Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Tulia Ackson atoa msimamo wa Bunge, asema Rais ni Mkuu wa Nchi na ana mambo yote!

Ndio aina ya asilimia kubwa ya wasomi tulionao. Pathetic !!
 
"Tunaahidi kuwa bunge litakapotakiwa kuikosoa serikali, basi tutakosoa kwa nidhamu, Rais @SuluhuSamia si tu kwamba ni kiongozi wa serikali,bali ni mkuu wa nchi,hivyo nguvu yake haiwezi kulingana na kiongozi yoyote wa mhimili mwingine"
 
Hii imekaaje

67C6575C-F836-49E8-B0CC-004E8F96D545.jpeg
 
"Tunaahidi kuwa bunge litakapotakiwa kuikosoa serikali, basi tutakosoa kwa nidhamu, Rais @SuluhuSamia si tu kwamba ni kiongozi wa serikali,bali ni mkuu wa nchi,hivyo nguvu yake haiwezi kulingana na kiongozi yoyote wa mhimili mwingine"
Basically siyo kukosoa. Ni kushauri. Wanakosoa kwani wao ni wakamilifu?
 
Kuuza mhimili wa nchi kwa sababu ya tumbo👇😁😁😁
 
Kumbukeni Huyu mama ni mwanasheria kabisa, pale Leo anapokuja na kusema kuwa Rais wa Tanzania ndo Muhimili mkubwa wa mihimili yote iliyoopo, hiyo ipo kwenye ibara gani ya katiba yetu au ni kujipendekeza kumezidi? Hebu wanasheria twambieni kama kuna Kifungu kama hicho kwenye katiba yetu
Huyu mama ni mwanasheria wa mirathi mkuu ndo alipobobea huko sio kwinginepo maana kuna vitu anavijua ila anajitoa ufahamu
 
Bunge halina maana tena, inashangaza Naibu Spika anapotamka kuwa sio lazima serikali ichukue ushauri wa bunge, sasa nini maana ya uwepo wa bunge kama taasisi inayoisimamia serikali?

Huyu Tulia anadhani hii ni nchi ya kidikteta, kwa hii kauli yake nae anatakiwa kujiuzulu, anaonekana bado ana "mindset" ya kitumwa licha ya kuwa mwanasheria.

Zaidi hafai kuendelea kuwa NS kwa huu mtazamo wake, sasa kama ushauri/ kuhoji wanavyofanya kwa serikali sio lazima kuna haja gani ya kuwa na bunge?

Kwa kifupi hatuna wawakilishi bungeni…ni maumivu tu kwa watanzania…
 
Tungepigania kwanza Katiba hii mbovu ikafuatwa angalau zaidi ya 50%.....maana tunataka katiba mpya wakati iliyopo tayari inakanyagwa..

Hafadhali umeliona hili mkuu…kwa njaa tulizokuwa nazo…itakanyagwa tu…
 
Naibu Spika akiongea katika hafla ya kuwaapisha mawaziri, manaibu na viongozi wengine, amewapongeza wote walioteuliwa na kuwashauri wameteuliwa kufanya kazi za Rais nao wao wanamsaidia hivyo wazifanye kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano na si vinginevyo. Kuhusu Bunge, amesema kuna watu wanahisi kazi ya Bunge kila wakati ni kukosoa pekee. Amesema uko wakati Bunge linaishauri Serikali, kuna wakati linatunga sheria pia uko wakati Bunge linaisimamia Serikali.

Tulia amesema katika kipindi cha awamu ya sita imekuwa ikiwasikiliza ushauri wa wabunge na imekuwa ikizifanyia kazi.

Kwa muktadha huo, Tulia amesema Bunge liko tayari kushirikiana na awamu ya sita kwa mambo yote ambayo itayaleta bungeni ili wasimamie Serikali.

Naibu Spika amesema pale ambapo wanahitaji kukosoa Serikali wataikosoa kwa heshma na kwa muktadha ambao katiba inaruhusu kufanya hivyo, kwenye kushauri watashauri na si lazima Serikali kufata ushauri wa Bunge lakini katiba imetoa nafasi ya Bunge kuisimamia Serikali na kupata fursa ya kuiuliza Serikali walifanyia ushauri gani.

''Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.

Naamini kwa ufafanuzi huu watu watafahamu kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa Serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo yeye uongozi wake hauko sawasawa yeyote wa mhimili wowote ulioko hapa nchini"


Alisema Naibu spika, Tulia Ackson
Yuko sahihi hio tafsiri ni next level, professor Richard Mabala anafahamu, The Animal Farm. All animals are equal but others are more......malizieni.
 
Kuuza mhimili wa nchi kwa sababu ya tumbo
 
Back
Top Bottom