haswa ( kwa kumuogopa Mungu), hekma, uvumilivu na ustahamirifu pamoja heshima.

Ndoa ni nzuri sana lakini haijawahi kuwa rahisi hata kidogo ina mambo mengi na mitihani mingi sana, kuivuka inahitaji nguvu ya Mungu pekee pamoja na hekima iliyopitiliza. Talaka haijawahi kuwa suluhisho la matatizo kwenye ndoa bali ni tatizo haswa mnapokuwa mmeshazaa. Talaka ni halali kutolewa endapo tu kuna ulazima na mazingira ya kufanya hivyo, vinginevyo talaka si kitu cha kukimbilia kabisa.
 
Ni hatari sana..!! Nina ndugu yangu, maneno ambayo mwanamke aliyaongea mahakamani hakutegemea hata kidogo..!! Mwanamke ndo aliyekuwa anadai talaka kwa nguvu zote. Ilifika point akatakiwa aeleze sababu za kudai talaka. Moja ya sababu aliyoitaja ilikuwa ni kutakwa kinyume na maumbile..!! Jamaa yangu ilimshitua ile mbaya..!! Wala hakutegemea hilo..!! Na kile kitendo cha kujikusanya baada ya kutawanywa na maneno hayo, watu wote pale mahakamani walipigwa na butwaa wakiamini madai hayo ni ya kweli..!! Mwishi wa siku waliachana na athari zake kila mmoja kwa wakati wake anazipata hadi hivi sasa.
 
50/50 kesho kutwa nauza nyumba za wanandoa na kiwanja, ni kizuri balaaa, mahakama haijawaji kosea, huwezi mfubaza binti wa watu ukamzalisha akakondeana afu unataka aondoke mikono mitupu
Hapana ni 50/50

Athante mahakama
 
Roho ya talaka haiwezi kuja kama hamjapata watoto. Lengo la talaka ni Ili watoto waharibike kwa kukosa msingi uwepo wa baba na mama Ili waweze kubalance saikolojia yao maishani.
 
Umeandika kwa huzuni sana bro toa talaka tembea mbele nakuhakikishia ukirudisha moyo eti kwa kuwa mna watoto utapigwa tukio ambalo duniani na mbinguni hutasahau huyo mtoto wa miaka 7 sheria inakurusu kuwa nae miaka hii kwa sasa walezi wa watoto wamekuwa ni wanaume na sio wanawake.
Mwanamke ambaye mmetengana mwaka then leo umrudishe eti watoto bro nimekaa pale episode ya pili itakayokukuta ni balas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…