nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,106
- 12,916
Naam madereva tuliishi kama ndugu, tulikuwa na umoja na Upendo wa kweli tuliishi kifamilia zaidi...Mkurugenzi/ mmiliki kila weekend kama tumerudi (Kwa sababu kampuni yetu tulikuwa tunapakia pamoja tunasafiri pamoja na kurudi pamoja), alikuwa na utaratibu wa nyama choma yard.
Nyama za kutosha na nyingine tunabeba nyumbani, siku za ijumaa baada ya swala ya mchana wote tunajumuika pamoja majris juu ghorofani tunakula mandi mbuzi au mandi kuku(ni chakula mfano wa pilau).
Ikawa usiku ikawa mchana, Mungu jaalia Kampuni ikakua ikaleta malori 80 kwa pamoja...duuh hapo ndio balaa na mitihani ikaanza kuongezeka kwenye kampuni, kila mtu akirudi safari anakuta kuna kesi ofisini mara hili mara lile.
Maneno yakaanza kuwa mengi kuliko kazi.... Mkurugenzi akawa kama kachanganyikiwa hata ofisini akawa hafiki madaraka akamkabidhi muhindi wa India ambaye umeneja ulimshinda kwenye moja ya Kampuni ya Mkurugenzi Malawi. Utaratibu wa nyama choma ukafa ......kula mandi ikawa historia chuki na magomvi baina ya madereva ikaanza hasa madereva wageni.
Majungu, husda, visa na fitina zikakomaa....ushirikina ukawa unafanyika waziwazi, baadhi ya kiongozi akategeshewa sumu kwenye chakula na kupoteza uhai ndani ya Yard,,,,balaa ikazidi kukomaa,,,,,,uzuri wa Kampuni ukafubaa......
Yoote yakawa Historia......Wenye kuona mbali tukaona ni wakati muafaka wa kuondoka kwa amani,,,,,baada ya kusoma na kuelewa ALAMA ZA NYAKATI........