Tuliishi kwa raha sana....Kabla kampuni kupanuka

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,106
Reaction score
12,916
Naam madereva tuliishi kama ndugu, tulikuwa na umoja na Upendo wa kweli tuliishi kifamilia zaidi...Mkurugenzi/ mmiliki kila weekend kama tumerudi (Kwa sababu kampuni yetu tulikuwa tunapakia pamoja tunasafiri pamoja na kurudi pamoja), alikuwa na utaratibu wa nyama choma yard.

Nyama za kutosha na nyingine tunabeba nyumbani, siku za ijumaa baada ya swala ya mchana wote tunajumuika pamoja majris juu ghorofani tunakula mandi mbuzi au mandi kuku(ni chakula mfano wa pilau).

Ikawa usiku ikawa mchana, Mungu jaalia Kampuni ikakua ikaleta malori 80 kwa pamoja...duuh hapo ndio balaa na mitihani ikaanza kuongezeka kwenye kampuni, kila mtu akirudi safari anakuta kuna kesi ofisini mara hili mara lile.

Maneno yakaanza kuwa mengi kuliko kazi.... Mkurugenzi akawa kama kachanganyikiwa hata ofisini akawa hafiki madaraka akamkabidhi muhindi wa India ambaye umeneja ulimshinda kwenye moja ya Kampuni ya Mkurugenzi Malawi. Utaratibu wa nyama choma ukafa ......kula mandi ikawa historia chuki na magomvi baina ya madereva ikaanza hasa madereva wageni.

Majungu, husda, visa na fitina zikakomaa....ushirikina ukawa unafanyika waziwazi, baadhi ya kiongozi akategeshewa sumu kwenye chakula na kupoteza uhai ndani ya Yard,,,,balaa ikazidi kukomaa,,,,,,uzuri wa Kampuni ukafubaa......

Yoote yakawa Historia......Wenye kuona mbali tukaona ni wakati muafaka wa kuondoka kwa amani,,,,,baada ya kusoma na kuelewa ALAMA ZA NYAKATI........
 
Pole sana penye ridhiki hapokosi fitina.
Rafiki yangu hivi nilikuja kitelewasi toka saa tatu jana usiku na hapa nimemalizia bia ya mwisho ila sina hata nauli ,nawaza nitembee au nipae maana niendako ni mbali .

Starehe mbaya sana kama una rafiki mitaa hii niombee lifti walau anifikishe mbalizi kuhusu kufika nyumbani labda nitapata pia lift
 
Punguza pombe mkuu, kunaraha gani kua a drunken man.

Mimi pia nakunywa Ila na drink responsible.

Weka namba ya simu tukutumie nauli japo najua haito zidi elfu 5.

Pole Sanaa.
 
Naam madereva tuliishi kama ndugu, tulikuwa na umoja na Upendo wa kweli tuliishi kifamilia zaidi...Mkurugenzi/ mmiliki kila weekend kama tumerudi(manake kampuni yetu tulikuwa tunapakia pamoja tunasafiri pamoja na kurudi pamoja),,,,alikuwa na utaratibu wa nyama choma yard..nyama za kutosha na nyingine tunabeba nyumbani,,,,siku za ijumaa baada ya swala ya mchana wote tunajumuika pamoja majris juu ghorofani tunakula mandi mbuzi au mandi kuku(ni chakula mfano wa pilau).
Ikawa usiku ikawa mchana...Mungu jaalia Kampuni ikakua ikaleta malori 80 kwa pamoja...duuh hapo ndio balaa na mitihani ikaanza kuongezeka kwenye kampuni,,,,kila mtu akirudi safari anakuta kuna kesi ofisini mara hili mara lile,,, maneno yakaanza kuwa mengi kuliko kazi.... Mkurugenzi akawa kama kachanganyikiwa hata ofisini akawa hafiki madaraka akamkabidhi muhindi wa India ambaye umeneja ulimshinda kwenye moja ya Kampuni ya Mkurugenzi Malawi.....utaratibu wa nyama choma ukafa ......kula mandi ikawa historia chuki na magomvi baina ya madereva ikaanza hasa madereva wageni,,,,,majungu,husda,visa na fitina zikakomaa....ushirikina ukawa unafanyika waziwazi,,,baadhi ya kiongozi akategeshewa sumu kwenye chakula na kupoteza uhai ndani ya Yard,,,,balaa ikazidi kukomaa,,,,,,uzuri wa Kampuni ukafubaa......
Yoote yakawa Historia......Wenye kuona mbali tukaona ni wakati muafaka wa kuondoka kwa amani,,,,,baada ya kusoma na kuelewa ALAMA ZA NYAKATI........
IMG_20250311_200459.jpg
 
Pole sana penye ridhiki hapokosi fitina.
Rafiki yangu hivi nilikuja kitelewasi toka saa tatu jana usiku na hapa nimemalizia bia ya mwisho ila sina hata nauli ,nawaza nitembee au nipae maana niendako ni mbali .

Starehe mbaya sana kama una rafiki mitaa hii niombee lifti walau anifikishe mbalizi kuhusu kufika nyumbani labda nitapata pia lift
Kaka nakumbuka uli sema una itaka tuzo ya mfanyakazi bora, ila jitahidi upunguze na wenzio ni watu ujue 😁😂.

Yaani saa kumi uko macho?
 
Fanya juu chini usogee mpaka pale Rungemba mtafute Kalinga au Mwangimba watakuombea lift,,,,,,wape salaam waambie Mululu anawasabahi.....Ukiwatajia jina Mululu....msaada utapata.
 
Punguza pombe mkuu, kunaraha gani kua a drunken man.

Mimi pia nakunywa Ila na drink responsible.

Weka namba ya simu tukutumie nauli japo najua haito zidi elfu 5.

Pole Sanaa.
Nashukuru sana ndugu ,nitabadirika ila nina mambo mengi kichwani .

Natoka sehemu ambayo ni almost safari ya masaa mawili kwa gari mpaka nafika hapa mbalizi

Jana nilimkumbuka sana wife ,nikawa natamani walau hata nipige simu apokee ila hakupokea nikiwaza kumfuata alikoolewa naogopa maana jamaa linaweza kuniua ,ikabidi nimfuate dada yake songwe ili ampigie walau nimsalimie na kumuuliza wanangu kama ni wazima .

Dada mtu naye kanitoa baru kwake ni hapo laki na nusu nikaona niende nikainywe ,sikubahatika kutembea na corolla yangu maana hali ya hewa huku ni mvua sana nilihofia kukwama .

Najieleza hivi ili nisinukuliwe vibaya sana kama napenda haya ,daktari nashukuru kwa maneno yako nitabadirika ndugu .
 
Kaka nakumbuka uli sema una itaka tuzo ya mfanyakazi bora, ila jitahidi upunguze na wenzio ni watu ujue 😁😂.

Yaani saa kumi uko macho?
Na hili ndilo linaloniuma alfajiri yote hii nawaza ikifika saa moja sijafika kazini nitakuwa sijawa wa kwanza kufika nitaanza kuweka alama mbaya .

Kaka nawaza mengi na roho inauma
 
Nashukuru sana ndugu ,nitabadirika ila nina mambo mengi kichwani .

Natoka sehemu ambayo ni almost safari ya masaa mawili kwa gari mpaka nafika hapa mbalizi

Jana nilimkumbuka sana wife ,nikawa natamani walau hata nipige simu apokee ila hakupokea nikiwaza kumfuata alikoolewa naogopa maana jamaa linaweza kuniua ,ikabidi nimfuate dada yake songwe ili ampigie walau nimsalimie na kumuuliza wanangu kama ni wazima .

Dada mtu naye kanitoa baru kwake ni hapo laki na nusu nikaona niende nikainywe ,sikubahatika kutembea na corolla yangu maana hali ya hewa huku ni mvua sana nilihofia kukwama .

Najieleza hivi ili nisinukuliwe vibaya sana kama napenda haya ,daktari nashukuru kwa maneno yako nitabadirika ndugu .
Mioyoni tumebeba MENGI YATAKUTOA MACHOZI...usione watu wanapitapita mtaani ukadhani wanaraha.

Najua hisia za kum miss mtu / watoto familia Ina uma Sana.

Jf ni familia yetu tuna share tuna communicate pole sanaa mkuu everything will be okay.
 
It will never be ok kaka ,nishaachwa kukubali imekuwa shida .

Lakini nitakuwa na muda wa kujitafakari tena nahitaji kuanza tena maisha yangu nayaona yakipotea mikononi mwangu
 
Back
Top Bottom