Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Sidhani kama unafahamu tofauti ya mwizi au wezi na jambazi aisee! Hao uliokutana nao katika matukio hayo ni wezi na sio majambazi, mziki wa (ma)jambazi sio wa kitoto aisee! Nikiwa na muda nitasimulia!
Tunasubiri mkuu upate muda, tupate ushuhuda wako. Tuzidi kujifunza na kuchukua tahadhari.
 
2017 .siku hiyo tulikua geto tumekaa tunapiga story.gafla tukasikia kishindo

Kuchungulia nje tukaona njemba mbili zinapita kwa kasi huku zimebeba mfuko wa salfet yani mmoja kabeba kushoto na mwingine kulia.

Kuona hivyo tukachukulia poa na kuendelea na story zetu.

Gafla baada ya dak15 baba wa jamaa ambae tupo nae akasikika anapiga kelele weziiii weziiii

Ikabidi fasta tusogee kufika pale mzee analalamika et walikuepo hapa hapa.kumbe mzee alibamizwa ukutani akazimia.

Tulishindwa kujizuia tukaanza kucheka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimegundua pombe ndio kisababishi kikubwa cha watu kukutana na majambazi hasa nyakati za usiku. Miaka kadhaa iliyopita majambazi walivamia bar ambapo bro wangu alikua akikata kilaji. Wakaamrisha watu wote walale chini. Bro alikua anatembea na mguu wa kuku nafikiri aligoma akataka kupambana nao. Masikini walimchapa shaba kisha wakasepa wala hawakuiba tena. Alikimbizwa hospitali lakini siku iliyofuata aliaga dunia.
 
Maskini bora angekubali kulala chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo jamaa anaroho ngumu aise michezo hio asirudie atakuja kupewa adhabu ya kutoa beria wale jamaa ni nyoko ujue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hio mimi nilishuudia arusha jamaa alikua mbishi hivyo hivyo aise walimpa ya kichwa moja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa miaka ya tisini mwishoni maeneo ya mbezi beach,vibaka walisumbua sana kuanzia saa mbili usiku...wanaanza kurusha mawe kwenye paa za nyumba kwa fujo...na ikifika saa 6 wanavamia tunawakurupusha wanakimbia...jirani yangu alikuwa analindwa na mjeda lakini bado hawakuogopa walivizia yuko eneo lingine ndani ya fence wanaruka ukuta upande mwingine wanaingia wanadokoa..siku ya siku mjeda akagundua mchezo wao....akawalia timing hawakujua kajificha wapi...akatangulia mmoja akadumbukia ndani....kosaa...mjeda kaikoki SMG kamwambia tulia hapo hapo....kibaka kaanza kusema kausha basi mshikaji...mjeda kampa moja ya mkono,kibaka chini lakini bado akawaeza kukurupuka akapanda fensi kurukia nje... akala risasi nyingine ya mkono... akakimbilia kwenye uchochoro mjeda nyuma akampiga ya mguu kibaka akaaanguka...wakati hayo yanatokea sisi tupo tunasikilizia tumezima taa zote...baada ya mda mjeda akaja akanigongea akasema tayari....tukatoka nje mpaka kibaka alipolala...hajafa ila mikono yote miwili na mguu vimevunjika...na anaongea...sikio moja hana (tulimuuliza akasema alikatwa siku za nyuma kwenye tukio)...unatokea wapi ...Mwananyamala...mjeda(mwenyeji toka mkoa wa mara) alihakikisha anataja wenzake wote baada ya kumtonesha madonda yake kwaxkumchokonoa kwa mtutu!baadae walikuja polisi wakamchukua,kwa jinsi alivyokuwa na roho ngumu,huyo kibaka alikaa muhimbili miez 3 licha ya kuwa kipindi hicho kulikuwa na mgomo wa madaktari kutowatibia vibaka baada ya daktari mwenzao mmoja kuuawa na majambazi.....lakini baada ya tukio hilo hakuna kibaka yeyote alikanyaga maeneo hayo kwa miaka kadhaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nacheka kama mazuri,,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daahh kama masihara ila umenichekesha sana unakimbia unazunguka
 
Hii nimecheka Kwa sauti[emoji12] [emoji12] [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We unajiongelesha mwamba anakusikiliza tu uzingue
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah nimekumbuka mbali sana teh teh teh teh teh,.. Kwa wale wa kazi wa mwanza kama mnakumbuka, kuna kipindi flani majambazi walikua wanavamia mida ya Jioni Jioni, tena walikua wanafunga center nzima wanaingia duka Kwa duka,

Siku Hiyo niko maeneo ya nyambiti Hapo napata uji Kwa Maza mmoja maarufu sana Hapo, ilipigwa chuma juu Daah Sikumbuki vizuri, hila nilijikuta home Na kikombe cha uji,..

Hila wanadai wale majambazi walikua wanalipa kisasi, maana walikua wanaingia dukani hawachukui Chochote hila wanachanganya mafuta ya kula na ya taa,...unga wa mihogo wanachanganya Na sembe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…