Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin

Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin

Sikapendi yani ningekuwa mbunge ningekapiga mpaka kakome kufanana na ngedere

Hah hah mchezo huu wa siasa hauhitaji hasira, ni ushwawishi na nguvu ya hoja.

Huyo kama CHADEMA ikichukua dola na uongozi wa nchi utashangaa mabadiliko ya Dr. Tulia Ackson, ni chama dola kongwe ndiyo kimemuharibu kwa kumkinga na dunia halisi kiasi akiingia katika dunia nyingine kama hii ya Bunge la IPU ana panick.

Kama 2019 na 2020 kungekuwa hakuna uchafuzi bunge na vikao vya diwani vingekuwa na CHADEMA wengi hata ulaya asingepaniki.

Ile wingi wa CHADEMA katika bunge na vikao vya maamuzi ni shule tosha kwa wanaCCM, tatizo miaka 8 tangu 2016 waliondoa upinzani wakabweteka kuwa unanijua mimi ni chama tawala, mimi mbunge wa CCM, mimi nipo kwenye kamati ya ulinzi ya Mkoa / wilaya, mimi M-NEC mjumbe wa Halmashauri kuu wa chama dola kongwe n.k Bila kutikiswa na upinzani unakuwa ktk dunia isiyo halisia.

Somo zuri kwa viongozi wote wa CCM kuwa pekee yenu katika ngazi za maamuzi, ona sasa mnaaibika kimataifa.
 
Endelea kumpotosha. Atafanywa na ku...rwa.
Hivyo vikao vya kimataifa usipokuwa jasiri huwezi ongea

Miafirika mingi mioga ikifika hata forum za kimataifa hata semina tu mwafrika kama wewe akikutana na wazungu kuongea shida

Na hii imeshasemwa sana hata na wazungu wenyewe kuwa waafrika huwa kinywa sana vikao vyenye wazungu wengi

Nimpongeze tena vizuri sana Tulia kwa kutuwakilisha vizuri boldly na proffesionally keep it up

Dunia pia ingependa kusikia mawazo ya waafrika na misimamo yao bold kwenye issue serious sio tu yes yes mzungu na bendera fuata upepo za ohh kama alivyosema mzungu nakubaliana nalo
 
Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU), Tulia Ackson, amewataka wajumbe kumheshimu wakati wa mkutano wa Bunge uliofanyika Geneva siku ya Jumatatu Oktoba 14, 2024.

Mvutano ulianza baada ya Artur Gerasimov, mwakilishi wa Ukraine, kuomba "ripoti kamili ya mchakato" wa mkutano wake na kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, na aliuliza ikiwa maazimio ya IPU kuhusu "uchokozi wa Urusi" yalijadiliwa.

"Nataka sote tukumbuke kuwa hili lilitokea siku chache tu baada ya makombora ya Urusi kuharibu hospitali maarufu ya watoto huko Kiev," alisema Gerasimov, huku mwakilishi wa Canada pia akiunga mkono wito wa majibu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Gerasimov alijaribu mara kadhaa kumkatiza na kuchukua tena nafasi ya kuzungumza, kabla ya Tulia kumwambia: "Umeshazungumza, ulipata nafasi ya kuzungumza hapa. Nipe, niachie muda kwanza kulihutubia baraza kuu, nijibu masuala yaliyotolewa kisha turudi kwenye ajenda."

Ziara hiyo, aliendelea kusema, ilipaswa kuanza na Ukraine. "Ukraine ilijibu siku tuliyokuwa tayari kuwatembelea, [kwamba] Bw. Zelensky na Spika wangekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa NATO. Ningewazuia? Hapana, isingekuwa busara, na kwa hali yoyote sina mamlaka hayo," Dkt. Tulia aliendelea kusema.

Pia Dkt. Tulia aliongeza kuwa hakuna atakayemzuia kuhudhuria Mkutano wa BRICS wiki ijayo huko Urusi.

Pia, soma:
 
Attachments

  • WAZUNGU WAMCHOKOZA DKT. TULIA, AWAPIGA ZA USO UKUMBI WALINDIMA.mp4
    63.8 MB
Hah hah mchezo huu wa siasa hauhitaji hasira, ni ushwawishi na nguvu ya hoja.

Huyo kama CHADEMA ikichukua dola na uongozi wa nchi utashangaa mabadiliko ya Dr. Tulia Ackson, ni chama dola kongwe ndiyo kimemuharibu kwa kumkinga na dunia halisi kiasi akiingia katika dunia nyingine kama hii ya Bunge la IPU ana panick.

Kama 2019 na 2020 kungekuwa hakuna uchafuzi bunge na vikao vya diwani vingekuwa na CHADEMA wengi hata ulaya asingepaniki.

Ile wingi wa CHADEMA katika bunge na vikao vya maamuzi ni shule tosha kwa wanaCCM, tatizo miaka 8 tangu 2016 waliondoa upinzani wakabweteka kuwa unanijua mimi ni chama tawala, mimi mbunge wa CCM, mimi nipo kwenye kamati ya ulinzi ya Mkoa / wilaya, mimi M-NEC mjumbe wa Halmashauri kuu wa chama dola kongwe n.k Bila kutikiswa na upinzani unakuwa ktk dunia isiyo halisia.

Somo zuri kwa viongozi wote wa CCM kuwa pekee yenu katika ngazi za maamuzi, ona sasa mnaaibika kimataifa.
Safi sana kwa uchambuzi yakinifu
 
aliulizwa maswali alipaswa ajibu maswali na sio kutaka kujitetea kwasababu ametoka Africa, wauliza maswali wanataka majibu, angeishia kujibu technically na sio kuonyesha udhaifu na mipasho waliozoe kuwapa CDM.

Nafasi ni kubwa kuliko yeye.
 
Toka akiwa mwalimu wangu wa Sheria, na hadi sasa, ninaukubali uwezo wake wa kujieleza na kuzungumza Kiingereza kwa umahiri kabisa.

Hongera sana (Mwaisa) Tulia Ackson Mwansasu (LL.B., LL.M., PhD)

Duh kingereza gani hapo tena Mzee, mbona cha kawaida sana ambacho sidhani kama kinalingana hata na ukubwa wa hiyo position.
 
Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU), Tulia Ackson, amewataka wajumbe kumheshimu wakati wa mkutano wa Bunge uliofanyika Geneva siku ya Jumatatu Oktoba 14, 2024.

Mvutano ulianza baada ya Artur Gerasimov, mwakilishi wa Ukraine, kuomba "ripoti kamili ya mchakato" wa mkutano wake na kiongozi wa Urusi, Vladimir Putin, na aliuliza ikiwa maazimio ya IPU kuhusu "uchokozi wa Urusi" yalijadiliwa.

"Nataka sote tukumbuke kuwa hili lilitokea siku chache tu baada ya makombora ya Urusi kuharibu hospitali maarufu ya watoto huko Kiev," alisema Gerasimov, huku mwakilishi wa Canada pia akiunga mkono wito wa majibu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, Gerasimov alijaribu mara kadhaa kumkatiza na kuchukua tena nafasi ya kuzungumza, kabla ya Tulia kumwambia: "Umeshazungumza, ulipata nafasi ya kuzungumza hapa. Nipe, niachie muda kwanza kulihutubia baraza kuu, nijibu masuala yaliyotolewa kisha turudi kwenye ajenda."

Ziara hiyo, aliendelea kusema, ilipaswa kuanza na Ukraine. "Ukraine ilijibu siku tuliyokuwa tayari kuwatembelea, [kwamba] Bw. Zelensky na Spika wangekuwa New York kwa ajili ya mkutano wa NATO. Ningewazuia? Hapana, isingekuwa busara, na kwa hali yoyote sina mamlaka hayo," Dkt. Tulia aliendelea kusema.

Pia Dkt. Tulia aliongeza kuwa hakuna atakayemzuia kuhudhuria Mkutano wa BRICS wiki ijayo huko Urusi.

Pia, soma:
KIBURI, amezoea kuwafokea CHADEMA, hao ni magharibi mkuu.. subiri soon atapigwa pini.
 
watanzania acheni chuki zenu mbona kajieleza vizuri sana huyu dada yuko vizuri sana aisee
Kujieleza vizuri ni kitu kimoja...

Lakini logic ya maelezo yake na tendo alilofanya vinakuwa under scrutiny...

Asifikiri kuwa na huko anaongoza bunge la Dodoma la kina Msukuma au Kibajaji...
 
My Take
Kuwa tempared na Unaongea kizungu hakuleti ukakasi kama kwa Kiswahili.

Tulia ajifunze kuzuia hasira zake vinginevyo atakuja kupayuka kubwa kuliko 🤣🤣🤣🤣
Bila kutumia tone hiyo, hao wajumbe wange mpanda kichwani! Wakati mwingine watachuja maneno ya kutumia wakati wa kuuliza maswali!
 
Hah hah amepanic sana, sijawahi kuona mwanasiasa ktk youtube, online media na TV akiongea kwa jabza kiasi hiki.

Hii clip ita trend sana duniani kote. Alizoea kuziba midomo watu Mbeya, Dodoma, Dar es Salaam n.k yaani nyumbani Tanzania.

Sana anakumbana na ulimwengu halisi. Lazima achokonolewe kwa kuangaliwa mienendo yake, hata jinsi bunge la chama kimoja linavyoendeshwa Dodoma.

Chaguzi za TAMISEMI, uchaguzi mkuu 2025 watamuuliza wabunge wamepatokanaje, mchakato mzima unaonekana siyo huru wala wa haki n.k

Bado balozi namba moja wa Tanzania aliye rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na taasisi yake ijitayarishe kuhojiwa wakienda zile safari nyingi ngambo.

Mtandao huu wa JamiiForums, clip zilizopo YouTube n.k unasomwa kwa google translator, hakuna pa kujificha. Kuhojiwa kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi serikali za mitaa TAMISEMI 2024 kaa la moto, wajirekebeshe ama sivyo ya Dr. Tulia Ackson yataibuka Commonwealth, UN, EU, AU, SADC n.k

View: https://m.youtube.com/watch?v=VQzcl1p-fkE&t=24s

Kaswali kamoja tuu kamemchanganya nusura apigine na meza😂
 
Back
Top Bottom