babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,478
- 18,341
Hamna lolote,kwa ufikiri wangu haraka tu ni kwamba hamna custom staff pale bandarini mda huo.Ungeuliza sababu ni nini? Ya kuendelea kukaa kwenye boat wakati mmeishafika!!
Jibu Lao lingetupa fursa nzuri ya kujadili na kushauri lengo likiwa KUBORESHA.
Hujawahi kufika Russia, acha porojo zako.Wewe unaongea nini?
Kasema mwenyewe alichelewa akalazwa majini kwamba wateremke muda custom wako hai.
Kawaida tu hiyo.
Si tulikaa Russia masaa manne ndio kutoka na hatukufika mbali tukaanza kughasiwa.
Tukarudi ndani kutulia.
Kulikua na kila kitu mle so
watoto hawakuboreka
chochote.
Nimekujibu kistaarabu kwasababu hujaongea matusi.
Kaa kwa Amani
Usimjibu mtu mwenye stress na wewe unaweza kuingiza kwenye stress zakeTatizo ni nini mpaka kuwasubirisha watu masaa matatu? Giza au kukosa wafanyakazi, unaonekana akili zako ndio za hao hao anaowaongelea.
Hapo ndo nakupendaga mamaa Faith,kwenye issue za maana unachambua vizuri tu nakupa 👍kwenye hili.Ni mambo ya kiusalama na utendaji zaidi. Wewe umefikiria upande wako wa abiria lakini hujafikiria upande wa wafanyakazi wakaokuja kukuhudumia. Wengine hiyo saa 9 usiku ndiyo wanatoka makwao ili waje kukuhudumia wewe saa 12 asubuhi.
Kifupi ni mipangilio ya kikazi tu.
Tatizo letu kubwa Tanzania ni ujinga tu, kwanini meli iondoke huko ilitoka saa ambazo wanafahamu itafika Dar saa 9 usiku na abiria watakalishwa ndani ya boti mpaka ifike 12 asubuhi?
Ni ujinga tu wa safari ilipoanzia siyo ilipoishia.
😅😅😅Sasa we ni maskini,huko mi ni sebuleni kwangu bwege wewe MASIKINI.Hujawahi kufika Russia, acha porojo zako.
Hii Chai asubuhi hii.CRDB waliwahi kufunga mlango tukabaki mimi na wahudumu tu na muda ulikuwa umeshaisha. Walicheza na tatizo langu hadi likaisha. Akaunti ilikuwa inakubali kutoa pesa tawi moja tu tena kuna mhudumu ndio alikuwa anaipatia.
JF kuna vituko Sana, miezi 18 niko darasani DMI plus sea time, leo wewe ndio wa kunipa tofauti ya MV? Principal wangu Ninalwo akisoma hapa atacheka Sana.Wengi humu hamjui tofauti ya meli na boti, hiyo ni meli ya mizigo na abiria inaitwa azam sealink. Unatumia masaa 6 Dar-Znz.
Na wewe usijepanda meli halafu ukasema hufanyi biashara hiyo.
Umasikini uko kwenye fikra (muflisi)!Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat. Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi. Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu. Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee. Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
Je, inawezekana muda huo wa usiku hakuna boti na meli nyingi za abiria zinashusha, hivyo wanaona ni hasara wafanyakazi kukesha wakati abiria wanaowasili ni wachache?Kabisa bandari ikeshe..soko la kariakoo likeshe..etc
Uchumi uliochangamka, usafiri ni masaa 24.We mwenyewe maskini,
umechelewa, ukapanda boti la usiku.
Umeshindwa nini kulala Hotel uondoke kesho?
Ndege hazipo kwanza?
We ni Maskini kuliko hata hao unaita Maskini
Sijui mkuu, wanasema ndio utaratibu. Niliongea na baadhi ya abiria wakasrma walishangaa kuona inaondoka Zanzibar saa 9:43. Kawaida unaambiwa Boat inaondoka saa 3 usiku ila ukipanda inakaa mpaka saa 6 au 7 usiku ndio inaondoka ili ifike Dar saa 12 asubuhi. Nilizan ni kwa ajili ya ukaguzi lakini tuliposhuka tulitokea yanapotokea magari na hamna mtu anakagua mtu.Pole sana ndugu, sababu ya kuwasubirisha ni ipi?.
Angepanda boti angefika saa 5 kasoro na angeruhusiwa kutoka. Sasa yeye kapanda la mizigo na akashushiwa bandari ya mizigo!Mkuu,
Tatizo sio spidi, anacholalamika yeye Kwanini wakae bandarini masaa matatu na tayari safari imeisha.
Hilo la kupanda saa3 mpaka saa9 sio hoja.
Hoja ni kwanini wakae masaa matatu na tayari mshafika?
Umeelewa lakini?
Serikali huwa haipati hasaraJe, inawezekana muda huo wa usiku hakuna boti na meli nyingi za abiria zinashusha, hivyo wanaona ni hasara wafanyakazi kukesha wakati abiria wanaowasili ni wachache?
La mizigo linaruhusiwa kubeba abiria??Angepanda boti angefika saa 5 kasoro na angeruhusiwa kutoka. Sasa yeye kapanda la mizigo na akashushiwa bandari ya mizigo!
Ya Tanzania siyo... Nakubali kabisa...Serikali huwa haipati hasara
Ndiyo maana akazuiliwa mpaka kuche!La mizigo linaruhusiwa kubeba abiria??
Wanazungumzia usalama wakati bus likifika huo muda linashusha Nchi hii ina mambo ya ajabu sana na bila jamaa kuandika hivyo tusingejua kuwa bado tupo kwenye giza...Usitetee vitu vya ajabua ajabu,
Kwa nini bandarani hawafanyi kazi masaa 24?
DP World hawajaanza kufanya kazi??
Umasikini taabu sana, unauza muda wako😂😂Wanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkono😀