Wale vibaka wangu walikuwa wajinga sana..........2001 hiyo nimetoka zangu kupiga liquid narudi home kama saa 7 hivi ucku, nilipokuwa naishi kuna umbali kidogo kutoka barabarani, dereva taxi kanishusha nikaanza kukata vichochoro kuelekea nyumbani, ghafla nikamulikwa usoni na tochi yenye mwanga mkali sana halafu ikatoka amri kali eti:- simama hapo hapo na ujisachi mwenyewe utoe kila ulichonacho mfukoni........yani sikujiuliza mara mbili mbili, niligeuka kwa kasi na kufyatua mbio kali sana ambazo sijawahi kukimbia.
Kuona ivo na wao wakaniunganishia kuanza kunikimbiza halafu mbaya zaidi wakaanza kuniitia mwizi, mi kusikia ivo nikapunguza mwendo hatimae nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, kuona natembea na wao wakaanza kutembea na hawapigi tena kelele za mwizi, nilipoona wananikaribia nikachomoka tena mbio kali......zoezi likarudia lile lile la kupigiwa kelele za mwizi, bahati nzuri natokeza barabarani na gari ya police hii hapa, nikawaelezea tukarudi hadi walipoanza kunikimbiza lakini hakuna mtu, basi wakanisindikiza hadi nyumbani.
1993 Tabora hiyo jamaa yangu mmoja kaja mjini kupokea pesa yake ya mauzo ya tumbaku, akawa na mipango mingi balaa ikiwemo kununua baiskeli mpya, kununua radio kaseti ya Lasonic na kuongeza mke wa tatu..........hakuna hata mpango mmoja uliotimia, usiku wa hyo aliibiwa pesa yote sh 100,000/= na baamedi aliyelala nae gesti (nadhani ndo alikuwa anamfanyia intavyuu kama anafaa kuongezwa kuwa mke wake wa tatu, tangu siku hyo jamaa yangu huyo alishikwa na uchizi akatoweka nyumbani hadi tulipokuja kupata taarifa za kifo chake cha kugongwa na gari.
Juzi juzi tu hapa kuelekea kipindi cha sikukuu za krisimasi na mwaka mpya kundi la vibaka wapatao kama 17 hivi walivamia kwa jirani yangu aliyekuwa kauza kagari kake kamechakaa chakaa kwa sh milioni 6, wale wapuuzi wakataka kuja kuchukua zile pesa kama vile walimuwekeza........kwa mara ya kwanza ndo nilikatumia vizuri ka manati kangu ka kizungu, nilimkongoroa goti mmoja wao na wengine wakakimbia, yule tulimmalizia pale pale kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali.
2007 kuna majambazi yalivamia mtaa flani wenye maduka mengi, sasa ile tabia ya mlinzi mmoja analinda karibu maduka 40, wakamkamata mzee wa watu wakaenda nae hadi kwenye mojawapo ya maduka anayolinda wakamkazimisha aanze kuvunja, zoezi lilipokamilika wakamlazimisha aanze kusomba vitu anapakia kwenye gari la majambazi.......ile wanamalizia mara paaaaap na mwenye duka akatokeza akamuona yule mzee mlinzi wa duka lake yupo kwenye harakati kupakia vitu kwenye gari ya wale wezi, jamaa akafyatua risasi hewani, wale wezi wakawahi kwenye gari yao ili wakimbie, na yule mzee mlinzi na akaona hapo sio pa kukaa tena, akadandia kwenye gari ya wale wezi akaondoka nao...........!!!!!!!!!!!!!!!!
komando kinjekitile ngwale