Tulioangalia Kombe la Dunia mwaka 1986 nyumbani kwa Sheikh Yahya Magomeni tukutane hapa

Hongera Sana kwako mkongwe. Nakiri kwamba umenizidi fainali moja tu katika maisha yangu. Mungu kanijalia kuangalia Kombe la Dunia Tangu fainali za 1990, Argentina ikifungwa na German Kwa penalty ya dakika za mwisho iliyopigwa na Andreas Brehme. Argentina wakipinga penati hiyo Kwa Muda mrefu wakiongozwa na Maradona. Watu wengi wakiamini kocha atamteua Lothar Matheus kupiga penalty ile, ghafla kocha anamwita pembeni wakati Argentina wakiendelea na ubishi na kumwagiza penalty ipigwe na Brehme.
 
Ile Argentina ya kina batista, huyu alikuepo jana
Maradona aliibuka mchezaji Bora 1986
Kuna mwamba anaitwa Gary lineker wa uingereza[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Gary Lineker, a fair play player ever.
 
Nakumbuka mwaka huo na Wasomali walitunga wimbo kuwasifu Argentina
Zamani mpira ulikuwa ni Hamasa haswa dunia nzima haijalishi ni nani ili mradi wanacheza vizuri
 
Mwaka 1990 luninga zilishaanza kuwa nyingi, halafu anaibuka mjinga mmoja anasema Mzee Ruksa hakufanya kitu.

Mwaka 1986 hata mwaka ulikuwa haujatimia tangu Mwinyi aingie madarakani ndio maana hali ilikuwa hivyo.

Tumetoka mbali

Wacha uongo wako, zilikuwa nyingi aapi? Usitukuze vitu vya kijinga na ambavyo havikuwepo!
 
Hiyo mechi naikumbuka ilikuwa ni kama kipindi cha pili cha fainali ya 1986 maana final contenders walikutana tena.enzi hizo mechi zilikuwa wa msisimko wa aina yake
 
Hiyo mechi naikumbuka ilikuwa ni kama kipindi cha pili cha fainali ya 1986 maana final contenders walikutana tena.enzi hizo mechi zilikuwa wa msisimko wa aina yake
Uko sahihi. Ilikuwa ni kama marudio ya 1986 Mexico.
 
Ujerumani ya Magharibi kipindi hiko ilikuwa na mchezaji hatari sana Matthaus.

Alimkaba sana Maradona, hivyo Barrachugga ndiyo akawa hatari sana upande wa Argentina, fainali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…