Tulia Ackson aache upotoshaji, Kiti cha Naibu Spika kiko wazi kikatiba

Yan wampige chini ili akacheze ngoma zake za kimila huko Songwe
 
Unataka apoteze mwana na taulo?
Ndugu yeriko Tafsiri ya vifungu vya katiba unavitoa kichwani mwako au kuna ndugu kakuambia...naomba unijibu maswali yangu kama ifuatavyo,
1.Rais anapofariki bila kigugumizi makamu wa raisi ndio anachukua nafasi yake.kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tz.swali ni Je
Makamu wa rais anatakiwa ajiuzulu kwanza ndio awe Rais?Au awe,Rais wakati huohuo ni Makamu wa Rais?
2.Kifungu kipi cha katiba kimekataza kuwa Naibu spika na Spika kwa wakati mmoja.?na ni kifungu kipi cha katiba Kimemruhusu makamu wa Rais kuwa rais na makamu kwa wakati mmoja.?
"Punguza vijiti kama hujui ..hujui tu"
 
P nakuheshimu lakini kwa kuunga kwako hoja ya Yerriko nimesikitika mnoo.
Naomba kifungu chochote cha sheria kilichotungwa na bunge kinachomzuia naibu wa spika kuwa spika?
Kama hakuna huo wivu wa nini?
Pili...Kama imewezekana kwa makamu wa rais kuwa Rais na makamu kwa wakati mmoja...vipi inashindikana kwa Spika?
Acheni ukanjanja na wivu usio na Manufaa,,,,
Kimaumbile hakuna M/adam asiyependa kupanda nafasi za cheo au kuongeza utajiri ndio hulka zetu na ndio maumbile yetu...."Ujinga ni Ujinga tu hata kama ukisemwa na mtu kwa mtazamo wa wengi anaonekana kama mwerevu"
 
Hata wakati wa kumpandikiza Unaibu Spika ilikuwa hivihivi.
Ndugai, katika unafiki wake, alimlinda ili asijibu maswali yaliyohusu 'uanachama wake na ushiriki wake katika siasa' akiwa bado Mtumishi wa Serikali; Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Tuliona pia matendo yake ya kujikomba kwa serikali, akiwa Naibu Spika kulifanya kwa makusudi Bunge kuwa dhaifu/duni katika kuisimamia serikali. Ninachokiona ni kuwa ushetani wa Tulia wazidi kuwekwa hadharani ili kutuepusha kama TAIFA kuzama zaidi huko ambako kwa uroho wake, anajitahidi kutupeleka.
Mkono wa Mungu unaendelea kutenda kazi. AMEN
 
Unajua bado sijapata jibu...

Hivi posts za namna hii zinaandikwa huku mtu akiwa anaamini kabisa anachoongea ni sahihi or it's just politics?! Nauliza hili swali kwa sababu nimeona posts zingine sawa na hizi tena zikiandikwa na Wanasheria kabisa hadi mtu unafikia kujiuliza "Like serious"?

Shaka yangu ni kwamba tusije tukawa tunaingilia mambo ya siasa za kivyama!!!

Yericko Nyerere, ni kweli unaamini unachokisema?!
 
Upo sahihi LAKINI HUJAMJIBU KISHERIA bali kishabiki!!

Huu ushabiki ndio nami umenifanya nisite kujibu kwa vile inavyotakiwa ndo maana nimemuuliza Yericko Nyerere kama anakiamini alichaondika or it's just yale mambo yetu!!

Labda pia nimuulize na Pascal Mayalla aliyeunga mkono hoja... DO YOU REALLY BELIEVE Yericko is right?
 
Tulia amechukua form ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya spika, na bado hajateuliwa . . Hivyo u naibu spika utakoma tu iwapo chama chake kitampitisha kuwania kiti cha spika .

Soma vizuri maelezo ya vifungu mlivonukuu. Uchaguzi unafanyika ndani ya bunge na huu ni mchakato wa ndani ya CCM sasa leteni vifungu vya kisheria vya CCM vinavyomkataza tulia asuchukue form ndaninya CCM.
Bora ungekaa kimya kuliko kujibu usiyoyajua. CCM ina katiba na nchi ina katiba na popote pale inapotokea mgongano wa kimaslahi baina ya mifumo, taasisi au vyama katiba ya nchi inatakiwa iwe ndio jibu la mwisho hata kama vyama husika katiba zao hazijasema chochote.

Katiba ndio sheria mama. Hakuna katiba ya chama chochote iliyotoa sifa za mtu kugombea lakini vyama vyote vinatoa wenye kulingana na katiba ya nchi.
 

Ningefanya ushabiki ningekubaliana na mtoa hoja, kwa sababu naamini Tulia hafai kuwa Speaker. Kauli ya Tulia mbele ya Rais siku za karibuni inaonesha yeye anaamini kwamba Bunge halina nguvu ya kumdhibiti Rais. We cannot afford to have a leader of the people’s house who is submissive to the leader of the very branch the house is to oversee!
 
.......Sheria iliyotungwa na bunge....
haya maneno mbona Unayaruka!!??? Tulia yupo sahihi usikitazame hichi kifungu kwa mrengo wa kichama Hakuna Sheria inayomzuia naibu spika kugombea kiti cha uspika
 
''Una akili nimeelewa sana''ubarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…