Mkuu risasi isikie tu ,ile bomba ilivyopigwa kila kitu kilikuwa kimya mpaka mbu na kwa wenge lile nilidhani wajomba ndio wanaingia kwetu kumbe kwa majirani huko.Nikajua ulienda kusaidia, kumbe ni baada ya kugundua mlango umefungwa ikabidi ujiongeze
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaa haaaaaaaaaaaaaWale vibaka wangu walikuwa wajinga sana..........2001 hiyo nimetoka zangu kupiga liquid narudi home kama saa 7 hivi ucku, nilipokuwa naishi kuna umbali kidogo kutoka barabarani, dereva taxi kanishusha nikaanza kukata vichochoro kuelekea nyumbani, ghafla nikamulikwa usoni na tochi yenye mwanga mkali sana halafu ikatoka amri kali eti:- simama hapo hapo na ujisachi mwenyewe utoe kila ulichonacho mfukoni........yani sikujiuliza mara mbili mbili, niligeuka kwa kasi na kufyatua mbio kali sana ambazo sijawahi kukimbia.
Kuona ivo na wao wakaniunganishia kuanza kunikimbiza halafu mbaya zaidi wakaanza kuniitia mwizi, mi kusikia ivo nikapunguza mwendo hatimae nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, kuona natembea na wao wakaanza kutembea na hawapigi tena kelele za mwizi, nilipoona wananikaribia nikachomoka tena mbio kali......zoezi likarudia lile lile la kupigiwa kelele za mwizi, bahati nzuri natokeza barabarani na gari ya police hii hapa, nikawaelezea tukarudi hadi walipoanza kunikimbiza lakini hakuna mtu, basi wakanisindikiza hadi nyumbani.
1993 Tabora hiyo jamaa yangu mmoja kaja mjini kupokea pesa yake ya mauzo ya tumbaku, akawa na mipango mingi balaa ikiwemo kununua baiskeli mpya, kununua radio kaseti ya Lasonic na kuongeza mke wa tatu..........hakuna hata mpango mmoja uliotimia, usiku wa hyo aliibiwa pesa yote sh 100,000/= na baamedi aliyelala nae gesti (nadhani ndo alikuwa anamfanyia intavyuu kama anafaa kuongezwa kuwa mke wake wa tatu, tangu siku hyo jamaa yangu huyo alishikwa na uchizi akatoweka nyumbani hadi tulipokuja kupata taarifa za kifo chake cha kugongwa na gari.
Juzi juzi tu hapa kuelekea kipindi cha sikukuu za krisimasi na mwaka mpya kundi la vibaka wapatao kama 17 hivi walivamia kwa jirani yangu aliyekuwa kauza kagari kake kamechakaa chakaa kwa sh milioni 6, wale wapuuzi wakataka kuja kuchukua zile pesa kama vile walimuwekeza........kwa mara ya kwanza ndo nilikatumia vizuri ka manati kangu ka kizungu, nilimkongoroa goti mmoja wao na wengine wakakimbia, yule tulimmalizia pale pale kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali.
2007 kuna majambazi yalivamia mtaa flani wenye maduka mengi, sasa ile tabia ya mlinzi mmoja analinda karibu maduka 40, wakamkamata mzee wa watu wakaenda nae hadi kwenye mojawapo ya maduka anayolinda wakamkazimisha aanze kuvunja, zoezi lilipokamilika wakamlazimisha aanze kusomba vitu anapakia kwenye gari la majambazi.......ile wanamalizia mara paaaaap na mwenye duka akatokeza akamuona yule mzee mlinzi wa duka lake yupo kwenye harakati kupakia vitu kwenye gari ya wale wezi, jamaa akafyatua risasi hewani, wale wezi wakawahi kwenye gari yao ili wakimbie, na yule mzee mlinzi na akaona hapo sio pa kukaa tena, akadandia kwenye gari ya wale wezi akaondoka nao...........!!!!!!!!!!!!!!!!
komando kinjekitile ngwale
Kumbe ulikuwa wewe mwanangu, hahahaaaaa.Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
Yaaan hapa sijaelewa...ulipanda juu ya pikipiki kama Vandamme kwenye ile movie ya Hard target alivyorukia treni?[emoji848][emoji848]Nakumbuka mwaka 2011 Siku Ya Eid pili nilienda Wet 'n' Wild Beach with Family, ilivofika Jioni saa 12 rafki zangu wakaniforce Niende South Beach... Nyumbani nilikatazwa kutoka ila sikuskia na Nilikosa gari ya kunipeleka kila mtu analalamika lile nyomi la magari Kigamboni siku za Skukuu inakua ZOGO.... Basi nilitaka kukodi Taxi lakini mwenye Taxi alikataa kunipeleka kigamboni akidai kwamba kuna foleni sn labda aniache kivukoni halafu nikishuka Pantoni ntachkua Bajaji au Pkpk mpk South Beach. Nikafata ushauri wa mwenye Taxi Sikujua km kuna Mabalaaa huko Kigamboni siku za Skukuu maana siku za Skukuu sisi huwa tunaenda Beach za hukuhuku hatuvuki.
Nilivoshuka Pantoni ilikua mida ya saa 1 usiku mapema tu, watu kibao km mkutano wa siafu! Bajaji zilikua hamna kituoni zilibaki pkpk tu, ikabidi nipande pkpk nilikua nimevaa Jeans, Blauz refu na Handbag yangu kwapani magari yalikua yanatembea taratibu mno hakuna pa kukanyaja Watu wengi walikua wanatembea kwa miguu, kumbe wale wanaotembea wengi ni wezi wamejichanganya kwenye umati wa watu. Njiani nilikua naona wanaharass wanawake na kuwashika shika, mara gafla nikashtukia mwanaume mmoja anaivuta handbag yangu, sikumuachia na mm nikawa naivuta.. Vuta nikuvute hatimae nikamshinda. Ndio yule Bodaboda ananiambia ooh 'samahani Dada nilisahau kukutahadharisha km kuna wezi shika vzr mkoba wako,' nageuka nyuma yule mwizi anaikimbiza pkpk yetu tena yupo na wenzie km 3 hivi na mbaya zaidi foleni kubwa mno magari yanatembea very slowly, nilichanganyikiwa sikujua hatma yngu itakuaje, nikageuka upande wangu wa kulia kulikua kuna gari (pickup) ipo kwenye foleni pia lakini ya Kurudi mjini yaani inaelekea magogoni, (nyuma kwenye hio pickup kulikua kuna watoto wamekaa km 4 hivi wadogo) nilijishtukia tu nimesimama juu ya Bodaboda nikamwambia mwenye Pkpk asogeze karibu na ile gari nikairukia ile gari ya watu mwenye bodaboda ananidai hela yake nikamlipa kisha nikamwambia mtoto mmoja aikalie handbag yangu ili aifiche, wale wezi walivofika walizunguka ile gari wanatafuta Handbag yangu hawaioni Bahati nzuri Dereva wa hilo gari akashuka alikua mtu mzima na ana mwili kiasi akawauliza mnataka nn kwenye gari yngu? Wakakimbia, yule Mzee akaanza kunihoji maswali nikamuelezea mkasa mzima wakanionya yy na mkewe siku nyengine nisirudie tena kwenda kigamboni siku za skukuu bila gari ya Family ni hatari. Tena walinambia una bahati sn sisi tulikua tunatoka Dar es salam Zoo, tulikua hatutaki kupita hii njia, tulipanga tuzunguke njia ya Mbagala kukwepa foleni ila nashangaa sielewi kitu gn kimenipitisha huku kumbe Mungu alipanga tuje tukunusuru ww. Walinifikisha mpk nyumbani na wao wakaendelea na safari yao, Dah. Mwenyezi Mungu awazidishie kheri popote walipo.
Hahaa huyo mama mbona hakuendelea kudai !?Mwaka 2007 asubuhi tukiwa kwenye daladala kufika buguruni mama mmoja kabaini simu yake imechomolewa na kibaka na anauhakika kibaka hajashuka akauwasha moto kuwa aliyeiba simu hajashuka akamwambia dereva tafadhali twende polisi akajitokeza Kaka mmoja akamwambia yule mama simu yako ni Aina gani na ni Sh.ngapi mama kajibu Nokia elfu sabini
Kaka akazama mfukoni akatoa laki moja tusiende polisi maana anaharaka saa hiyo tumekaribia mataa Buguruni gari ya Gongolamboto hiyo.
Mama kajibu sitaki laki line yangu instead majina ya wateja wangu wa samaki sitaki laki yako nataka simu yanguu twende polisi
Huyo aliyekua anataka kutoa laki alikua siti ya mbele karibu na dereva, basi Hari ziliporuhusiwa alitoa bastola akamuelekezea dereva akamwambia hatuendi polisi endesha gari kuelekea tazara bwana red Kumbe hakuwa peke yake huku kwenye siti niliyokaa Mimi Kumbe nimekaa na mwenzie naye akatoa bastola akaiinua juu akiamuru tutulie
Ulimi Wang ulikua wa moto mdomoni mpaka ninaufeel nilitetemeka Sana dereva alinyoosha mpaka Around uwanja wa taifa wakashuka jamaa wanne na Makoti makubwa wakaenda zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kigamboni kwa vibaka ndio kwenyewe!.....madenti wa IFM si wanachukuaga huko vyumba vya Bei rahisi, full kubakwa hukoo[emoji17]Kigamboni kuna wezi sana sijui kipindi hiki,nakumbuka nikiwa nakaa hostel kigambon siku hiyo nimewahi kutoka chuo kama saa.sita hivi mchana nimeshuka kwenye panton pale natembea mdogo.mdogo upande wa kulia wa barabara kuna dada mbele.yangu tushafika mbele kabisa huku walikuja vibaka kwa nyuma yangu speed wakampora yule sister pochi wakavuka barabara wakaingia kwenye lile pori la jeshi kule beach tulipataga story wakienda huko usithubutu kuwafuata.
Siku nyingine mchana hivyo hivyo kuna mzungu alijichanganya akaenda kule kupiga picha alitoka.kule damu.mwili.mzima walimkata na visu mkononi usoni wakachukua camera yake. Karibia kila leo kulikua na tukio
Story tamu lkn ndo sijakuelewa yaaan[emoji134][emoji134][emoji134]Kuna jamaa mmoja alikuwa askari kabisa ila kumbe ana kazi zake za ziada
Sasa siku hiyo akamchukua dereva tax ambaye mara nyingi wanambeba
Wakaondoka wakaenda zao jamaa anaenda kufanya tukio kwenye sheli moja
Dreva tax akaachwa kwenye gari
Ghafla anashangaa yule askari anakuja mkuku kuingia kwenye gari ,Dreva tax akabakiwa na mshangao jamaa kamuambia ondoa gari akawa haamini askari ni jambazi ...Ile kusuasua jamaa akamfumua risasi ya bega dereva tax halafu akatokomea
Basi jamaa kajikongoja kufika kituo cha Polisi kutoa taarifa ,Polisi wakakataa kumfungulia wakamuambia ni wewe ....Tumeiskia hiyo mashine inavyolia
Msaada tutakao kupa simu hii hapa wapigie ndugu zako wakupeleke hospital
Pf3 tutakuletea kesho hospital.
Yule jamaa sijui alikuwa na Silaha ya aina gani mpaka polisi wakasema hiyo ndio yenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tunaweza tukawa tunafahimian mtendel maeneo yangu hayo mm mwenyewe jamaa walishwahi kunikosakosa nduta paleMwaka Jana tulikua tunatoka kasulu mida ya jioni tulikua watu saba hivi kwenye cruiser tunaelekea mtendeli. Kwa wanaoifaham hii njia kuna utekaji magari sn, kwa hiyo mazungumzo ya kutekwa yalitawala na kuulizana kama kila mtu ana hela angalau kuanzia elfu 20 ili msala ukitokea angalau uwe na cha kuwapa LA sivyo utachapwa vibaya. Safari ikaendelea huku hofu imetawala, tukaipita malagarasi salama maana ndio eneo hatari zaidi, tukaendelea na safari hapo ishafika SAA mbili kasoro na angalau amani ikatawala. Sasa kuna eneo moja linaitwa nduta nako huwa ni hatari kwa matukio ile tunaimaliza tu tukaliona gogo kubwa limewekwa katikati ya barabara dereva akasema hapa tayari, lakini akapata ujasiri wa kulipita pembeni, baada ya kama dakika moja tukalipita fuso mbele yetu kwa kasi tukaenda kusimama mbele kuna kijiji dereva akaenda kununua maji. Tukiwa pale baada ya muda lile fuso tulilolipita njiani likatukuta pale kijijini. Yule dereva wa fuso akaja kutugongea dirishani huku yupo tumbo wazi na kaptula akawa anaongea kama kapagawa akasema yani nyie mna Mungu. Kumbe tulipowapita ndo walikuwa wahanga wa lile gogo na majambazi walikuwa bado wapo eneo LA tukio wamejificha coz waliposikia gari letu likija wakadhani ni askari doria hivyo ikawa pona yetu. Ila walimpiga yule dereva vibaya wakampora nguo na kila kitu, alikuwa na mpenzi wake naye wakamvua akabaki na sidiria tu mpaka wigi wakamvua, aisee nguvu zilituishia kila MTU alibaki na butwaa dereva akaondoa gari. Nakumbuka tulikua kimya ndani ya gari mpaka karibu tunafika nyumbani ndo akili zikakaa sawa tukaanza kuambiana kwa nn hatukuwasaidia wale watu hata hela kidogo ya kununua nguo au kumpa yule Dada angalau mtandio ajisitiri. Yaani kwa kweli sikulala karibia wiki lile tukio linanijia nawaza kama tungetekwa na kubakwa ingekuwaje. Toka siku hiyo sitakaa nitembee hiyo njia kuanzia SAA nane mchana maana ni hatari mno.
Mi sina gheto ila na Mansion mkuu...Geto lako lipo pande zipi hapa mjini ?
Mabibo sehemu gani....karibu na muleba?Kwa sasa nipo mkoani ila nenda mabibo mwisho unanyanyua vyuma free,ulizia kwa mama Felix near Chabruma Bar utaelekezwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Mmh!! Heb nambie kwenye ki vitz unaingiaje chini ya uvungu wa gari??Huyo dada ambaye mume wake alishuka kwenye gari n kwenda kujaribu kutoa gogo barabarani huo sio uanaume ni ubabe usio na akili..
Maana ilikua usiku hujui adui yupo wapi ana siraha gani wewe unashuka kwenda kusogeza gogo wangemshot kwenye tako..
Mwanaume sio mabavu tu mwanaume ni pamoja na kutumia akili nyingi kwenye tukio la ghafla.
Ni bora wangepak gari na kushuka chini kulala kwenye uvungu wa gari
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Mkuu umenichekesha sanaWazee wa kazi walivamia kwa jirani yetu alikua ametoka kuuza gunia zake za mpunga,Kahama hiyo. Picha linaanza mida ya saa mbili mbili za usiku.Home nipo mimi ,bibi na mbwa .Mimi nimekaa nje ,bibi anaunga unga mboga maharage kwenye jiko la mkaa.Bwana wee ikavurumushwa risasi huko ,kwa lile wenge bibi akapiga katafunua chungu cha maharage na moto akamwagia maji kisha kwa speeed ya umeme ndani akafunga mlango akazima taa zote.Mimi nimebaki nje peke yangu kwa mbinu na medani za kivita nikavua shati nisionekane kisha nikajisunda kwenye jalala kimya.Baada ya sereka kuisha tafuta sana mbwa kuja kumkuta kumbe na yeye kaingia ndani zamani sana yuko chini ya uvungu wa kitanda.
Mmh!! Heb nambie kwenye ki vitz unaingiaje chini ya uvungu wa gari??