Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Haya unayosema huwa yanafanyika katika nchi zenye demokrasia uchwara, mataifa yenye demokrasia imara kama US serikali imewahi kufungwa mara nyingi tu baada ya bunge kuikataa bajeti ya serikali, pia mkuu wa jeshi la Marekani amewahi kutangaza mbele ya vyombo vya habari kiapo chao ni kwa katiba ya nchi na sio mtu binafsi hivyo hawatatekeleza amri yoyote batili isiyofuata utaratibu wa sheria na kuingilia uhuru wa demokrasia.

Mimi mwenyewe sio muumini wa katiba maana njaa inatoa ufahamu wawakilishi wetu..

Mtazamo wangu kinachotakiwa ni kupasuka kwa CCM tupate upinzani wa kweli…hapo ndio tutakaa sawa..CCM wamejisahau sana…

Tumuajiri kiongozi wa chama cha upinzani imara Kenya aje awape consulation watu wafanye mambo…😄 we are tired of CCM kwa kweli..
 
huyu akipewa u spika, Basi wabunge hawajielewi !!! ameanza kulikana bunge ,mapema hivi, hajui kuwa bunge ndo kilanja mkuu wa serikali!!??.
 
Kwa kweli CCM ina watu washenzi na makatili sana, kuanzia wa chumba cha 7 mpaka ma professor
 
Kasema ukweli.

Bunge la JMT liko chini ya serikali!

Naam, ndio sababu wenye chama wanataka kupiga shortcut kuuruka mchakato wa katiba mpya ili kuiwahi “tume huru” ambayo nayo itakuwa chini ya serikali.
 
"Tunaahidi kuwa bunge litakapotakiwa kuikosoa serikali, basi tutakosoa kwa nidhamu, Rais @SuluhuSamia si tu kwamba ni kiongozi wa serikali,bali ni mkuu wa nchi,hivyo nguvu yake haiwezi kulingana na kiongozi yoyote wa mhimili mwingine"
Huyu ndo mteule tayari
 
Tulia asigombee Ni aibu kujitokeza kugombea hiyo nafasi inaonyesha alikuwa amebanwa na ndugai,kugombea kwake Tena Ni uroho wa madaraka na angewaachia wagombea wapya na akabakia na heshima ya kuwashauri maspika wapya.
 
Tatizo letu kama nchi ni kubwa kuliko katiba. Nimeshaona tunajificha tu kwenye katiba lakini uozo umejichimbia chini sana.
 
Wabunge angalieni wagombea wapya achaneni na huyu tulia na hafai kukalia hicho kiti chagueni mtu kwenye msimamo na asiyeyumbishwa na muhimili wowote.
 
Kumbukeni Huyu mama ni mwanasheria kabisa, pale Leo anapokuja na kusema kuwa Rais wa Tanzania ndo Muhimili mkubwa wa mihimili yote iliyoopo, hiyo ipo kwenye ibara gani ya katiba yetu au ni kujipendekeza kumezidi? Hebu wanasheria twambieni kama kuna Kifungu kama hicho kwenye katiba yetu
Naona wanaunda genge lingine bungeni,
Huyo Tulia ni mnafiki na opportunist ,anaangalia upepo unapoelekea nae anaufwata ,kwa sasa anajifanya kama Job hakuwa nae kabisa
 
Kama Ndugai alishambuliwa na kutakiwa kujiuzulu kwa kusema nchi itakuja kupigwa mnada, basi Tulia ndio anapaswa kujiuzulu kwa kauli hii:

Screenshot_20220110-220602_Twitter.jpg


Pia tuone tofauti iliyopo kati yetu na wenzetu wakenya:

Screenshot_20220110-220150_Twitter.jpg
 
Back
Top Bottom