Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Dah, pole sana mkuu,, vp kuhusu huyo njagu aliyekuwa jambazi pia,, hukutoa taarifa yyte?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba unipe huo ujuzi wa kuomba dua

Nifate masharti gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
siri kubwa ya dua yoyote kubwa hasa ya kudhulumiwa au kufanyiwa ubaya basi wakati unaifanya ufanye na watoto hasa watoto yatima wale wadogo kabisa then mwisho uwape sadaka na kwa kusudi kabisa kabla ya kuanza kusoma nao hyo dua waambie kilichotokea mpka wasikitike haswa then piga nao dua hali ya kuwa wanakuonea huruma na huzuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole jamaa
 
Aisee hawa watu sio binaadamu wa kawaida
Mtu kuchinja tu kuku unatetemeka na kusikia huruma sembuse kumpiga mtu panga? Tena unataka kumuua? Binaadamu ni kiumbe katili sana
Wale sio watu wa kawaida amini nakwambia na Nina imani they are born, not made!. Kuna mdau humu kasema eti majambazi wa siku hizi ni masharo baro!!! Sidhan kama amaekutana nao Hao jamaa anawaona tu kwenye TV.

Fikiria situation hii!! Unakwenda kwenye msiba wa swaiba yako kipenzi labda tuseme amefariki baada ya kuugua, majonzi yanakuwa kwa watoto aliowaacha, mke majirani wanaomzunguka na wanaomtegemea kiujumla, ni full majonzi ila kwa kuwa amepanga mungu unasema poa. Sasa ifikirie situation hiyo kwa kifo ambacho 100% anaamua binadamu mwenzako kitokee!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
We mzee umekutana na visa vingi maishani, nimekumbuka kisa chako cha mambo ya uchawi na lile jini, halafu mbn uligoma kutuambia mlimalizanaje na lile jini??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzebaba hao walokufa kwa dua ndo walikuwa majambazi wenyewe ama??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka ilikua mwaka 2014 or 2015 mwanzoni, maskani tulivamiwa na jamaa kama 9 hivi ilikua inanyesha mvua kubwa sana ya upepo mzee akasikia mlango kama unajibamiza, akahisi milago ilishahaulika kufungwa akawa katoka free kabisa kwa lengo la kwenda kufunga mlango aise kumbe jamaa ndio walikua wanamalizia kuvunja. Ile Mzee anafika mlangoni tochi hizo akawekwa chini ya ulizi...

Kufupisha story Mzee walimvunja mguu kwa kipigo cha fasta fasta Mama alikula nondo moja ya paja, pesa alizokua nazo Mzee akawapatia. Walimchukua mdogo wangu wa kike wakampeleka kwa wazazi wakamwabia awaambie wazazi watoe pesa vinginevyo wanaondoka nae . Mwisho waliondoka na dogo, dogo akasema walivyofika getini mmoja wao akasema huyo mtoto wa shule mwacheni, dogo akarudi ndani.

Maskani tulikua na mbwa 4 cha kushangaza mbwa zote zilikua bandani zimetulia, kipindi icho sikiwa na desturi ya kulock mlango wa chumbani kwangu walifungua wakaniita jina langu kamili wakaniambia nitulie hivyo hivyo, waliniamsha kistaarabu sana nilikua Usingizini zilikua zimepita kama dakika 50 hivi tangu niiingie kitandani hawali nilikua nacheza PS na dogo wangu wa kiume. Kama wangewahi kidogo wakatukuta macho.

Sim zote hawakwenda nazo waliziacha mezani walikua wamekusanya vingamuzi vi3 wamekiweka kwenye mkoba na subufa ila mwisho vyote waliviacha mlangoni hawakwendanavyo.

Cha kushangaza kuna majirani waliona wakati wanaruka ukuta kuingia ndani lakini walikaa kimyaa. Mmoja akampapigia sim mwezake kuwa kwa flani wamevamiwa. Alikua na chance kubwa ya tuoa msaada maana wale jamaa walikaa sana ndani zaidi ya dakika 45+ .

Daah inasikitisha miezi mzee anauguza mguu hicho ndio kitu kilichokua kinaniuma sana.
 
Hiyo sauti uliisikia ya Polisi jirani yenu ukuchukua hatua yoyote baada ya kuponA

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikutaka kabisa kujihusisha hata mama alikuwa nanamfahamu na yeye alimsikia maana mara kwa mara akiwa anaenda kazini....

Alikuwa anapita maeneo ya home wanasalimiana na mama shemeji haujambo!! Kumbe alikuwa na lake jambo .....

Polisi waliniuliza sana ila nilificha maana nilijua wengine wanaonihoji wanaweza kuwa sehemu ya mtandao wakanitafuta na kutufyekelea mbali

Kwa hiyo niliiimeza pini!!!

sent from toyota Allex
 
We mzee umekutana na visa vingi maishani, nimekumbuka kisa chako cha mambo ya uchawi na lile jini, halafu mbn uligoma kutuambia mlimalizanaje na lile jini??

Sent using Jamii Forums mobile app
ntawaelezea mkuu,nikiwa free maana ntawaeleza jinsi tulivyoendeshwa mpka tukamalizana nalo tena kwa evidence maana mpka now kuna baadhi nnazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzebaba hao walokufa kwa dua ndo walikuwa majambazi wenyewe ama??

Sent using Jamii Forums mobile app
yani aliyekuwa jamabazi,aliyetoa ramani,inshort yoyote aliyeshiriki mpka aliyenunua vitu vyetu na akawa anajua ni vyetu na yeye alikwenda na maji inshort kulikuwa na misiba ya kutosha mtaani na ote walokuwa wanakufa wakawa wanatunyooshea vidole kuwa ni sisi ndo tulofanya hiyo dua,ombwa sana msamaha lakini ndo hvyo tena dua ishasomwa nakumbuka ilifikia kipindi mpka nikawa narudi home saa 7 na kuondoka saa 11 ili tu nsionane na watu wa mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili yangu yote hili wazo nilikuwa nalo peke yangu.
Majambazi wana kanuni za kutumia silaha hawatumii hovyohovyo na kitendo cha kurusha hewani risasi nyingi kwa eneo kama la Mecco ni alert kwa askari walioko doria.
.
Jambazi hazungumzi maneno mengi vinginevyo ni vibaka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…