Tukutane tunaomiliki magofu kwa ajili ya kufarijiana

Mngetupia walao tupicha picha ingekuwa bye
 
Niliiona juzi mitaa ya goba, kishapitisha umeme na kapiga plasta ila haijaezekwa....nikabaki nashangaa
Ela yako tu mkuu. Mimi tanesco waliniwekea nguzo na kuweka kabisa nyaya wakati hata wiring sijafunga. Fundi alifanya kufunga wiringa na kuunga tu
 
Anza na kununua material mkuu, kidogo kidogo mkuu
Utakuja kunishukuru
Hii ilikuwa formula yangu... nilikuwa nanunua material nayaacha dukani yakitimia ya stage fulani namshtua fundi anakuja analiendeleza.
Niko mbioni kuhamia mwezi huu japo finishing haijakamilika naenda kuhamia hivyo hivyo maana maji, umeme, skimming, gypsum grills, milango tayri, nataka nimalizie master bedroom kwa tiles na aluminum nihamie kwanza maana ni mimi pekee sina familia huku nikimalizia finishing taratibu.
Ila katika ujenzi nimegundua kama ela kama yangu ya kusanya sanya, ni kama unakwua unaukia pesa tu na vitu haviishi.
Mpaka sasa najiuliza watu wanaochukua mkopo sijui 20 mls wakajenge, naona kama ni kosa kubwa. Maana mtu unakuta mshahara milioni 1 anachukua mkopo 20 mls, anajenga nyumba haishi, kuhamia haamii na bado anakatwa, na kodi iko pale pale.
 
Kungekuwa hakuna wizi wa vifaa vya ujenzi kama mchanga, mawe, matofali etc Bunge kupa mbinu ya kusogeza ujenzi.
Hardware zipo na wanatunza risiti ukilipia sema hela haikai pia nilipofikia panataka hela cash approximation ni kama 3m- 4m
 
Nimechoka na kulimia
 

Attachments

  • IMG_20241130_085316_129.jpg
    753 KB · Views: 10
Ni hatari hii stage nimekwama kwenye tope nashukuru kwa hamasa mkuu
Mimi niliipiga kunzia mwaka jana mwezi wa tatu, nikakwamba baada ya kumalizia kozi zile tatu za juu baada ya lenta. ilikuwa mwez wa tisa mwaka jana. nikapumzika nikaja kuezeka mwaka huu mwezi wa nne. uzuri mashimo yachoo niliyajenga nilipomaliza kujenga msingi ili nipae kifusi cha kujazia msingi.
now imebaki kupiga rangi, tiles na aluminum. gypsum, skimming, mifumo ya maji, milango yoteya chuma na mbao, na frills za madirisha tayari.
Sema kujenga boma rahisi... kuanzia kwenye kuezeka ndipo unaanza sasa kuona uhalisia wa ujenzi.
 
Ukiona nyumba imeisha kila kitu na mwamba kaweka mpaka pavements na fence,mpe shkamoo...
 
Ezeka chumba na sebule hamia.
 
kwenye kila hatua ya maendeleo unayopiga, tambua kuna vita ya nyama na kiroho itakuandama.

Jifunze kuweka GUARD kila mara na unatakiwa utambue ADUI yako ni nani ili upambane nae MAPEMA..

Mimi nilinunua kiwanja mwaka 2021 mwezi wa tano nakumbuka siku simba anacheza na mashujaa, simba akala chuma moja.

Nilikua na milioni 2 nawaza kuweka chumba kimoja cha SLOPE (msingi upo), lakini hadi leo kiwanja kimebaki Jina tu..

Vita niliyokutana nayo baada ya hapo kuanzia kwa ndugu zangu tu baada ya kujua nimenunua kiwanja ilikua balaa sana maana sikuwashirikisha chochote...

Ikawa ndio mwanzo wa ile mil 2 kumeguka na kuisha..

Ila naamini all is well one day Yes
 
Hongera sana mkuu hakika umejinyima vya kutosha mimi renta bado ndo napambana niondoke kwenye hii stage ya renta na bati
 
Hivi pagala linaweza kukaa miaka mingapi mpaka liwe gofu la kubomoa na kuanza upya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…