Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!


Mimi mwenyewe sio muumini wa katiba maana njaa inatoa ufahamu wawakilishi wetu..

Mtazamo wangu kinachotakiwa ni kupasuka kwa CCM tupate upinzani wa kweli…hapo ndio tutakaa sawa..CCM wamejisahau sana…

Tumuajiri kiongozi wa chama cha upinzani imara Kenya aje awape consulation watu wafanye mambo…😄 we are tired of CCM kwa kweli..
 
huyu akipewa u spika, Basi wabunge hawajielewi !!! ameanza kulikana bunge ,mapema hivi, hajui kuwa bunge ndo kilanja mkuu wa serikali!!??.
 
Kwa kweli CCM ina watu washenzi na makatili sana, kuanzia wa chumba cha 7 mpaka ma professor
 
Kasema ukweli.

Bunge la JMT liko chini ya serikali!

Naam, ndio sababu wenye chama wanataka kupiga shortcut kuuruka mchakato wa katiba mpya ili kuiwahi “tume huru” ambayo nayo itakuwa chini ya serikali.
 
"Tunaahidi kuwa bunge litakapotakiwa kuikosoa serikali, basi tutakosoa kwa nidhamu, Rais @SuluhuSamia si tu kwamba ni kiongozi wa serikali,bali ni mkuu wa nchi,hivyo nguvu yake haiwezi kulingana na kiongozi yoyote wa mhimili mwingine"
Huyu ndo mteule tayari
 
Tulia asigombee Ni aibu kujitokeza kugombea hiyo nafasi inaonyesha alikuwa amebanwa na ndugai,kugombea kwake Tena Ni uroho wa madaraka na angewaachia wagombea wapya na akabakia na heshima ya kuwashauri maspika wapya.
 
Tatizo letu kama nchi ni kubwa kuliko katiba. Nimeshaona tunajificha tu kwenye katiba lakini uozo umejichimbia chini sana.
 
Wabunge angalieni wagombea wapya achaneni na huyu tulia na hafai kukalia hicho kiti chagueni mtu kwenye msimamo na asiyeyumbishwa na muhimili wowote.
 
Naona wanaunda genge lingine bungeni,
Huyo Tulia ni mnafiki na opportunist ,anaangalia upepo unapoelekea nae anaufwata ,kwa sasa anajifanya kama Job hakuwa nae kabisa
 
Kama Ndugai alishambuliwa na kutakiwa kujiuzulu kwa kusema nchi itakuja kupigwa mnada, basi Tulia ndio anapaswa kujiuzulu kwa kauli hii:



Pia tuone tofauti iliyopo kati yetu na wenzetu wakenya:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…