Tukutane hapa wapenda ujasiriamali

Tukutane hapa wapenda ujasiriamali

Mitaa ya kkoo inanichanganya majina ila mtaa wa mapazia ni aggrey na swahili utaona tu nje mtaa huo umejaa mapazia ingia ndani waambie nionesheni sampo za vitambaa vya mapazia unachagua unanunua (zunguka maduka hata matatu angalau) nunua urembo mwenyewe fundi kazi yake kutoboa kuweka urembo na kuyapinda basi (2,000 tu) kwa pazia moja


Wengi wanashona nzito mita 1 na nusu (2)nyepesi mita mbili, wengine mita 2 kwa madirisha makubwa

Ila madirisha ya futi 6, yani pazia la 3/4x6 unakata hata 1 na robo mara 3
Shukrani boss
 
Mito, kuna vitambaa vya mapazia vya maneno such as gucci, i love you unakata unashona au plain

Vya maneno mengi vinapatikana kwa habby kkoo ukifika sokoni tahfif mtaa unaofatia ulizia kwa habby au wanapouza foronya hapo hapo mwambie nataka kitambaa unachagua unachotaka, ukitaka kushona hapo hapo au kwingine

Foronya kushona ni 1,000 zipu kuna za 2,00 kwa 5,00

Nb: wanakuangalia wakikuona wakuja UNAPIGWA!
Shukrani boss na mashuka hapo kwa habby yapo
 
Hizo kitambaa za pazia na mashuka unaweza pata zenye maandishi?
 
[emoji120].kwaiyo unawaambia wakuuzie kwa bei ya jumla au

Hata ununue mita moja au mita 50 bei ni hiyo

8,000/9,000/10,000/11,000 (wengi bei zao ni hizo)
 
Nakubari sana boss vijana tunaitaji tafiti nyingi na connection kabla ya kuanza biashara

Wengi wanaogopa kujaribu wakati kila vitu vinachangamoto walioko maoffisini kuna changamoto balaa, kwenye biashara pia Yani kila kona, cha muhimu ni kujituma na kupenda unachokifanya mbona unatoboa tu

Na ukijua unataka nini!!!

Mbona hela ya bata unaipata, mtaji bado utakuwa nao wa kutosha na vitu vingine vya maendeleo

Na watu wengi wakikuona unavitu vizuri Uko smart basi wanaamini bidhaa yako ni nzuri zaidi[emoji1][emoji1]Ndio hapo unauziwa kitu cha kkoo unaambiwa kimetoka uturuki,uk,USA, Au dubai Kumbe Bongo hii hii[emoji1]

Nunua simu yako nzuri (Apple hivi Samsung) vaa vizuri hata kama sharobaro basi sio mihereni midread basi nguo imechanika kama chizi[emoji28] kipensi sijui taiti imekubanaa nywele chafu miguu hovyo hovyo jamani kujipenda muhimu Kunaongeza Pia wateja

vaa tu kawaida ila smart hata mtu kabla hajaona unauza nini anavutiwa na wewe kwa muonekano wako tu (sio kimapenzi[emoji9])
 
Mkuu huyu chidi bidhaa original anapatikana mitaa gani pisi kali
 
Hii idea yako imeshaanza kusambaa kwenye magroup ya forex, jamaa kacopy kama ilivyo na namba za simu kaweka kabisa au ndio wewe mwenyewe?

Sipo kwenye forex wala sijawahi kujishirikisha na vitu vya forex sijui vitu gani vitu gani
 
Pisi kali wapi napata nguo za ndani za wadada kwa bei rafiki. Unaoendekeza mtaji gani wa kuanzia

Mwendokasi kituo cha pili upande wa kulia kama unatokea muhimbili ingia maduka ya ndani ndani kuna chupi dozen hadi 3,000 taiti nzuri 12,000 (upande wa china plaza, unapita kanisa)

Kwa kuanza 30,000 au 50,000 sio mbaya changanya chupi na taiti kama na za watoto basi ukiwa na 100,000 sio mbaya unapata mzigo wa kutosha tu
 
Back
Top Bottom