Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tatepa
 
Miaka miwili iliyopita tulivamiwa na wezi nyumbani usiku wa saa saba, sina uhakika waliingiaje maana ilikua nyumba ina fence na geti milango yetr ina grill za nondo ngumu, vioo vya madirisha tuliacha wazi ili kupata hewa

Nadhani walikua wanatuchora muda maana waliingia wakati Mr hayupo amesafiri so nilikua all alone na watoto and i was 9 months pregnant

Nikiwa usingizini nikahisi kama nazibwa mdomo nakosa pumzi, nikahisi labda nipo ndotoni lakini nilipofungua macho nakutana na sime tatu, mbili zimeelekezwa kwa boys wangu wawili na moja imenielekea, huyu alieniwekea sime akaniambia tulia kimya ukipiga kelele tunachinja watoto(mr akisafiri huwa nalala na watoto hawa wadogo mmoja alikua na miaka minne na mwingine 6)

Huyu wa miaka sita yeye akaanza kupambana nao akawa anawarushia mara mateke mara vingumi vyake anawaambia muache mama yangu maana alikua amenishika shingo kama anataka kunikaba

Nikiangalia hali yangu na tumbo la miezi tisa, nina watoto watatu ndani tena wa kike yupo chumba kingine, I was terribly worried nikajisemea nainachohitaji ni usalama wa watoto wangu kwanza

Ikabidi nimwambie mtoto atulie, wakati namtuliza mtoto mwizi mmoja akaniamrisha ninyanyuke nifungue safe maana ilikua imefungwa kwa password, walikua wamevaa mask na waliwasha taa zote za nyumba nzima, ndani walikua watatu, sijui nje walikua wangapi

Nikawa mpole nikamfungulia, palikua na document tu hapakua na hela,

Kwa hesabu za harakaharaka ni kwamba ndani waliingia muda mrefu sana na walikua wameshahamisha baadhi ya vitu sema sijui walituwekea dawa hatukusikia, maana pale chumbani palikua pamepekuliwa kila kitu kilikua hovyo mpaka simu yangu walikua wameishika mkononi na baadhi ya vitu walikua wameshachukua,

Yule kiongozi wao akanimuru nimvulie pete zangu za ndoa,nikafanya hivyo, akahitaji passowrd za mpesa na airtel money, nikampatia na akahamisha pesa hapohapo, nilikua na app ya sim banking wakahitaji passowrd pia,nikawapatia na wakahamisha pesa, walipoona nipo calm na ninawapa ushirikiano wakaweka silaha chini wakavua na mask wakawa very confortable kusearch, walisearch kila mahali, vyumba vyote na walichukua kila walichotaka, walikua na Noa imepaki nje

kifupi walispend zaidi ya dakika 30 pale ndani, mmoja akabaki wakati wengine wanapeleka vitu kwenye noah nje na walikua wanatokea geti kubwa bila woga

Walipomaliza, wakaniambia ole wako upige kelele, bado tuna kazi kwa majirani zako,ukipiga kelele tutarudi na tutakubaka mpaka huyo mtoto tumboni atoke, Nilikaa kimya nikachungulia dirishani mpaka nilipohakikisha wametoka, nikatoka nikafunga milango na geti maana waliiacha wazi, then after tukaka na watoto sebleni, walikua wanaogopa,nilikua naogopa pia nikashindwa kujizuia nikawa nalia tu, i had nothing to tell the kids, sikua na neno la kuwatia moyo au kuwafariji, i was helpless,sikua na simu wamechukua zote,tv hamna, laptop hamna, hata tablets za watoto,sikua na kitu chochote cha kuniwezesha kufanya mawasiliano, na mtaa tuliokua tunaishi ulikua kimya nyumba zipo mbalimbali na hata ukipiga kelele sio rahisi kwa jirani wasikie. For the first time i cried like a baby mbele za watoto, ikabidi wao wageuke wafariji wangu, huyu wa kiume aliekua anapigana na wezi akawa ananiambia mama usilie, kesho baba akija atawakamata wote na tutawapiga mpaka warudishe tablets zetu tucheze game

Watoto walisinzia kwenye miguu yangu ila mimi sikulala mpaka mida ya saa 11 nikasikia mngurumo wa bajaji ya jirani inapita(huwa anarudi saa 11 kila siku. Nikatoka nje ya geti mbiio nikamsimamisha, nikamwambia tumevamiwa usiku, ndio ikabidi aanze kuwapigia majirani wengine,na mimi nikaomba simu nikatoa taarifa kwa Mr, ndugu jamaa na marafiki, cha kushangaza kumbe wale wezi walifunga mtaa, walivamia nyumba sita kwa usiku huo,ten nyumba zingine wamingia zilikua na fence ya umeme

Nashukuru Polisi walifanya kazi yao kikamilifu, walikamatwa woote,tulikwenda kuwatambua na sikukosa mahakamani hata siku moja mpaka siku ya hukumu, watoto wangu walikua sehemu ya ushahidi, nakumbuka siku watoto wanatoa watu walipata hisia kali sana na uchungu, yule mwendesha mashtaka alishidwa kujizuia alipata hisia za uchungu na hasira sema miiko ya kazi ilimbana akakaa kimya

Mwisho wa siku hukumu ilitoka na Walipigwa mvua thelathini kwa kwesi ya Arm robery

Tuliuza ile nyumba na hatujawahi kurudi ule mtaa tena,baadhi ya vitu vilipatikana tukaambiwa tukavitambue pale oysterbay ila hatukwenda maana tuliona vitayupatia kumbukumbu mbaya, wakala aliehamishiwa pes akutoka kwenye simu yangu alikamatwa na alishtakiwa pia

Go down walilokua wanahifadhi vitu lilivamiwa na polisi na mmiliki alikamatwa

Hii kumbukumbu haijafutika mpaka leo, na kwa watoto ilikuwa worse,ilibidi tuwatafutie mwana saikolojia wa kuwasaidia, maana ilifika wakati hata mtu akigonga geti wanakimbia kujificha wanahisi ni mwizi
 
Hizo Medani za kivita ni balaa, weusi wako ulikuokoa baada ya kuvua nguo🤣😅
 
oh God 😭😭 poleni sana aisee
 
Duh poleni sana
 
Inasikitisha sana, poleni sana
 
Dah pole sana aisee najua maumivu ya kuona watu wananyima amani na kuwatia hofu watoto wako
 
Poleni nyote mliokabwa na wezi na majambazi, mimi matukio yangu siyo mazito sana.

Tukio la kwanza hili lilitokea nikiwa shule ya msingi sikumbuki ni darasa la ngapi ila ni kwenye darasa la 4 kuendelea hivi, sasa kuna siku nipo kwa jirani, tulikuwa sebuleni nipo mimi huyo mama na watoto wake watatu, mumewe alikuwa nje kwenye banda la kuku, huyu binti yao alikuwa anachukua sahani kabatini kwaajili ya kupakua chakula mara ghafla akaingia kijana yupo kifua wazi kashika mti wa mrunda maana kuna ghorofa lilikuwa linajengwa hapo jirani, akaanza kumpiga nao yule mama ya kichwani anamwambia " toa simu, toa simu" sasa yule mama licha ya kupigwa vile alikuwa anaita mwizi, mwizi. Mimi kwa akili yangu ya utoto nikajua akitoka kumpiga yule mama ataanza kutupiga na sisi saa ngapi nisikimbilie chumbani kwao kujificha😁😁 nimefika chumbani sielewi elewi nikatoka nakuta yule mwizi kashaondoka, kumbe zile kelele mumewe alizisikia baada ya mwizi kutoka hapo nje akapigwa teke akadondoka na simu ikamponyoka akakimbia, yule baba akamkimbiza hadi alivyotokomea ndiyo kurudi,, huku anakuta majirani wamekusanyika nje pale ndiyo kuanza kuwahadithia pale, yule mama akabatizwaga jina la utani "magongo" dah watu wabaya sana 😁😁

Tukio la pili, nikiwa secondary kuna siku natoka zangu kuzurula kwa rafiki yangu ni mbali na home sasa ile njia niliyopita watu wanaotoka kuangalia mpira uwanjani huwa wanaitumia na hiyo siku kulikuwa na mpira mimi nilijisahau, njiani nikakutana na vijana kadhaa mmoja akanifata akaniambia "mimi naitwa micky wewe unaitwa nani" nikamtajia jina la uongo mkononi nilikuwa nimevaa saa na kacha akaniomba namba ya simu nikamwambia sina simu akanishika ule mkono wenye saa na kacha akazivua alafu akaniambia nikaushe kabla hajanipasua, aisee lilikuwa tukio la dk 2 lakini nilichanganyikiwa baada ya hapo nilikimbia vibaya sana kuelekea nyumbani.
 
Mmm!
 
Mstari gani unaotofautisha jambazi na kibaka. Afanyacho kibaka ni sehemu ya ujambazi, maana kibaka anaweza kukwapua, kupora, kupiga, kuuwa, n.k

MTU akikwapua Sh. 1,000 hutasita kumuita jambazi, akikwapua Sh. 100,000,000 ni rahisi kumwita ni jambazi.
Ni kwel ,Kama wakulima mkulima wa jembe la mkono na mkulima wa kutumia trecta wote ni wakulima, wanatofautiana uwezo tu wa kutumia vifaa .kibaka hana uwezo wa kupata bunguki atatumia nondo
 
Pole sana
 
🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…