Ndoa ni hiyari iliyo halalishwa na Mungu.
Tena ndoa ni kiapo mbele za Mungu.
Binadamu tumekuwa na kawaida ya kuvunja,
-- ndoa zetu,
--Ndoa za ndugu zetu,
--Ndoa za marafiki na jamaa zetu bila kujali.
Elewa tunafanya makosa makubwa sn mbele za Mungu.
Ni kweli kuwa ndoa inafika mahali inafifia na kukosa mapenzi ya mke na mume.
Lakini ni vizuri zaidi wahusika wakakaa na kujadili jinsi gn wataweza kurudisha mapenzi kwenye ndoa yao,
na sio kuvunja ndoa,
Tena bila sababu za msingi.,,
Talaka sio kitu kizuri ndg zangu,
Kitendo cha mwanaume kutoa talaka,
au mwanamke kuomba talaka,
Ni Sawa na kuvunja ahadi ambayo mliiweka mbele za Mungu kwamba mtapendana kwa shida na raha kwa maisha yenu yote.
Talaka huwa ina kawaida ya kurudi kwa wanandoa na kumuhukumu yule mkosefu,
Kuna mwanamke ambaye yeye ndy chanzo cha ndoa kuvunjika,
Lakini bado anadai talaka kwa nguvu zote,
tena kwa kashfa na vurugu.
Mwanamke huyu hatopata faraja ya ndoa huko aendako.,
Talaka itamrudia na kumchapa haswa.
Kuna mwanaume ambaye yeye ndy chanzo cha kuvunjika ndoa,
Na bado anatoa talaka kwa kosa alilofanya yeye.
Huyu mwanaume hatobaki salama huko aendako.
Talaka itamchapa haswa,
Mwishowe kujutia maamuzi ya talaka.
Talaka unatakiwa uitoe ukiwa upo very calm na sio hasira .
Unahitaji umakini Sana kwenye hili.
Talaka inaweza ikawa ndy mwanzo wa kuvurugikiwa maisha yako au mwanzo wa mafanikio,
Inategemea ni Kwa jinsi gani mmeachana.
Ushuhuda
Nilibahatika kuoa mwanamke fulani mrembo sn miaka 17 iliyopita.
Nikiwa bado kijana mdogo sikuwa na kipato kizuri ,
nilikuwa na kipato cha kawaida cha kuunga unga.
Yule binti alinisumbuwa sn sababu ya uzuri wake.
Nilijitahidi kumtunza kwa kadiri ninavyoweza,,
lakini mwisho wa siku alianza visa na kuomba talaka,
Tena kwa vurugu,
kashfa nyingi,
Alikwenda mbali zaidi na kusema mimi sio type yake,
ninamfuja na kumbana bana ili asiolewe na wanaume wenye pesa.
Alilazimisha talaka kwa matusi na kashfa ,
Alikuwa akitoka asubuhi na kurudi jioni tena amelewa na sijuwi pombe amenunuliwa na Nani,
Nikiuliza atajibu kashfa tupu,
"Nilishakwambiya niache na maisha yng wewe unaning'ang'ania nini?"
Aliponambiya maneno haya nilipata uchungu Sana moyoni
Nikiifikiria ndoa yng bado hata mwaka haijafikia,
Sababu nilikuwa na mapenzi mazito Sana kwake ,
nilishindwa kufanya maamuzi ya haraka,
Kwa kweli nilimpenda sn mke wangu.
Nilijitahidi kuwaeleza wazazi wake tatizo,
Lakini kwa majibu aliyonijibu mama mkwe nikagunduwa ,
hata mama mkwe pia hanitaki niishi na binti yake.
Sababu ya kipato changu duni ,,
Yaani mke wangu nimekuoa kwa mahari halafu Leo unambiye hunitaki?
Kwamba siyo type yako?
Hunipendi tena?
Niliitoa talaka kwa uchungu Sana.
Now ni miaka 17 ya talaka lakini still yupo mitaani anahangaika kupata Mwanaume hata wa kuishi nae store hamuoni.,
Hata mtoto wa dawa hana,
Kapauka kama mguu wa Teja.
Tusipende kutoa/ kuomba talaka kama wewe ndy mkosefu.
Jishushe/ omba msamaha maisha ya ndoa yaendelee..
Sent using
Jamii Forums mobile app