Tulia Ackson: Wanaoamini nguvu ya dola ilitumika uchaguzi 2020 ni imani tu, hamna mtu ameona mahali. Auliza mbona hawakwenda mahakamani!

Lugha sahihi siyo dola ilitumika bali ni watu waovu wakitumia vyombo vya dola vibaya kwenye uchaguzi.
Siku zote dola lazima iwepo na itumike vizuri.
Ndiyo sababu, ni halali kwa wananchi kutumia nguvu kuwaondoa waovu madarakani.
Dola hiyo hiyo ndiyo hutumika kuwashughulikia hao waovu wanaoharibu uchaguzi n.k.
Changamoto inakuja kama itatokea watu wasio waadilifu, wajinga, wasojiamini kwenye vyombo vya dola, hivyo wote kushirikiana kutenda uovu dhidi ya uma (ushirika wa serikali, majeshi na mahakama).
Tatizo ni watu waadilifu.
 
Hakuna uhusiano wa ghasia na mahakama kutoa hukumu kwa wakati. Kwahiyo hii kesi ya Covid 19 hapa nchini inacheleweshwa kwa kuhofia maamuzi yakitolewa kutatokea ghasia ama?
Kama uharaka huo wa kutoa hukumu umepelekea upande muhimu usiridhike huoni mahusiano ya uharaka na vurugu? Kama kujipa muda wa kutafakari na kukusanya ushahidi pengine ungepelekea hukumu kuwa tofauti jee?
 
Waende mahakama zipi, hizi hizi zinazoendesha kesi ya Covid 19 mwaka wa pili huu? Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi nafasi ya urais imeisha ndani ya muda mfupi, iweje hii ya Covid 19 ichukue zaidi ya mwaka?!
Wengi wanajua sana, ila wanajifanya hawajui! Zitto Kabwe alifungua kesi ya kutaka kujua uhalali wa Rais Magufuli kumtumbua CAG Assad. Kwa kipindi hicho JPM hajafa, ilikuwa kama hiyo kesi haipo. Amekufa, imesikilizwa chap chap, na hukumu kutoka kuwa JPM alikosea!
Nina imani, kama angekuwepo, wala hiyo kesi isingesikilizwa! Hivyo, pamoja na kuwa dhuruma za uchaguzi zilikuwa wazi, waathirika walijua kuwa hata huko mahakamani, hawatapata haki!
 
kama uharaka huo wa kutoa hukumu umepelekea upande muhimu usiridhike huoni mahusiano ya uharaka na vurugu ? kama kujipa muda wa kutafakari na kukusanya ushahidi pengine ungepelekea hukumu kuwa tofauti jee ?

Uharaka umetokana na ushahidi kukamilika, kutokuridhika ni jambo jingine. Hali hiyo imeiweka mahakama ya Kenya mbele sana ya haya majengo ya mahakama za Tanzania yaliyo chini ya Makada wa CCM.
 
Awadanganye Wajinga
 

Ndiyo mkiambiwa Waafrika wakiuza waafrika wenzao msishangae, yaani Tulia anafika kutoa ufedhuli Kama huu? Na wa TZ wametuliaaa, Ni kuwa Wa Tanzania bado wana akili Za kitumwa na wataendelea kutawaliwa na mijitu hii ya CCM siku zote.
 
Huu ushahidi unaupeleka lini mahakamani? Mnajua mlimnenea mangapi Makonda na sasa hamna ushahidi hata mmoja?
Huyo alikuwa mtoto wa baba,na huenda aliacha hisia wa mwanae kutoguswa mbali na madhambi yake yote,mengine hata hayakumfurahisha baba yake 🤔
 
Kesi za Uchaguzi walizoshinda Lissu na Lema ziliamuliwa na Mahakama ya Burundi?Acheni utoto!
Hatutaki huruma kweny vyombo vya kutoa haki.

Kitendo cha majaji na viongozi wa tume yote ya uchaguzi kuteuliwa na mwenyekiti wa ccm kimtazamo wa kawaida hapo hakuna uchaguzi wa haki na halali.

Mtu mwenye akili timamu hawezi akajadili jambo hili vichaa tu wa ccm na wavyamapindani ndiyo watajadili huu ujinga.
 
Ndiyo mkiambiwa Waafrika wakiuza waafrika wenzao msishangae, yaani tulia anafika kutoa ufedhuli Kama huu? Na wa TZ wametuliaaa, Ni kuwa Wa TZ bado wana akili Za kitumwa , na wataendelea kutawaliwa na mijitu hii ya CCM siku zote
Wajinga ni wengi sana na huu ujinga unarithishwa vizazi na vizazi
 
Hili la Dr. Tulia kutoa rushwa nalilitilia shaka kwavile yeye ni mtu wa Mungu sasa kama alisha-backslide hiyo itakuwa habari mpya kwangu.
Ahsante
 
Mahakama gani kwa ule ushetani uliokuwa unaendelea?
Mahakama zote sio majaji au mahakimu walikuwa hawana maamuzi zaidi ya kupangiwa!
Kama unabisha 2025 kutana na Sugu jimbo likiwa halijagawanywa ndio utalijua Jiji!
 
Kwanini hawakuenda mahakamani baada ya Magufuli kufariki
Kuna law of limitation Act ambayo inatoa cut off ya muda wa kufungua shauri la Judicial review Mahakamani. Nahisi mwisho ni miezi 6 kuanzia tarehe ya maamuzi yanayobishaniwa.
 
siipend ccm ila sipendi udaku , una ushaid wa mahusiano kati ya jpm na Tulia? tukosoe vitu bila mihemko ni kwel mbeya waliiba kura ila tusifike hatua ya kuongeza chumv nying kweny taarifa
Unataka nikuonyeshe picha? Kweli kuona huoni hata sauti husikii?
 
Hili la Dr. Tulia kutoa rushwa nalilitilia shaka kwavile yeye ni mtu wa Mungu sasa kama alisha-backslide hiyo itakuwa habari mpya kwangu.
Ahsante
Tulia siyo mtu wa Mungu bali ni wa Shetani. Ukiona mtu alikuwa anakubalika na Magufuli ujuwe huyo hana Mungu. Mimi nilikuwa msimamizi wa uchaguzi kwenye moja ya Kata zilizopo barabara ya kwenda Chunya. Nimeshuhudia mwenyewe Bajaj na vijana wa Tulia wakigawa bahasha kwa wajumbe usiku wa kuamkia tarehe ya kupiga kura za maoni kwa wajumbe wa Jimbo.

Mbona hii siyo siri, njoo Mbeya muulize Mwenyekiti au Katibu wa Kata yoyote, atakuambia alivuna ngapi siku hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…