Tulikuwa tunaambiwa USA inaendeshwa kitaasisi na si maamuzi ya mtu mmoja. Mbona sasa tunashuhudia vituko?

Mbona mi naona ni yaleyale isipokuwa ilikuwa inafanya vitu kwa kinyago cha mbuzi sasahivi inafanya vitu kwa kinyago cha chui ila simba ni yuleyule!, sikuzote marekani husimama upande wa faida haijalishi atakuja na sura gani!.
 
Opinion zako sio ushahidi. Ulichoandika ni nafsi yako na sio Sheria yoyote ya Usa.

Mimi nimeweka kesi ya kwanza ambayo Tayari Trump Ameshashindwa, kama Alikua sahihi kwanini kashindwa? Na kesi sio moja zipo nyingi tu.


Hii nyengine.

So anachofanya Trump ni kutumia mabavu tu sasa hivi na kukiuka Amri za mahakama.
 
Duh!...kwamba Trump ni mvunjifu wa Katiba?...
 
Duh.!.ubeberu wao ni kiwango cha juu mno....yaani wenye nguvu/fedha ndio wanafaidi.
 
Mkuu wengi tuliaminishwa hivyo mpaka majuzi tulipoyaona haya.
 
Yani USA sasa haina tofauti na nchi za kiafrika maamuzi yanatolewa na mtu mmoja tu
Rais wa Ukraine kamtolea nje deal lake la kumsainisha kujichotea madini ya Ukraine, kamfanya adui na kuendesha kampeni ya kumwondoa madarakani. 😳
 
Maamuzi anayofanya Trump YAPO ndani ya mamlaka yake kama Rais, mimi na wewe pamoja na wamarekani Gen Z tunaona ajabu kwasababu ni kwa muda mrefu rais hajawahi kutumia mamlaka yake namna hii
Sawa kama ni hivyo lakini najiuliza ni kwa nini marais waliomtangulia hawakufanya anachofanya yeye leo hii? Walipotezea kwa ajili ya masilahi mapana ya marekani au ni kwa kutokujuwa?
Zamani nilifikiri kabla marais hawajakutana kwa ajili ya kukamilisha deal fulani kuna wasaidizi wao wanakuwa wameshakaa na kukubaliana kila kitu then marais ni showoff tu ya kukubaliana na kusaini, lakini sio nilichokiona juzi pale WH.
 
Kila anachofanya Trump kiko ndani ya mamlaka yake....HAVUNJI SHERIA WALA HAKANYAGI KATIBA. Ni sawa tu leo hii mama Abdul asaini mfungwa kunyongwa,walio wengi watashangaa humu...
 
Chadomo huwaga ni roporopo wanaweza kudanganya wajinga tuu.

Rais ndio Kila kitu kwenye Nchi yeyote hakuna Cha Katiba Mpya Wala ya zamani.
 
But ataangukia pua very soon kama akiendelea na haya maamuzi yake, within 100 days but alot of disasters
 
Watashangaa vipi wakati sheria ya kunyongwa ipo?

Kila anachofanya Trump kiko ndani ya mamlaka yake....HAVUNJI SHERIA WALA HAKANYAGI KATIBA. Ni sawa tu leo hii mama Abdul asaini mfungwa kunyongwa,walio wengi watashangaa humu.
 
Kavizuia kwasababu katiba inamruhusu kuvizuia , angekuwa kavunja sheria kwa kufanya hivyo tayari wapinzani wangeanza zengwe la impeachment ili aondolewe
Nalo hilo la impeachment linawezekana kama ndani ya siku 100 tu za utawala wake ndio haya tunayoyashuhudia mbeleni tunaweza kuliona hilo la kumtaka aondoke madarakani.
 
Kiranga Nguruvi3 Mag3 Nyani Ngabu
 
Wewe unafikiri matamko ya trump yapo kikatiba na ni kwa maslahi ya marekani au anajitamkia tu kama huko kwenu kwa kusadikika?
 
Basi mfumo wao wa uongozi ni mbovu sana!

Kwahiyo pale alipo anaweza hata kuamuru kubonyezwa kitufe cha nyukilia kulipua nchi flani bila kuingiliwa na yeyote.
unataka Rais awe na madaraka sawa na mbunge??
ndivyo ulivyokuwa unaitafsiri demokrasia??
 
Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN. Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
Trump anawaumbua Wazungu kwa unafiki wao. Wakome sasa kutulecture sisi kuhusu democracy na waanzie kwako

Yaani mtu mmoja anaibuka na tamko tu au Executive Order moja tuu na kila Muhimili unaufyata kimyaaa

Sasa hivi amefuta msaada kwa nchi ya Ukraine kwa kutoa tamko tu wakati misaada mingine ilipitishwa Senate
 
Hizo zilikuwa ni propaganda za kumdidimiza Magufuli.
Ila utashi wa Rais ndio unaongoza nchi.
Huyu wetu kasema tule kwa urefu wa kamba.
Na tunakula kweli kwa urefu wa kamba, km angesema vinginevyo pia tungefuata tu.
 
Mpaka sasa yote ambayo kayafanya yanaangukia kwenye mamlaka yake ya kiraisi.

Hajafanya jambo lolote lile lililo kinyume na katiba, kwa mfano, hajapiga marufuku vyama vya kisiasa kufanya shughuli zao kisa uchaguzi umeisha. Hajakataza watu kuamini wanachotaka kuamini.

Hajafungia chombo chochote kile cha habari, si gazeti, kituo cha runinga, redio, wala kumfunga mwandishi yeyote yule wa habari.

Hajaingilia taasisi zingine zozote zile zilizopo chini ya matawi ya serikali, i.e., bunge na mahakama.

Majuzi hapa kamwondoa mkuu wa majeshi pamoja na viongozi wengine waandamizi wa jeshi. Mamlaka hayo anayo kikatiba.

Hivyo hajavunja katiba.

Yeye ndiye mkuu wa tawi la utendaji [executive branch] na kwa msingi huo, anayo mamlaka kiutendaji.

Sasa akitenda, ni kipi ambacho anakiuka?

Labda ni uelewa mdogo wa jinsi ambavyo Marekani inaendeshwa ndo maana watu mnafikia mahitimisho kimakosa….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…